Asalaam Aleiykum
Pata fursa nzuri ya kuijua Milango hii minne ya Dhanmbi inayotutesa sisi Walimwengu mpaka tukawa tunaishi bila ya Raha, tunaishi na Maradhi ya Dhanmbi, tunaishi kinyume na sheria za Ulimwengu huu, na sababu kubwa ni kupita kwetu kwenye Milango hii na kuingia kwenye hicho chumba chenye kuishi Dhanmbi.
Vipi tunaingia katika chumba hicho ndio chanzo cha darsa ya leo, Na dhumuni kubwa ni kukufanya usiwe unatumia milango hii kuingia kwenye hicho chumba.Labda tukikuonesha Alama na kukwambia (No Entry)pengine Mja unaweza kuepuka mateso na maangamizi yaletwayo na Dhanmbi.
Dhanmbi ilikujaje?, Ilikuja ili kutizamwa Mwanaadamu utamtii Mollah wako pale utakapo kula tunda la kujua, ndio maana kabla ya kula tunda hili unakua huna dhanmbi, na muda mchache baada ya kula unapata bahati ya kusamehewa, lakini matatizo yanakuja ukenda kuchuma tena au kuendelea kuishi kwenye bustani hii ya Dhanmbi.
Nini Dhanmbi?
Ili usije ukajichanganya kwenye ufafanuzi wacha nikupe tafsiri ya neno dhanmbi, Dhanmbi ni makatazo yote yaendayo kinyume na sheria za Mwenye enzi Mungu, Hapa nimetaja makatazo ili usibabaishwe na tafsiri ya neno Maamrisho, (Maamrisho na Makatazo)ni maneno mawili tafauti.
Naam hiyo ndio Dhanmbi, Sasa vipi unaingia?. ili kujua vipi unaingia itabidi kama ilivyo kawaida yetu tuombe muongozo au tusome aya ndani ya (Quraan) ili itujulishe kitu kilichomo ndani ya Bahari hii ya (Milango Minne ya Dhanmbi), na utakapo pata fahamu za kuelewa sababu zake hapo tena utachukua hatua za kujiepusha au kutumia milango hii ya dhanmbi.
Napenda kukumbusha tena jumba hili japokuwa lina milango minne lakini lina vyumba vingi, kuna vyumba vya Haram ambavyo ndio (Dhanmbi) na kadhalika kuna vyumba vya Halali ambavyo ni (Thawabu) na vyenginevyo. Hapa leo tunashughulika na vyumba hivi vya (Dhanmbi) na aya ya ukumbusho inasemaje kuhusiana na kadhia hii ya Milango.(An-Nisaa-17)
إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ۬ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ۬ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡہِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَڪِيمً۬ا
"Toba Inayopokelewa na Mwenye Enzi Mungu ni ya Wale wanaofanya uovu(Dhanmbi)kwa Ujinga, ikisha wakatubia kwa upesi, hao ndio Mwenye Enzi Mungu huipokea Toba yao, Na Mwenye Enzi Mungu ni Mjuzi na Mwenye Hekima".
Kitu cha mwanzo kabisa napenda nikujulishe kuwa daima (Ujinga unambatana na Werevu) aya inayofatia ya (18)ikaendelea na kusema.
وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّى تُبۡتُ ٱلۡـَٔـٰنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ ڪُفَّارٌۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمً۬ا
"Hawana Toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemhudhuria mmoja wao, Akasema, Hakika mimi sasa natubu, Na (Hawana Toba)wale ambao wanakufa katika hali ukafiri, hao tumewaandalia adhabu iumizayo."
Sasa nini kinatokezea kutokana na meneno yaliyomo kwenye aya mbili hizi, ili kupata faida zake endelea part 2
Sunday, May 1, 2016
MILANGO MINNE YA DHANMBI PART 2
Asalaam Aleiykum
Tunaendelea kufanya utafiti wetu wa kuiepuka Milango hii ya Dhanmbi, Na sasa inatubidi turejee nyuma ili kuitizama ile aya ya (17)ilipotaja neno ujinga, Hapa ujinga kusudio lake ni (Innocence) Kitu ambacho hukijui, huna (Experience)nacho, basi mwanzo kabisa ukitoka kwenye Msitu wa ujinga unaingia katika Mlango huu wa kwanza (1)unaoitwa kujua, jambo lolote lazima kwanza lipitie Mlango huu wa kujua, Na kujua huku kuna(Level)zake, Mnyama ana (Level)yake, Mti una (Level)yake, Mwezi una (Level)yake, Mpaka huo Mwili wako una (Level)ya fahamu zake, sasa hivi usage chakula, Sasa hivi uzidishe (oxygen), Na hiyo Roho yako hali kadhalika ina desturi ya kukusanya Ujuzi au ita Kujua, Na imepewa (level)hii ya juu kabisa na Mwenyewe Mollah Muumbaji, inapokwisha kukamilisha kazi yake kwenye Mlango huu wa ujuzi ndio hapo inapeleka taarifa hizo kwenye Mlango wa pili(2)wa (Experience)Pahala hapa kapewa Mwanaadamu ili apate uyakinifu au ladha ya mambo, katika Mlango huu wa pili watu wengi ndipo tunapopata matatizo, mambo yote yako hapa, unapotoka ujingani mwanzo unaishi hapa.
Basi ikitokea umetosheka napo kwenye Mlango huo ndio sasa unaelekea kwenye Mlango wa tatu(3)ambao ni (Memory)unapoweka Akiba yako ya matendo, Na hapo ndio unakua simjinga tena.
Kujua kwako huku kunakufikisha katika sehemu ambayo sasa unayo (chance)au nafasi ya kusamehewa, Mpaka hapa inakubalika ulifanya kuwa ulifanya kwa Ujinga ulokua nao, baina ya kufanya na kujua unapatikana uzoefu ambao ndio hiyo safari ya kutoka kwenye kiza kwenda kwenye Nuru, Na hiyo ndio (Education), ukimaliza hapo ushakamata (Certificate)yako ndio unaingia Mlango wa (4)Matendo(Action)Mlango wa kusudi,Hapo sasa ndipo zinapoanza (Dhanmbi) ni Mlango unokurejesha kwenye kumbukumbu au (Memory)ambayo ndio hiyo (Action). Hapa ndipo pale waswahili wakasema(Umeonja zabibu)utamu unakurejea tena, sasa unafanya matendo yako kwa makusudi, na hapo ndipo unapoanza kuandikiwa (Dhanmbi)na hapa ndipo hapapatikani tena msamaha. Sasa Kiumbe ufanye Nini? Endelea part 3

MILANGO MINNE YA DHANMBI PART 3
Asalaam Aleiykum
Katika Mlango huu ndio unafanya mambo kwa Ubabe wako wa akili, Unafanya hujuma na Fisadi katika Ulimwengu huu ukiwa umejipa Mwenyewe kidonge cha Usingizi, na Kidonge hichi jambo la mwanzo lina kusahaulisha kuwa wewe umeumbwa na Muumbaji yuko, Unaanza kudhulumu Haki za Watu, unafanya Fitna, unafanya uzinifu na mambo chungu nzima, na kubwa zaidi unajisahau hata kama unafanya Dhanmbi, ukifikia katika hali kama hiyo unatakiwa uchukue tahadhari kubwa sana, au unaweza kukumbwa na balaa kubwa siku ya kurejea kwa Mollah wako.
Aya imeweka wazi hakuna msamaha kwa yule anoendelea kutenda dhanmbi(Action)mpaka akasubiri keshakua mtu mzima mate yanamvuja mdomoni hawezi kuyazuia tena na anaona mauti yashawasili ndio anasema Mungu wangu sasa nishachoka , jeuri imenisha, sasa nataka unisamehe, hakuna msamaha wakati huo, umri wako wote ufanye jeuri ikisha sasa hivi kwa sababu unataka kunyakuliwa ndio unasema nisamehe, aya imekataa kabisa kwa yule alotenda Dhanmbi au yule anokufa (Kafiri) hataki kumuabudu Mollah wake.
Basi ikiwa ushaijua Milango hiyo Minne na bado una nguvu zako ni bora ukurupuke sasa hivi, jihadhari sana na huu Mlango wa Nne uwe huingii tena, Kiepuke chumba hichi cha dhanmbi ili isije ikakukuta Balaa, na Hilo ndilo Jumba letu la (Akili) lifanyalo kazi yake, kwa wale wenye kufahamu watazinduka na kuwacha kutawaliwa na Akili na mambo yake ya kurejea rejea matendo ya dhanmbi, kumbuka dhanmbi umekwisha zitenda nyingi, ufanyavo hivi sasa ni kuzirejea tena na tena, kwa hiyo kama umefahamu basi zitakie Msamaha kwa Mollah wako na kufanya yalo mazuri, nenda kaingie kwenye vyumba vya mazuri, Kwani matendo mazuri yanafuta mabaya yako, Na utaona kidogo kidogo Mollah wako anaanza kukupa furaha na afya njema, pia na tahfif na ziada katika riziki zako. Mollah wetu tujaalie yaliyo mazuri na uturuzuku yalo mema.

Subscribe to:
Posts (Atom)