Maswali na Majibu Yaloulizwa

Asalaam Aleiyku,

Kwa yoyote yule mwenye kutaka swali lake liwe (Private)basi naomba awasiliane na mimi kwa njia ya (E-Mail)ambayo utaipata kwenye sehemu ya wasiliana na mimi, Mwenye kutaka na wengine wafaidike aendelee katika sehemu ya uliza swali lako ambalo jawabu lake tutaliweka ukumbini.




SWALI(1)ASLM-ALKM: Shk, mimi nimeota navaa viatu nini maana yake? Alkm-mslm:Maana ya ndoto yako inaashiria utasafiri miezi ya karibu. Mollah wangu anajua zaidi.................... SWALI(2)ASLM-ALKM:Shk, kwanini masheikh wanatoa fatwa tafauti ambazo hazimo kwenye Quraa'n na zinakubalika? Alkm-mslm:Wanategemea ile hadith sahihi ya Bwana Mtume s.a.w alipomteua Muaz Ibn Jabal kwenda kuwa Gavana wa yemen alimuuliza vipi utahukumu utakapoletewa kesi, akajibu kwanza kabisa nitatumia Quraa'n,na kama sijapata jawabu kwenye Quraa'n basi nitafata sunna na kama sikupata kwenye sunna jawabu langu basi nitatumia akili yangu,Bwana Mtume s.a.w akafurahi na kukubali rai hiyo. Mollah wangu anajua zaidi..................... SWALI(3)Asalaam Aleikum. Swali sheikh, mimi swali langu nimeulizwa na wanafunzi wenzangu ambao sio waislamu nahisi kama walikua wananifanyia dhihaka,mimi nimesoma dini yangu sana lakini swali hili limenitatiza, swali lenyewe ni hivi, ilikuaje ikiwa Mwenye-enzi-Mungu anajua Mtume s.a.w hajasoma halafu akampeleka Seyyidna Jibril a.s akamwambie Mtume s.a.w asome. Jawabu:Asalaam Aleiykum, Namuomba Mollah wangu anipe ufahamu nikujibu kwa kukutosheleza.Kwanza kabisa yaonesha hili swala si lako wewe ikisha umetumia neno (mimi nimesoma dini yangu sana)ningekushauri usitumie neno hilo mimi nimesoma sana,kwani neno hilo linaonesha udhaifu mkubwa juu ya ufahamu wako.Ukisema umesoma mimi nafahamu ni kijana alojaza (information)tele kichwani mwake)hiyo ndio maana ya kusoma. Ama kuhusu swali lako kwanini Sayyidna Jibril a.s akamwendea Mtume s.a.w na kumwambia asome ni kutokana na Nature yetu wanaadamu tunazaliwa na kujua,Yakua tushafundishwa kutokea kwa baba yetu Nabii Adam a.s .Utaona wanaadamu mambo mengi tunayajua bila ya kufundishwa na yoyote na hiyo ndio kusudio Sayyidna Jibril a.s akamwambia "soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba"Maumbile hutaki kusomeshwa Mwezi,Jua,Nyota na kadhalika hutaki usomeshwe unaviona labda utalotaka uvitie majina tu.Hilo ndio kusudio lakuambiwa soma kwa kuwa kashajua vyote, kashafikia umri wa Hekima miaka Arobaini,hakuambiwa fundisha ila kaambiwa soma, na namalizia kwa kueleza kuwa kusudio hapo si elimu ila ni hekima ndio maana aya ikasimama kwenye "akamfundisha mwanaadamu chungu ya mambo asoyajua"hiyo ndio jawaabu ya swali lako.........................


Swali la ndoto:
Aslm Alkm. Sheikh, Mimi nimeota ndoto nipo Bandarini na meli inakuja, unaweza kunambia maana yake?

Jawabu:
Alkm Mslm: Maana ya ndoto yako, Tarajia kitu kipya(Au maisha mapya)yanakuja upande wako.Mollah wangu mjuzi zaidi wa hilo.


Swali:
Aslm Alkm
Nimekamata txt massage katika simu ya mume wangu, na mimi na mume wangu tumezaa tuna watoto wawili nataka kudai talaka naruhusika kidini?

Jawabu:
Alkm Mslm: Huruhusiki kabisa, na kwanini udai talaka sababu ya kukamata maneno yaloandikwa kwenye simu, Napenda uelewe katika ndoa kuna misukosuko, kuna raha zake na kero zake, kuna wakati wa shida pia na wakati wa raha, kuna Rehma pia zinafatia na Neema, basi kwanini maneno tu yakuvunjie nyumba yako, na sio nyumba yako pamoja na kuwapa mateso watoto wako waje kuishi bila ya baba yao, jaribu kuzungumza na mumeo mjulishe vipi (hisisa zako kuhusu hiyo Massage)na vipi inataka kuharibu nyumba yenu, yeye binaadamu asaa anaweza kuzinduka akalinda ndoa yake.


Asalaam Aleiykum,

Swali

Assalam aleykum, napenda kupata ufafanuzi ktk Quran na Hadith ikitokea mtu kasimamisha msikiti kwa njia ya RIBA na waumini wasilijue Hilo mpaka uliposimama. Nini



Jawabu

Hilo hapo juu  kwangu mimi ni swali, lakini kwako wewe ni mwenye kutaka ufafanuzi, kwa hiyo Shk wangu inaonesha kadhia hii umeshaijua unalotaka mimi nikuchambulie zaidi, na mtu ukiwa na jawabu ndio maana unashindwa kuuliza,Umesema ikitokea mtu kasimamisha msikiti, mwanzo wa kutokea lazima ilikua hayupo ndio maana akatokea,ikisha akasimamisha msikiti kwa njia ya Riba, Vipi anaweza kusimamisha Msikiti kwa njia ya Riba?Ima kachukua pesa za Riba au Kanunua kwa njia ya Mortgage, moja katika hilo linawezekana, Na umesema waumini wasilijue hilo mpaka uliposimama, aidha wamejua kabla au hawajui kabisa kwani umewataja waumini, waumini hawana sababu ya kuhoji nyoyo zao huwa zimeridhika, wanatoa na kusali pasi na wasiwasi sababu ndio msikiti ushasimama, shaka hii yote wanamuachia huyo alosimamisha, Ikiwa Pesa kapata London au kwengineko hiyo inakua ni hiari ya huyo alosimamisha.
umemalizia kwa neno nini, hilo siwezi kulijua maana yake. Ila maana ya Riba ni haramu na haifai iwe kwa mtu au kwenye Dini hairuhusiwi na wala hilo halitaki ufafanuzi. Natumai umeridhika.

Shukran Mollah wangu ndie ajuae zaidi



Asalaam Aleiykum
Swali

assalam alaykum warahmatul llah wabarakaatuh.
amma baada ya salam,sheikh swali langu mie ni kutaka kujua kutokana na hizi aya 2 za qur an.
1. quran (2:34)
2. quran (52:17),aya hyo ya kwanza Allah anawataka malaika wamsujudie adam,na wote wakasujudu isipokuwa ibilisi.aya ya 2 quran inaeleza kuwa malaika waliobeba arsh ya Allah wapo8.sasa swali langu ni:-
je!kusujudu kwa walivyoamrishwa malaika ni kama huku tunavyosujudu sisi?na kama ndio,hawa malaika8 walisujudu vp haliyakuwa wamebeba arshi ya ALLAH?.kama siyo hivyo je walisujudu vp?. nimeuliza hivyo ili nipate kufahamu, kama nitakuwa nimekosea namuomba ALLAH anisameh,
assalam alaykum.



Jawabu

Mwenye-enzi-Mungu anapotaka kuwasiliana na viumbe vyake inabidi atumie lugha, na inapotumika lugha kwa kila atofahamu anafahamu kwa tafsiri ya aina alivo fahamu  yeye,  lakini kutoka kwa Mollah wako, maana inabakia ni ile ile.
Nini Kusujudu? kusujudu ni kitendo cha (humble-surrender)ni kupotea kwa unyenyekevu na kukubali kwa ridhaa pasi na upinzani kwamba umekiri ndani ya nafsi(kuhusiana na Utukufu)au vitendo ambavyo vimekuzidi katika kila hali.
Sasa Najibu swali lako la Vipi Malaika walisujudu.Umesema wamesujudu kama sisi, hapo itakua umenijulisha mimi na wewe kukubali ya kuwa Malaika wana umbo kama la Binaadamu, hilo haliwezekani kwa kuwa tumeumbwa tafauti na sisi hatulijui umbile lao, kwa hiyo iondoshe dhana ya kusujudu kwa kitendo kama hichi tufanyacho sisi, sijida yao wao ilikua ile ya (Humble-Surrender)kama inavoonesha mwanzo wa kisa chenyewe katika Al-Baqarah aya ya 31-34, mpaka mwisho wake, kwa hiyo kiufupi ni kitendo cha (Elimu)kilichowazidi ambacho waloambiwa wakikubali na kitendo hicho mwisho kina mrejea yeye mwenyewe Mwenye-enzi-Mungu, Na Malaika kukubali  hilo tendo, Na kukubali kwao hao Malaika  ndio hiyo Sijida yenyewe.
"وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَہُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِى بِأَسۡمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَـٰدِقِينَ (٣١) قَالُواْ سُبۡحَـٰنَكَ لَا عِلۡمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمۡتَنَآ‌ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ (٣٢) قَالَ يَـٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئۡهُم بِأَسۡمَآٮِٕہِمۡ‌ۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسۡمَآٮِٕہِمۡ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّىٓ أَعۡلَمُ غَيۡبَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَأَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ (٣٣) وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأَدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَـٰفِرِينَ

Shukran na Mollah wangu ndie ajuae zaidi.



Aslm Alkm,

Swali:  Nini Fadhila au Faida za Kumsalia Maiti?


Jawabu: Ana Hadithia Abu-Huraira R.A, "Amesema Bwana Mtume s.a.w""Yoyote yule alohudhuria Maziko akasubiri mpaka atakaposaliwa(Maiti) Basi juu yake kuna zawadi ipatayo (Qirat)moja Na kwa yule alohudhuria akakaa mpaka hiyo (Maiti) Kuzikwa basi juu yake kuna zawadi ya (Qirat) Mbili. Ikaulizwa nini hiyo (Qirat) Akasema Ukubwa wake kama Milima miwili. Na hii kaikubali Muslim na wengine.






Asalaam Aleiykum

Swali:Baada kusali sala ya isha lipi lililotiliwa mkazo au lilo bora zaidi kusali rakaa 2 za sunna au bora usali rakaa3 za witri? Kama kusali rakaa 5 unaona uvivuu,


Jawabu:Ama lililotiliwa mkazo ni kusali rakaa tatu 3 za witri ndio(sunnah muakkadah)Anahadithia Sayyidna Ali r.a"Mtume s.a.w alikua akisali sala ya witr" ikisha akiwaambia enyi mnoifata Quraan, Salini sala ya witr, kwani Mollah wenu ni Mmoja na yeye ni mwenye kuipenda witr".(An-Nasai,Ahmad,Abu Daud,Ibn Majah, Tirmidh, Na Al-hakim)wote wameitaja.




Asalaam Aleiykum,

Swali:Nataka kujua tafauti ya mambo haya mawili, (1)Tukipatwa na Janaba inatulazimu tukoge Josho kubwa, Lakini tukienda haja ndogo tuna nawa tu.
(2)Nguo zetu zikipatwa na matone ya mbegu za uzazi ikisha yakikauka tunafuta kawaida na maji na tunaweza kusalia nguo hizo, ila nguo hizo zikidondokewa na vitone vya haja ndogo yatupasa tuikoshe nguo nzima, naomba unielemishe mambo hayo mawili.





Asalaam Aleiykum

Jawabu:kuhusu swali lako la kwanza(1)Napenda ufahamu unapotokwa na Janaba ni kitendo kilichotokea katika mapitio ya Uhai,Ndani ya tendo hili yanatokea mambo mawili, kwanza unatoa Uhai(mbegu za Uzazi)halafu pili unapatikana Umauti wa hiyo mbegu ya (Uzazi)kwa hiyo viwili hivyo vinakwenda (deep)mwili wako unakua na harufu isiyo nadhif kwa (Roho)na binaadamu wenzio, na la pili ni Kuurejesha Mwili wako katika hali ya Uhai na (Ufresh)kama ilivosema aya "tuka jaalia maji kwa kila chenye kuishi"na heshima hii hupewa Maiti kabla ya kuzikwa(Kuoshwa) kutokana na wao pia wanapitia (process)hiyo hiyo kutokea kwenye uhai kwenda kwenye Mauti.Ukenda haja ndogo una nawa sababu ni sehemu moja tu ndio ilotokea hiyo haja, na ufanyacho ni kuondosha harufu na uwe nadhif, lakini katika kadhia ya janaba inapatikana mashirikiano ya mwili mzima unashiriki katika tendo hilo, lakini wengi si wenye kuelewa.
Na sehemu yako ya pili(2) kuhusiana na nguo nikuwa, mbegu za uzazi zikishatoka na kukauka zinakua hazina tena harufu lakini mkojo harufu inabaki ndio maana ukaambiwa uzisafishe nguo hizo na kwa kuwa utakua hujui vitone hivyo vimedondokea wapi.





SWALI

A. Alykum naomba ufafanuzi kuhusu gelatin. Cause tunaambiwa mostly ni animal protein, lakini suali langu kama haikua specified vipi tuishie kusema ni pig protein?


JAWABU.Asalaam Aleiykum,
Kuhusu ufafanuzi wa suali lako, kwanini tuishie kusema ni pig protein inatokana na dhana ya kuwa pig protein ni rahisi na mifupa yake ni yenye kupatikana kwa wepesi pamoja na ngozi yake, lakini ngombe, kuku, au farasi inakua tatizo kupatikana, ngombe na kuku watu hawaachi hata mfupa, na farasi si mwenye kuliwa sana, kwa hiyo tumebakia na huyo pig,huyo ngozi, mifupa nk, si venye kutakiwa sana ndio vinaishia katika matengenezo ya hiyo Gelatine, na sisi ndio tunaishia kudhani ni pig protein




Swali:
Assalam alaykum warrahma tullahi wabarakatuh...samahi kwa usumbufu nilikuwa nna swali na hili swali ni muhimu naomba unisaidie kulitatuwa...mimi naitwa (Jina limehifadhiwa) na muislam Sunni nimefunga ndoa na mwanamme ni Shia lakini la ajabu kwamba hii ndoa Wakati tunaisoma nilikuwa mimi na yeye tu hakuna mtu yoyote amesema haihitajiki mtu yoyote kwa kuwa hii ni ndoa yangu ya pili na nilisema maneno Kama haya zawajtuka nafsi alaa sidaqi maalum na yeye akajibu kabiltu tazwija...na baada ya hapo akasema ya kuwa tayari mke na mume....naomba unisaidie maana sina uhakika na hii ndoa Kama iko valid au tunafanya haraam?? Na nimesoma mengi ya kuwa wanasema Shia sio waislam ni kafir je ni kweli? Na mengi yanasemwa kwamba ni wanafanya shirk je ni kweli? Na hairuhisiwi Sunni kuolewa na Shia ? Tafadhili nisaidie kwa majibu nimekuwa na wasiwasi na hii ndoa na sitaki kuumudhi Allah....jazaqaAllah Kheir


Jawabu:
Asalaam Aleiykum, katika kujibu swali kuna njia mbili ama ujibu swali au umjibu mwenye swali, na mimi hapa nimeamua kumjibu mwenye swali, "katika maulizo yako umetia neno la ajabu katika ndoa hii wakati tunaisoma tulikua mimi na yeye tu hakuna mtu yoyote, amesema hahitajiki kwa hii ni ndoa yangu ya pili", ulipotumia neno ajabu, ujue lina maana mbili, maana ya kwanza ni mshangazo(kushangaa)kwa jambo jipya, na maana ya pili kubeza au (Kutoridhika)mbona kawaida ya mwanzo haikufanyika, kwa hiyo ajabu ya kwanza umeshangaa, na ajabu ya pili umejua kipo kilo kosekana lakini umeamua kuelekeza dhamana ya hiyo ndoa yako kwa huyo (Mume)Sasa jawabu langu kwako ulofanya si kosa kabisa inakubalika kisheria, lakini sheria inataka ikamilike, na hapo imokosekana ukamilifu wa Sheria yaani kuwepo kwa mashahidi, kwa sababu kusudio lote la hiyo ndoa ni (Legitimate Procreation)Kizazi cha halali na (Social Placement)Na nafasi ya (Heshima)katika jamii, ndio maana ukatakiwa na kusisitizwa ushahidi,ndio maana ikaitwa kufunga ndoa, wanajulishwa watu sasa huyu wangu, hakuna haja (mapaka shume)kumzungukia, Sasa kwa kuwa mefanya peke yenu chumbani hakuna asiyejua ndio maana umeshikwa na mawazo ya (Ajabu)kwa hiyo hayo yanaweza kuwa makubaliano lakini si ndoa kwa mwenendo wa Kiislam, kwani yalikuwepo hayo kabla ya uislam ndio maana nikayaita makubaliano(Kitab-Sharah Al-Bidayah)Na hivi ndio Waislam imekua desturi yetu tunapuuza, hatujui mpaka talaka inahitaji mashahidi kama ilivo ndoa na pia Maandiko yanatakiwa kama (Marejeo ya kumbukumbu)Na kumbuka Ushahidi haukai mdomoni.
Ama kuhusu maulizo yako ya Ziada kuhusu Madhehebu kwa hilo siwezi kukujibu kwani sina elimu ya kutoa Fatwa nani kafiri au nani Mushrik, kwangu mie wote viumbe wa Mwenye-enzi-Mungu na yeye ndie mwenye kuwajua.





Swali:
Asalm alaikum , kumuombea dua maiti au kufanya khitma baada ya siku 40 inafaa ?

Jawabu:Aleiykum Salaam,
Kwanini umewekee idadi za siku maiti, na kwanini iwe siku Maalum, inafaa kumuombea kila siku kama utaweza kumkumbuka maiti huyo, hakujawekwa idadi wala siku maalum, dua ni siku zote, kwa hiyo kila ukipata nafasi omba utapata wewe na huyo Maiti, na Mollah wako ni mwenye kuendelea kukulipa.



Asalaam Aleiykum.

Swali:

Assalam Aleykum, Natumai umzima ndugu yangu mimi huota sana napita sehemu watu wanakula wamejipanga na hata muda mwingine nami naingia nakula mara nyingi maana yake nini ? ila jana nimeota tofauti nimeota niko sehemu kuna nyumba nzuri sana na hizo nyumba milango yake iko wazi na chini ya nyumba hizo kuna zulia tuu, halafu kuna sahani zimepangwa chini yaani ni kama vile watu wameshamaliza kula na wameondoka na chini kuna tepe tepe za wali ila kuna sahani moja iko mbele kabisa imefunikwa na kawa maana yake nini Ndugu yangu? natumai utanijibu Masalaam

Jawabu:
Kuhusu sehemu yako ya mwanzo ya hiyo ndoto, ni mpangilio wa shughuli zako za kila siku, maana yakuona watu wanakula na wewe ukajiunga ukala, inaashiria kupatikana kwa riziki yako kwa njia ya kawaida unaipata kama wanavoipata wengine, ama kuhusu sehemu ya pili ya Ndoto yako ni kuwa wewe ni mwenye nia au kutamani vya juu zaidi, na hiyo ndoto inakuashiria njia zishafunguliwa ya hayo mambo mazuri na neema unazozitamani lakini itabidi kuzipata ufanye jitihada ya hali ya juu, Na mwisho ni kitandawili kimefunikwa kwenye kawa hakijulikani nini, kwa kuwa umeona chembe za wali yaweza kuwa utajiri au neema nyengine, hapo sijui kitu gani, mpaka ufungue hilo kawa ndio utajua, Na Mollah wangu anajua zaidi.


Asalaam Aleiykum,

Swali:
asalam aleykum bismilahirrahmani rrahiim swali la
ngu ni kua mimi nna mume tunaishi miji tafauti lakini hatuna maelewano kila nnapomfahamisha mwenzangu wana ndoa wanatakiwa kuwe hakuna siri baina yao tuwe tunazungumza kila kitu lakini yeye hataki kuzungumza na mimi kitu chochote na kama kuna tatizo hataki kukaa tukalizungumza lakini hutoka nje akazungumza na watu wengine matatizo yetu lakini mimi haniambii kitu sasa nakuomba unipe njia ya kuweza kuzungumza nae ili aweze kuniambia lile ambalo linamkera

Jawabu:
Umesema wewe na mumeo mnaishi miji tafauti, lakini mimi sijui makubaliano yenu ya kuishi miji tafauti, ila najua kama itakua makubaliano yenu ya kulazimishana kwa kusudi au kwa mazingira, basi meondosha Rehma ya ndoa na mapenzi, maelewano hayawezi kuwepo, na hilo linatokana na huko kuishi kwenu tafauti,kuhusu kuwa hataki kuzungumza na wewe kitu chochote, inaonesha mwenzio ana hamaki au chuki, kuna jambo kafanya au umemfanyia au mmelifanya ndio linamueka katika hali hiyo, na huko kutoka akazungumza nje na watu wengine, lazima mambo yamemjaa kifuani hana pakuyatolea au anajihami kabisa kwa jambo alolifanya au atakalolifanya, unasema mimi hanambii kitu inaonesha ana hasira katika moyo wake. Umesema nikupe njia za kumfanya ili aweze kukwambia linalomkera, siwezi kukupa muongozo sababu sijui mambo mengi ya hicho chanzo, sijui mna Family yaani watoto, sina popote pakuanzia hata nifikie kukushauri ufanye nini, lakini kwa kuwa umenambia nikupe njia, mie sitokupa ila nitakuonesha, mwambie arudi mje kuishi pamoja, kubali makosa japo hujakosea,mpelekee msg za mke mwenye kheri mwenye kutaka mumewe arudi ili muishi kama mwanzo.

SWALI:
Asalaam Alaikum Nilikuwa nataka Dua ya kujiangalia kwenye Kioo shukran

JAWABU:

 Ana hadithia Sayyidna Ali r.a "Bwana Mtume s.a.w" Alipokua akijitizama kwenye kioo alikua akisema""Namshukuru Mollah wangu"Mollah wangu nifanye niwe mwenye tabia njema""kama ulivonifanya kuonekana mzuri""Imekaririwa na Ibn sinni"

Anas r.a "Anahadithia""Bwana Mtume s.a.w akijitizama kwenye kioo alikua akimshukuru Mollah na kusema ametukuka Mollah wangu aliyeniumba na kunifanya mkamilifu, akaufanya uzuri uso wangu, na kunifanya mie miongoni mwa waislam

Swali
Assalam Aleykum, swali langu ni kuhusu kusali sala la Eid, je unasali vipi pamoja na salat Jumaa?maana nimesikia inasaliwa kwanza Eid then Jumaa alafu muda wa kusali Jumaa tunasali Adhuhuri, naomba ufafanuzi wako katika hili, Wabilah Tawfiq


Jawabu
Anahadithia Sayyidna Abu Hurayra r.a " Alisema Bwana Mtume s.a.w" Eid Mbili zimekutana pamoja leo(Fitr na Ijumaa)Ikiwa yoyote hataki kusali Ijumaa. Basi inatosha kwa yeye kusali (Sala ya Eid)"Lakini sisi tutasali Sala ya Ijumaa" Ukiwacha hakuna matatizo na ukisali kheri zaidi, Bwana Mtume s.a.w kakupa uchaguzi na wewe una hiyari yako kwa hilo, Haisaliwi Adhuhuri inasaliwa Ijumaa.

Salam Alaikum, Ya Sheikh.

Swali langu ni kwamba
Nini Hekma ya Moto na ubani katika dua?
Na je imethibiti au ni utamaduni tu wa Tanzania na Africa Mashariki.

Ahsante

Jawabu:


Umeuliza nini hekima ya moto na ubani katika Dua, itabidi kwanza nilijibu swali lako kinyume nyume kama ulivo liuliza, Ama hekima ya kuletwa moto ni kuuchoma huo ubani, na mambo yote yamo katika huo ubani na wala sio moto, Ubani una nini? kama mtaalamu wa kulijua Ua,utaona ukilikamata Ua linatoa harufu nzuri, lakini mkononi mwako una Ua, lakini hujaikamata harufu, Harufu inatoka kwenye Ua lakini inabaki kuwa ajabu,Ua unaliona harufu huioni,inapotokea harufu ndipo anapotokea mvuta harufu, kwa hiyo jawabu lako litakua hivi. Ile harufu ya Ubani inambatana na mambo ya ajabu yenye kuhusiana na Kiroho, ila mimi hapa sitoyataja hapa, ila nitakutajia yanohusu (Mind) Ubani unasaidia ku (sooth mind) inakuweka katika hali ya utulivu, inaondoa (tension) inasaidia mambo mengi katika Akili, ambayo kama utayafanyia utafiti utayagundua. Ama kuhusu kuthibiti hakuna ithabati yoyote katika kusoma dua, Na mambo hayo ya Ubani yameanzia huko Arabuni na India, huku Africa Mashariki tumefatia baadae, kiufupi haihusiani na Dua ila inahusiana na (Mind). Nadhani imetosheleza. Shukran

Swali.
Bismilahi rahman rahhim Alhamdulilah rabil-aalamin. naishukuru sana glob hiikwa kunitowa kwenye kiza na kuniwek kweupeni. pia natumai kwa uwezo wa ALLAH itanitoa kwenye ndoto na kuniweka kwenye mwamko. swali langu lipo hapa;Ni mambo/matendo gani mengine ninayopaswa kuyafanya yakati za usiku ukiachia kusali kusoma Qur-ani kwa ufasaha? Aidha hizo sala ni zipi na nitazisalije?

Jawabu.
Umeuliza matendo gani ufanye hizo nyakati za usiku baada ya kumaliza kusali, (Omba Msamaha kwa wingi), na pia umetaka kujua hizo Sala za usiku utazisali vipi, ni kama kawaida, Na utasali Rakaa 8, unasali mbili kisha unatoa salamu, halafu utamalizia na rakaa tatu za (Witr), katika hizo tatu, mwanzo utasali mbili utatoa salam, ikisha utasali moja na kutoa salam, jumla zitakua Rakaa 11, na uzuri zaidi kusoma Quraan kwa wingi ndani ya hizo Rakaa, unaweza pia kukamata (Mashaf)wakati unasali huku ukisoma. Shukran.

Amslm Alk

Maswali.

1. Je ni aina gani ya waliokufa mashahidi katika aina sita zilizobaki (yaani waliokufa kwa uzazi,kwa maradhi ya tumbo,kwa maradhi ya tauni,waliokufa maji,waliokufa kwa kuangukiwa na nyumba na waliokufa kwa kuungua na moto) wanaofutiwa ubora wa malipo baada ya wale waliokufa vitani?

2. Tunajua kuwa wanaokufa mashahidi kwa hadithi ya Mtume (S.A.W) ukiondoa wale waliokufa vitani wanaweza wengine wakawa si waislamu,Je nini hatma yao kwa Mwenyezimungu hali ya kuwa wamekufa katika vifo ambavyo vimethibitishwa kuwa ni vya kishahidi.

3. Je,Muislamu ambaye alikuwa hatekelezi ipasavyo maamrisho na Makatazo ya Mwenyemungu lakini akafa katika kundi mojawapo katika kundi la mashahidi sita ukiondoa waliokufa vitani,Je Mwenyezimungu atakuwa amemsamehe mazambi yake?

4. Mtu ambaye amekufa kwa uzazi yeye pamoja na mtoto wake,anakuwa na ujira gani kwa Mwenyezimungu ukilinganisha na yule aliyekufa kwa uzazi lakini mtoto akawa hai? 

5. Dua gani au kipi tunapaswa kukifanya pindi tunapodhuru makaburi ya marehemu wetu,hasa wale ambao tunaamini walikufa kifo cha shahidi.

6, Je kuna dua yeyote ambayo mtu unaweza kuisoma kumuomba M/Mungu akuonyeshe hali aliyokuwa nayo marehemu wako katika maisha yake ya akhera? hasa yule aliyekufa katika uzazi?

Jawabu

Ama kuhusu maswali yako ntachanganya jawabu la 1-4 ili nikujibu kwa pamoja usije ukapata mchanganyiko, kama nilivokujibu mwanzo kuwa Malipo ni kusamehewa Dhanmbi, lakini inaonesha unataka kujua wapi watakuwepo, au tunzo gani watapewa, kwani wale wa mwanzo umewajua wamepewa pepo lakini nini habari ya hawa makundi sita, nini wao watapata, Najibu tena hawa baada ya kusamehewa Madhanmbi yao itatizamwa ikiwa Mtu katika Uhai wake katenda Mema kafanya vitendo vya Thawabu basi Jaza yake atalipwa Pepo, Na kama atakua hajatenda yalomema basi atawekwa katika sehemu Baina ya Pepo na Moto inayoitwa sehemu hiyo (Aaraf)inakua huku hayupo na kule hayupo, na hapo ndio itakua makaazi yake.
Ama kuhusu swali lako tano, Unachotakiwa kuwasalimia na kuwaombea Malipo mema kutoka kwa Mollah wako, 
Swali lako la sita, Ni kweli kuna mambo unaweza kufanya na kuoneshwa hali ya Maiti wako, Jambo la kwanza itakubidi uwache kula chakula chochote chenye Roho kwa muda wa miezi mitatu, halafu kila usiku baada ya sala ya isha utasome sura ya Israa, na ukimaliza utasema maneno haya (Allahumma-Tawaffana-l-Hadith-ila-fulan ibn Fulan)mara tatu ikisha lala, Na Mwenye enzi Mungu akitaka atakuonesha hali ya Maiti yako.

Shukran. Na Mollah wangu anajua zaidi.

Aslm Alkm

Swali:


Nimesoma makala yako ya namna ya kukutana na nafsi yako. Imeniongezea elimu. Nauliza je, kuna hakika gani kuwa hicho nitakachokiona kitakuwa nafsi yangu kweli na si kiumbe kingine?

Jawabu:
Naam uliposema nimesoma nilikua na tamaa umenifahamu, lakini uliposema imeniongezea elimu nimekata tamaa, sababu elimu inakuzidishia mashaka, inakupa maswali bila ya jawabu, ndio maana ukauliza, kuna uhakika gani kuwa hicho nitakacho kiona kitakuwa nafsi yangu kweli na si kiumbe kingine, Ni kweli kama huna uhakika basi hicho kitakua kiumbe kengine, kwani kwenye nafsi yako hutaki uhakika, ina maana wewe hujijui kama wewe uhai, hivyo unataka mtu mwengine aje kukwambia wewe ni fulani, ukiona umebakia unauliza jee hichi kiumbe kengine basi jua bado hujakutana na Nafsi yako, kwani ukibakia unajiona tambua hiyo sio nafsi yako, ukikutana na nafsi yako utakua unajua kama ulivokua unajua sasa hivi niko hai bado sijafa, kwani ukilala unajijua kama umelala? siku utojijua umelala basi pia siku hiyo ndio utakua umekutana na Nafsi yako, inatokea mara chache kwa watu kidogo sana kujiona kalala kitandani, hicho kinachoona ndio nafsi yako, au kwa ufupi kile kinachoona ndoto ndio nafsi yako ambayo bado hujakutana nayo. natumai imetosheleza.

Shukran

Aslm Alkm
Naomba kuuliza tena: Umesema kuwa elimu huongeza mashaka, 1. je ili tusiwe na mashaka tusiwe na elimu? sijaelewa naomba ufafanuzi (2) naomba unifahamishe mana ya neno nafsi kwani inawezekana nashindwa kuelewa kwa sababu ya maana. 3. Je wanyama, wadudu na miti ina nafsi? 4. kuna tofauti gani kati ya nafsi na roho?
 asante kwa ushirikiano na ningependa unifahamishe kwa urefu.

Jawabu:(1) Naam hivo ndivo nilivokusudia, usiwe na elimu, elimu ni mkusanyiko wa kumbukumbu za watu wanatia kwenye vichwa vyetu, nzuri inafaa kwa kutafutia maisha lakini kwenye mazingira ya kumjua Mollah wako na kuyajua mambo ya (Batin)yalojificha huko elimu haifai, na mimi sikukupa elimu, ikiwa utaisoma ile mada vizuri utaona haikupi elimu ila inakupa ujuzi, ujuzi ni wa Roho, elimu ni kwa ajili ya Akili, kwa hiyo ukijaza elimu unakua muflis kwenye ujuzi, na wewe fanya uchunguzi utaligundua hilo.(2)Nikisema nafsi nina maanisha kile kilicho kwangu na kwako ni kimoja(Min Nafsi Wahid) na nikitaja Roho natafautisha 
(Unique Being as You)(3)Ndio vyote hivyo vinayo nafsi, lakini sio (Being)(4) Nafsi ni (Collective)na Roho ni ( sense of individual  consciousness).
Nadhani japo kwa uchache utanifahamu, kwa sababu hizi ni darsa kubwa kwa hiyo hata nikikufafanulia kwa maandishi utakuwa huelewi,naogopa kukufahamisha kwa urefu ndio utakua hufahamu kabisa, bora hivi kwa ufupi unapata taaluma kidogo kidogo.
Natumai imetosheleza
Shukran.

Asalaam Aleiykum

Swali:

Mara nyingi sana inanitokea kila niwaza kitu huwa kinatokea. hii ina maana gani kwangu

Jawaabu:
Umesema Inakutokea kila ukiwaza huwa kitu kinatokea, unadhani tu unawaza, mawazo hayana nafasi katika kutokea, ungesema kishatokea ningekubali, kwa sababu mawazo ni jambo la kumbukumbu, ni kitendo cha (Mind)Akili, lakini kutokea ni kitendo cha Roho, kwa hiyo huwazi bali unaona na hiyo ni (Special Gift)zawadi maalum kutoka kwa Mollah wako, ukiitunza na kuilea kwa Ibada inaweza kuzidi lakini inategemea utaitumia vipi, hiyo ni kama (Special talent)vipaji, wengine wacheza mpira, wengine Ma-Doctor, na wewe unaweza kuwa( Seer's )au (Psychic Power) ita unavopenda, hiyo ndio maana kwako.


Shukran.

Aslm Alkm

Swali
Nini maana ya ndoto ya kuota unafukuzwa kazi na utokapo nje unakuta mvua ilinyesha na barabara zimejaa maji hazipitiki


Jawabu:
Ndoto yako ina maana mbili, ama maana ya kwanza inaashiria uadui au fitna ya adui. Na maana ya pili Inashiria mafanikio utakayo yapata ama kwenye afya au kipato.


Shukran

Asalaam Aleiykum

Swali:

Umuhimu wa Sadaka kwa Muislam.


Jawabu:

Ikiwa wewe ni Mwenye uwezo umuhimu wake ni mkubwa sana na ufafanuzi wake ni mwingi katika Quraan, basi nimekuchagulia haya machache ya kukujulisha umuhimu wake, jambo la mwanzo kama wewe ni mwenye uwezo basi ni hivi. Quraan (Al-Lail aya ya 18)ٱلَّذِى يُؤۡتِى مَالَهُ ۥ يَتَزَكَّىٰ.
"Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa" vipi?(Purified) kutoa ni tendo la kujisafisha, kwa sababu umepita katika vishindo katika hiyo njia ya kupata, ikiwemo ya kumsahau Mollah wako, mpaka umeamua kutoa ina maana umemkumbuka Mollah wako, Na kumkumbuka Mollah wako ni Ibada, na hiyo ndio Taqwa, na wewe ukifanya hivyo unakumbukwa kwa kusafishwa, kusamehewa na kubarikiwa huo ndio umuhimu wake, ama kwa nyongeza hudhuria uone umuhimu wa kutoa iwe uhuru au sadaka uko hivi(Al-Balad aya ya 11 mpaka 18)ili ujue inakuaje katika kutoa sadaka.
Kwanza:فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ 
"Jee Ameukata huo Mlima"
Unaujua huo Mlima? ni njia nzito ya kwenda peponi, umerundika mali, umekalia dhahabu,unatesa wafanyakazi wa nyumbani, 
Pili:وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ
"Nini kitachokujulisha huo mlima"(Njia hiyo ya kukupeleka peponi) imefananishwa na Mlima kutokana na ugumu wake.
Tatu: فَكُّ رَقَبَةٍ 
"(Kuukata mlima huo)ni kumpa Mtumwa uungwana(Umeiona sadaka hiyo)ndio umuhimu wake".Kumuachia huru ndio sadaka yako.
Nne:أَوۡ إِطۡعَـٰمٌ۬ فِى يَوۡمٍ۬ ذِى مَسۡغَبَةٍ۬
"Au kumlisha siku ya njaa" Ipate siku ya Njaa, itafute ili utoe ndani yake kuna faida kubwa, nje unalisha (Mwili) ndani unanufaisha Roho kwa furaha na utulivu.
Tano: يَتِيمً۬ا ذَا مَقۡرَبَةٍ
"Yatima aliye Jamaa" usitoke ukaanza kutafuta mayatima wengine, anza kwa walo karibu yako, tafuta huna katika jamaa zako mayatima, ukikosa ndio umuhimu wake katoe kwengine.
Sita:وۡ مِسۡكِينً۬ا ذَا مَتۡرَبَةٍ۬
"Au Maskini aliye hoi" wale ambao hawana njia nyengine ya kupata kipato(Omba omba)"
Saba:ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ
"Ikisha awe miongoni mwa walioamini na wakauusiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Ukisha fanya hayo sasa ujiunge katika lile kundi la waloamini kikweli, na uwe katika wenye kusubiri maana mali inaweza kukauka ili ufanyiwe mtihani, na muoneane huruma hiyo ndio sadaka, kwa sababu mambo hayo mawili ukiwa nayo unakua ushafuzu, Subira na huruma.
Nane: أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ 
"Hao ndio watu wa upande wa kheri"
Huo ndio umuhimu wa kutoa sadaka unakua upande wa waja wa kheri, kwa matendo yako ya kutoa, na kila ukitoa kumbuka unaongezewa.
Shukran

Swali

 A alaykum nashkur Kwa
 majibu haya. ALLAH akujalie kila la kheri. Katika hili
 jambo. Baadhi ya masheikh wametoa fatwa .wamesema inatakiwa
 mtu aombe msamaha toba tunnasuha.asirejee kufanya
 hivyo.wengine wamesema hiyo pesa haifai ni haram. Na wengine
 wanasema wambie serikali kama mimi nilidanganya.au
 ukishindwa urudi nchi i kwako. Na hata ukitoa sadaka 
 au zaka hupati twawabu. Naomba ufafanuzi zaidi. Shukran.

Jawabu

Ni Rahisi sana kununua Madhila, dhiki, lakini vigumu Kwa mja kupata raha, ndio maana Jawabu langu limekua la kushitukiza, kwanini nikasema hivyo, kwa sababu mwanzo nilikujibu muuliza swali, na sasa hivi inanibidi nijibu swali lenyewe japokua muda wenyewe nifinyu.
Sasa nini Uwongo? Uwongo upo wa aina mbili na wote ni wenye kutokea kwenye Akili, ndio maana ukaona ukisema Uongo mmoja inabidi uutete au uulinde kwa mauongo mengine mia. Uongo wa kwanza ni ule wenye kutafuta kheri katika tukio lake, ambalo ndani yake kunapatikana thawabu, na Uwongo wa pili ni ule wenye kuleta dhara au maafa ambao ndani yake ndimo kunapatikana dhanmbi. (Mfano wa Uwongo wa kheri) لَّقَدۡ كَانَ فِى يُوسُفَ وَإِخۡوَتِهِۦۤ ءَايَـٰتٌ۬ لِّلسَّآٮِٕلِينَ.
Kwa Yakini kwenye (kisa cha)Yussuf na Ndugu zake kuna Mazingatio kwa wanaouliza.
Alifanya nini Nabii Yusuf, Aya ya 69 inasema"Na walipoingia kwa Yusuf (Akamuona ndugu yake alikua ameingia peke yake)Alimkumbatia ndugu yake akasema""Hakika mimi ni ndugu yako, basi usihuzunike kwa sababu ya yale waliyokuwa wakifanya (Ndugu)zetu. inendelea aya ya 70,"Na Alipokwisha wapatia chakula chao akaweka Jagi la kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mnadi akanadi, enyi wasafiri hakika nyinyi ni wezi" huo ndio uongo wa kheri, alifanya hivyo ili awape watu wake UKIMBIZI kwa ajili ya dhiki ya maisha na Njaa iliyokua katika Mji wao, lakini ilibidi ipatikane sababu ya wao kuweza kuja na kumleta Baba yao.
Ama Uongo wa Dhanmbi ni ule wa Ndugu za Yusuf kwa mambo waliyokua wanawafanyia ndugu zao mpaka kufikia kutaka kuwa uwa na kuwatupa ndani ya visima. Ndio maana ukaona Uongo wa Yusuf Hakutubu, ila ndugu zake aliwaombea Mollah awasamehe. Kwa hiyo utaona Uongo unakaa kwenye Akili na ikiwa kwa sababu ya kujinusuru maisha yako basi huo unakubalika, Na Ukweli ni Jambo lenye kukaa katika moyo halina nafasi kwenye kichwa, ndio maana ukisema ukweli hutaki kufikiri unajibu moja kwa moja. Sasa ikiwa Hao Masheikh wametoa Fatwa sijui kwa vigezo gani siwezi kuwasemea, kazi yangu mimi ni kukupa ukweli na kukuondolea huzuni ulokua nayo, nakufahamisha kuwa hata Mtume wa Mwenye enzi Mungu kasema uongo wa kheri ili kuwaondolea dhiki na matatizo watu wake, sasa kama hao Masheikh wanakwambia rudi, au unapata dhanmbi, hapo unahiyari yako kuwafata, lakini ukija kwangu mimi nakupa njia ya Furaha, nakwambia usihuzunike huna makosa, na pesa sio haramu, ila kama unafanya yale mambo wewe na mkeo hamkai pamoja, sijui hivi sijui vile hapo itakua meingia kwenye makosa ya dhuluma.

Natumai imetosheleza ufafanuzi wangu.











5 comments:

  1. Nimeota mtu(mwanaume) wakifanya mapenzi na maiti wawili(wanawake), mtoto na mtu mzima nini maana ya ndoto hii

    ReplyDelete
  2. mim cijaolew na nimetoka kulala na mwanaume je naruhusiw kuswali

    ReplyDelete
  3. Kukopa simu za mkopo inaswihi unalipa kidogo kidogo

    ReplyDelete