Friday, May 9, 2025

NYUMBA YA ROHO

 Asalaam alekum 

Mwanaadamu ana usingizi wa aina mbili, usingizi wa kwanza ni wa kimwili halafu wa pili ni wa kiroho(Japokua Roho hailali)inayo lala ni (BODY)yako tu. Sasa leo itabidi tujiulize swali, kwani Roho ina nyumba?.Jawabu ndio Mwili wa binaadamu ndio Nyumba yake. Kivipi inakua huu mwili ni nyumba?. Kulijibu swali hili inabidi tuiangalie sayansi na maendeleo yake, tumeshuhudia katika zama hizi za karibuni vipi elimu ya (A I) ilivo fanikiwa kutengeneza (Robot) ambalo lina uwezo wa kufanya kazi zote zinazofanywa na Binaadamu , katika hilo kuna mazingatio makubwa kwa wenye Akili kulitizama kwa undani. Imefika wakati wana sayansi wadini tutoe maelezo ambayo yapo karne nyingi lakini tulikua hatuelewi. Inabidi sasa niseme hata wewe huo Mwili wako ni (Robot)Lakini ilotengenezwa na Mbora wa kuumba (Mollah)wako, Na yeye ndo alotupa Elimu hii ya kuweza kutengeneza hawa (Ma Robot) tafauti yake yetu tunatumia chuma na hii ya mwili wetu imetumika (living organism), kuelewa hayo inabidi kwanza uamshwe kiroho kwa kutumia akili uelezwe kwamba wewe na huo Mwili wako ni vitu viwili tafauti. Mwili ni Jumba lilo na cheo kutukufu ambacho kakiumba Mwenye enzi Mungu kwa uwezo wake Mkubwa, vitu vyote katika Mwili huo vinafanya kazi yake (Automatic)bila ya wewe kuingilia kati kwa chochote kile na vyengine bila wewe hata kujua, kuvuta kwako Pumzi (Automatic) unakula chakula ukishatia Mdomoni yalobaki yote (Automatic) mpaka kwenda kwako chooni (Automatic)Unatoa sumu mwilini (Automatic) Mpaka hiyo (Sex)unayo ipenda ni (Automatic)Kazi nyingi katika hiyo (BODY) yako ni (Automatic)kwa sasa huwezi kuelewa mpaka ukae kwa utulivu na ukimya na mazingatio makubwa ndio utaweza labda kunielewa na huenda ukapata kwa uchache maarifa ya kujua maelezo yangu. Ukijua Maelezo yangu moja kwa moja utagundua hili Jumba ninalo Ishi ndani yake Mollah kalipangia muda wake, akatupa (Hint) kutudokeza tutakupeni nyinyi kuishi katika jumba hilo kiasi cha umri wa miaka 60 halafu tuta kuongezeni (Bonus)miaka 10 itakapo pita hiyo miaka 70 na ukaanza kuingia 80 basi hapo tena elewa baada ya hilo jumba kuitumikia Roho kwa muda wa miaka sabini sasa itakua zamu ya Roho kulitumikia Hilo Jumba, kwa njia gani? Mwanzo niliposema Roho ipo kwenye usingizi nikasema hailali sasa ule usingizi unaondoka na roho inaanza kutumika, na utumwa wa Roho ni kule nyakati zote kua (Alerts)nikupe mfano unapokua na afya Akili haijui nini Afya, jumba liko zima unaendelea kujitafutia mali , kufanya uharibifu, unafanya maasi ya kila aina, unakunywa pombe , unakula rushwa, unatesa wenzio, unjifaharisha na kila kitu, hukumbuki chochote umelala Kiroho, lakini subiri unaposhikwa na Maradhi umwa kidole au jino (Automatic Mode) inaondoka unaanza kuishi kwenye Roho, hapo ndio unajua tafauti yako na huo Mwili, hapo ndio unaweza kutafautisha baina ya wewe na huo mwili, wakati wote jino lilikuwepo , kidole kilikuwepo lakini ulikua huna habari, lakini Maradhi ndio yanakuzindua , yanakutoa usingizini, mpaka pale ukipewa dawa ukapona unarudi kwenye usingizi wako unaendelea kuyachapa maisha kama kawaida, sasa kwa watu wazima (BODY) haisikii tena dawa , maumivu yanakua yanaendelea Roho inatumikia mwili hakuna tena furaha ndio maana tabu sana kumkuta Mzee wa miaka 80 ana furaha ya kuendelea kwa sababu (constantly) yupo kwenye (alert)ya Maradhi wachunguze watu wazima utalijua hilo mambo ni (vice versa) Ni wakati wa Roho kutumikia Mwili , kwa hiyo utagundua sasa (full awareness)imepatikana kuwa sasa unaishi ndani ya (BODY)na una (Experience)kubomoka kwa jumba lako ambalo limemaliza muda wake wa kuishi. Ukiwa Mja Mwenye Akili utagundua sasa hivi wewe ni Mwenye Nyumba ila unatawaliwa na wapangaji. Katika Jumba hilo Mollah kakupa neema nyingi sana leo ntakutajia kwa uchache.

No comments:

Post a Comment