Tuesday, February 24, 2026

NJIA YA KUIPATA SALA

 Aslm alekum. Limekuja  . Swali wameniomba muongozo japo kidogo ili na sisi  wasomaji wako tupate faida. Na swali la lenyewe tunakuomba tupe uchambuzi wa aya ya 45 iliyomo kwenye sura ya (An-Kabut)Tunaomba ufafanuzi kwa sababu aya hiyo inasema Sala inatuepusha na machafu  na maovu, Na sisi tunasali kama wengine wanavosali, ila sisi bado tunaendelea na maasi na machafu, Na hali hii inaendelea miaka nenda miaka rudi na tumeshindwa kabisa kujivua katika katika kadhia hii ya uchafu na maovu. Naam Kwanza kabisa wacha niweke wazi mimi ni msafiri mwenzenu tumo kwenye meli hii ya Dunia tuna kwenda kwenye safari hii ya Ulimengu  tunazungumza na nyie kwa kile kidogo alichotupa Mwenye enzi Mungu katika elimu zake, na ikifika wakati kila mmoja wetu anateremka na kuachia wengine waendelee na safari hii ya Maisha, Kwa hiyo kazi yangu mimi sio kusomesha (hiyo ni kazi ya Masheikh)kazi yangu mimi ni kukumbusha kile ulicho sahau,  Naam sasa twendeni kwenye swali lenu lenye kuhusu  hiyo aya mloitaja,  Ama kuhusu kuendelea kwenu na maasi na machafu wakati mnasali inakushangazeni wakati (Quraan) imetoa Ahadi hilo nishalizungumza  kwenye makala ya (Dawa ya Dhanbi)Lakini leo ntatoa tena ufafanuzi ili niongeze (Dozi)ya hilo swali ili mtibu maradhi mlonayo.Katika darsa hii wacha nikukumbushe kitu, katika harakati zote hizo lazima upate taa ya Mwenye enzi Mungu kwa njia ya Neno au ufahamu ndio utaweza kutekeleza kwa ukamilifu agizo la utiifu kwa Mwenye enzi Mungu, kwanini nikasema hivyo? Kwa sababu bila ya kupata taa uongofu huo itakua Taa inawaka lakini wewe (Still) Huoni bado upo kwenye kiza. Nikisema (TAA)(Light)Nina maana gani?, Maana yangu kuwa Uislam ndio dini pekee iloanza na Neno Soma, kwa hiyo Dini inakutaka usome kwanza ili upate kufahamu, ukisha kufahamu ndio matendo yako yote yatakua na mafanikio, sio ufate tu ukiambiwa, kwa hiyo ukisoma utapata kujua vipi Neno lina nguvu ya kubadilisha mwenendo wa mtu, Hapa wacha niwape kisa ili kukuonesheni nguvu ya neno linavopasua moyo na ujumbe kufika kwenye roho na ukaacha maasi na machafu mara moja, Lakini kwanza ifahamike Mwenye enzi Mungu hakubadilishi mpaka utake Mwenyewe kubadilika, kama anavosema kwenye sura ya (RAD aya ya 11), kwanza napenda ieleweke kuacha kuna aina mbili aina ya mwanzo unaacha hapo hapo, ukipata (Single spike)Ya neno likapenya kwenye Roho yako sio kwenye Akili basi unabadilika daima, na aina ya pili unaacha kidogo kidogo mpaka unatambua haya mambo hayana faida kwangu wala hayanipi furaha ila kunipa matatizo sasa na baadae.  Sasa nifanye nini,? wacha tukisikilize kisa cha Tajiri Mmoja aliyeishi Iraq akawa na yeye mtenda maasi kama wewe na huku Ana sali Anafanya ibada lakini anaendelea na Maasi.kisome au kisikilize kisa hiki kwa mazingatio makubwa inaweza kuwa na wewe ni sababu yako ya kuacha maasi na ukaendelea na Ibada. Alikua tajiri huyu Akiishi kwenye nchi ya (Iraq) Na ikawa kawaida yake akialika watu kwenye (Party)zake wao wakiziita (Samra, au Raksa) au (Sumsumia)ila kwa lugha yenu ya sasa wacha tuite (Kizaizai). 1

NJIA YA KUIPATA SALA

 Aslm alekum,  Mambo yanofanyika katika (Kasri) ya Bwana huyo hayasemeki, wanaingia wanawake wamefunga vioo kwenye viuno ukiwatizama mpaka wewe mtazamaji unapata kizunguzungu kwa jinsi wanavocheza, muziki na mvinyo unagaiwa bila ya kikomo watu wanalewa na kufurahi yote hayo kutoka kwa fadhila za Bwana aitwaye (Ashraq bin Malik), Siku moja katika baadhi ya hizi (Party) akawa anapita Mcha Mungu Mmoja kwenye hilo kasri akasikia kelele za ngoma na watu wanaimba mara akafungua mtu mlango anatoka nje na hakuwa mwengine ila mfanyakazi pendwa wa Ashraq bin Malik anakwenda kutafuta ongezo la mvinyo ambao ulikua umekwisha, kwa bahati wakakutana uso kwa macho na huyu Walii aliyekua anajipitia njia ndio Akamuuliza nani nani huyu anafanya (Party)hii , yule Mfanyakazi akajibu Bwana wa mabwana (Ashraq bin Malik)ndie anafanya hii Party, yule Walii Akamjibu neno moja tu akamwambia(Laaillah Illah Allah) nilijua atakua Bwana wa mabwana kwa sababu Mtumwa wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya haya, huyoo yule Walii akashika njia na kuzama mitaani, mfanyakazi akanunua ulevi kufika juu ikawa kachelewa kidogo (Ashraq bin Malik) akamuuliza mbona umechelewa?, yule Mfanyakazi akamuhadithia yale mazungumzo na yule Mcha Mungu akamwambia kasema kwanza kabisa Katamka Laaillah Illa Allah , ikisha akasema Mtumwa (Abidi)wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya mambo haya, kusikia maneno hayo pale pale (Ashraq bin Malik)Alitoka mbio kumtafuta yule Walii akamwambia umesema maneno makubwa yamepasua Moyo wangu kuanzia leo mimi nimeacha kila kitu, nimeacha mali yangu na nimeacha family yangu mimi kuanzia sasa nataka kuwa mtumwa wa mwenye enzi Mungu, yule walii akamwambia ewe (Ashraq bin Malik)Mollah wako kakupenda kakupa mali zote na furaha yote ulonayo kwa ajili ya mapenzi yake kwako, (Ashraq) Akajibu na mimi kuanzia leo naacha kila kitu kwa Ajili ya Mollah wangu muumba, Na kuanzia leo sitovaa viatu tena kwa sababu Mollah wangu kaniita bila ya viatu vipi leo mimi nirejee nikavae vitu, ndio kuanzia hapo (Ashraq)akajulikana (Kwa jina la Darweish asovaa viatu)Na akasamehe Mali zake na Kasri lake akawa Mcha Mungu mkubwa kwenye Jiji la Iraq, family yake walimbebeleza sana arudi nyumbani lakini hakutaka tena akawa ni mwenye kumsabahi Mollah wake na vikao vyake ni vile vya wacha Mungu tu, ikapita miaka miwili mitatu watu wake wa nyumbani wakamsihi akawatemblee japo kwa masaa tu wamuone,  basi ikapangwa siku wakamualika kahawa akawa amekaa kwenye varanda na watu wake anakunywa kahawa kwenye urefu wa kama ghorofa moja hivi, mara huku chini wanapita vijana wanadhikiri chini mtaani huku wanasema kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge, kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge nasi, mara wanasikia makelele Ashraq bin Malik Juba linazunguka hewani kachupa mpaka chini, alipofika chini wale vijana wote wakatawanyika wakenda mbio, mara wanamuona Ashraq bin Malik ananyanyuka anakumta juba lake wakarudi wakamuuliza hujaumia akawajibu  yule alonambia nichupe atashindwa kunidaka, vijana wakatizamana machoni, Ashraq akwaambia nikadhani nyie wapenzi wa Mungu kumbe ni mdomoni tu lakini bado hajaingia moyoni, nendeni mkajizoeshe mpaka Mollah wenu ajae moyoni hapo ndio mtakua mesimamisha Sala. Sasa tunaingia kwenye Aya mloileta pengine na nyinyi mnataka neno moja muwe kama Ashraq bin Malik,  lakini tukumbuke kuacha ni aina mbili, ya kwanza ni aina ya Ashraq bin Malik, hapo hapo unaacha kila kitu na ya pili hii ya taratibu anasema (Mshairi) (Nilipogundua mimi kwenye Moyo wangu anakaa asiekua wewe, nilifanya jitihada, kila njia kuujaza muongozo wako mpaka akawa hakai asiyekua wewe) sasa wacha tuingie kwenye hii Darsa soma kwa makini na wewe uwache maasi yote, sasa Ufanye nini? 2

NJIA YA KUIPATA SALA

 Aslm alekum.  Aina ya kwanza ni kupata uongofu wa taa ya Mollah wako ukaacha hapo hapo na aina ya pili ndio hii aya mloileta kwenye swali lenu kutoka kwenye aya ya 45 sura ya Ankabbot? Linasema hivi: 


ٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَصۡنَعُونَ"Soma uliyoletewa Wahyi Katika kitabu na usimamishe Sala, Bila shaka (Sala ikisaliwa vizuri)Humzuiliya anaye sali na mambo machafu na maovu, na kwa yakini kumkumbuka Mwenye enzi Mungu ni jambo kubwa kabisa, na Mwenye enzi Mungu anajua mnayoyatenda"   Naam ukweli wenyewe hii aya imeshajibu swali lenu lakini tunapishana katika ufahamu,  Tatizo liko kwenye hiyo sala  unaisali vipi?. Imepambanua hii aya halafu jibu rasmi tutalipata kwenye aya nyengine lenye kuitilia nguvu aya hii twende taratibu usikurupuke utakua hujafahamu kitu, najua litawagusa hili lakini itanibidi mnipe nafasi nifafanue kidogo ili mpate kuamka usingizini, pengine mja bado kalala japo  anajiona yuko macho.Sala ziko za aina mbili aina ya  mwanzo ni ile inotegemea Akili na aina nyengine ni ile  inayo saliwa na Roho, hii ya Akili ndio wengi wetu Muadhini akinadi sote tunakimbilia msikitini na hapo vinaendelea vitendo vitupu ndio maana utajikuta mara upo bank mara upo ofisini, mara unamfikiri mkeo mara unakumbuka madeni,  mara chache sana kuipata Sala yenyewe ndio maana ukitoka hapo unakwenda kuendelea na vitendo vyako viovu na machafu ya kuzini, kula rushwa kudhulumu kuiba, kusema uongo na kudhulumu masikini haki zao na hali ya kuwa umetokea msikitini kwa sababu kwenye hiyo sala yenywe wewe hupo kabisa madeni yanakuja hapo, Mara unamdai mtu hii ndani ya sala Mollah wako ulomuendea humkumbuki kabisa, Lakini yeye Ana kusubiri kwenye enzi ya       kusubiri , anakungoja labda utatubia,bado umo kwenye Level ya kwanza ya Uislam,unajua kwanini? K  kwa   sababu Huzijui (Level)ya  sala yenywe. Salah ina (Level 3) Sala ya mwanzo ndio niliitaja hapo juu ni (Level 1), na (Level 2) ya pili Hii ni ya Muumin  (Fii Salat Ghashiun)Sala hii sasa niya  unyenyekevu (Empty) hakiji kitu ndani ya Sala isipokua kumsabahi Mollah na kumtukuza hayaji mambo ya kidunia kabisa, Hii ndio ile Sala ya (Ghaib)ilothibiti Imani na matumaini  halafu kuna hii (Level 3) Sala ya (Shahadat)ambayo hiyo imejaa (Taqwa)Mwanzo mpaka mwisho wa hiyo Sala  inasaliwa Kiroho ndio za Mawalii na wacha Mungu wakweli  mara utamuona mtu machozi yana miminika kwa sababu Sala imegusa kitu kisicho onekana. Kwenye (Level) hii wewe unageuka kuwa Shahid na hiyo ndio iwe (Target) yako ungali ukiishi kwenye Ulimwengu huu, Na Wakati wa kufa kwako, Naam sala hii inapatikanaje hapa nitakupeni(Dalili) halafu utaangalia mwenyewe unasali vipi kiroho au kutumia Akili. Aya inasema "Soma katika uliyoletewa wahyi katika kitabu na usimamishe Sala"Ulipoambiwa Soma umefundishwa uzingatie yaliyomo kwenye hichi kitabu ndio iwe muongozo wako ndio iwe taa yako, hayo utakayo yasoma ndio yatakufundisha usiibe, usizini, usidhulumu, usiseme uongo, usidhuru wenzio, usile rushwa, yaani kila ukisoma basi utakuta kuna mafundisho ambayo itakua muongozo na ndio taa yako itakayo kuepusha kwenye msitu wa  mchana wa hayo machafu na maovu quraan itakua inakushitua, usome wahyi huu, halafu ukishasoma ufanye nini? Udumishe kumkumbuka Mollah wako aliye Mkubwa, kwanini ikawa umkumbuke kwa sababu ni jambo kubwa kabisa kivipi?Ukimkumbuka Mollah wako kila mara utaona kuna vitu viwili  tafauti moja ni Sala na na la pili kukumbuka.nini kukumbuka? Ni (Awareness )(Hadhir)na  unapofanya hivyo huipi Akili kupenyeza jambo lengine na Akili ikiwa haipewi nafasi inafanya nini? Ina kufa(au kutulia) Akili ikifa ndio mwanzo wakufunguliwa juu yako mambo mengine, (Elimu zengine)(Na Hekima nyingi)Sala yako sasa itakua tafauti,  ucha Mungu wako unakua wa hali ya juu ila kufikia hali hiyo inabidi usubiri mlangoni kwenye kukumbukuka, kuna mambo mawili Mwanaadamu Huna uwezo nayo huwezi kuyatafuta ila yanakutafuta wewe,  Kifo na Mapenzi viwili hivyo Huna uwezo navyo kabisa lakini kaa mlangoni gonga mlango asaa utafunguliwa itumie quraan au yatumie Majina 99 ya Mwenye enzi Mungu mlango ukifunguliwa utaacha machafu yote na maovu yote na utakua unapata Sala yako kikamilifu na aya inamalizia kuwa Mwenye enzi Mungu anayajua yote mnayoyatenda. Huo ndio Muongozo wa mwanzo kwenye hiyo aya mloleta, ama aya ya pili inayokupa    nguvu zaidi ni hii aya ya 3.3b

NJIA YA KUIPATA SALA

 Aslm Alekum,  Kama nilivosema huo ni muongozo wa mwanzo sasa wacha tuingie kwenye muongozo wa pili pia tunabebwa na (aya ya 78 Sura ya israa)" simamisha Sala linapopinduka jua mpaka unapoingia usiku na Quraan wakati wa alfajir imekua yenye  kushudiwa" Naam wamefasir kwa ukamilifu kuhusu kusimamisha sala na wakasema inashuhudiwa na Malaika, sasa sisi tuendelee zaidi tuchambue nini neno (Shahada)?Kwanini ikatajwa Shahada, na Kwanini ikazingatiwa Alfajir? Kwanza kabisa wacha tujue Shahada yenyewe ikoje,? Shahada iliyo kusudiwa hapo ni ile Shahada ya mwanzo ,napenda uelewe Shahada ina nguzo saba kikamilifu(Katika hizo 4 ndio kubwa) Lakini zote zinategemeana na katika hilo La shahada umelibeba wewe Mwanaadamu kutokana na kuwezeshwa na Mollah wako, Amma nguzo ya Mwanzo ya Shahada ni kusikia (Ndio maana utaona mwanzo inatajwa Samia 1) ikisha inafatia (Basira 2)Kuona, halafu tena inakuja Uwepo(Present au moment of Now 3)Na baadae inafatiwa na Kumbukumbu(history 4)nguzo ya tano (Experience 5)Nguzo ya sita ni elimu(Knowledge)au ita kujua na ya saba ni hiyo (Silent)Ukizipitia hizo zote hapo ndio utajikuta wewe mwenyewe jiite utakavo (Roho) Au (Human being) hizo ndio (Level) za Shahadat ambazo mja unatakiwa kuzitambua unaposema neno Shahidi, ujue umekusudia nini ama una shuhudia nini?, Sasa kwanini ikatajwa nyakati za Alfajir?. Tukitaka kulijua hilo tukihudhurie kwanza kisa kilichomo kwenye (Quraan) Kuhusiana na wale (As-Habul-Kahf)Kuhusiana na Kadhia ya kusikia ili tupate kujua kwani kusikia kuna faida gani, Mollah wako ?Alifanya nini, (Quraan  aya ya 11 sura ya  Al-Kahfi) "Tukaziba masikio yao (Wakalala hawasikii   chochote) Katika pango hilo kwa idadi ya miaka mingi. Wameondoshewa uwezo wa kusikia ili wapate kulala, hata wewe unafanyiwa kitendo hicho kila usiku ukenda kulala,  bila kuondoshewa uwezo  huo utakua hulali kabisa, kumbuka huna uwezo wewe wa kuzuia usisikie, ( Natural)Huwezi kufanya usisikie, ukiziba masikio (Still) Utasikia sauti  Nyengine ambayo pia ita ku (Disturb)Utaipa jina (Tinnitus), sasa baada ya kujua hayo Sayansi inasemaje katika hili,  Wanasema wanasayansi Kusikia ni kitu cha Mwisho Mwanaadamu anapolala kuondoka,  Kwa Sababu kusikia ndio chanzo kinachoiweka Akili (Active)Ukiondoshewa Uwezo wa kusikia Akili inajizima (Data)Na kuanza (Kudelete)Mambo ya mchana kutwa. Na ikiwa haijazimika inabakia (Alert) utaona kelele kidogo umeshituka, Wagonjwa walio kwenye (Coma) Wanapata kusikia ndio maana (Akili)zao zikitizamwa zinafanya kazi, kwa sababu ya sauti,  wakaendelea kusema Wachunguzi wa Sayansi ya usingizi sauti zinakuzuia kupata (Deep sleep)Mwanaadamu katengenezewa (System)Maalum itwayo (The Reticular Activating System) Hii (RAS) ndio inayokuweka (Awake,conscious, Aware) Na sikio ndio Sehemu yenye nguvu ya kupitisha sauti za kila aina, hiyo (RAS System) inapofungwa au kufunikwa ndio Mwanaadamu anapata (Deep unconscious sleep) Akili haipat (Sensory disturbance) ndio inapoingia kwenye (Minimal activity ) hapo ndio unapata nafasi ya kufuta yale yote yasokua muhimu na mengine kuyaweka kwenye (Memory) Ukiamka usha (Deleted) Unakuwa mweupe hukumbuki mengi yalopita jana. Sasa nini kinatokea unaporudishiwa uwezo wa kusikia, Jambo la mwanzo linalo rudi ni kusikia, ila wewe kwakua huko (Aware) unadhani ni kufungua macho, Lakini ukichunguza utakuta jambo la mwanzo ni kusikia kama ulivokuja duniani wakati wakuzaliwa, (Umo kwenye darsa ya simulizi ya kusikia katika fani ya Shahada zingatia sana Miujiza ya Mollah wako ikisha useme Ametukuka mbora wa Uumbaji) Naam  Sasa kumbuka ikiwa ulipokuja kwenye Ulimwengu kwa mara ya Mwanzo ni kusikia basi elewa na jambo la mwisho pia itakua kusikia itakua sauti (Kwa hiyo kuweni na tahadhari mkiwa kwa wagonjwa mahtuti wanokaribia kufa kumbukeni wanasikia mnayoyasema yote), Sasa kwanini ikatajwa (Quraan) Wakati wa Alfajir ni kwa sababu kinachoingia na kusikiwa Mwanzo ndio kina kua (Pure) kina kaa kwa muda mrefu kina kuwa Na (Direct communication) Na Roho yako, hapo kinakupa (Deep Meaning) Ufasaha wa wazi , sasa ikiwa tabia yako kusoma, kusikiliza, Quraan nyakati za Alfajir wakati una Sali au baada ya sala ndio nyakati hizo za Alfajir unapata hiyo (Hudan lin-nasi)Muongozo kutoka kwa Mollah wako(Al-Baqarah 120) Ukiufata sawa sawa muongozo huo ndio itakua taa yako (Torch) ya kukumurikia njia kwenye huu msitu wa dunia ulojaa maasi, hapo ndio unapata (clear Picture) Wewe usitende Dhanbi, usile rushwa, usidhulumu, Usizini, unapata ufafanuzi wa mambo hayo kama ulivopata ufafanuzi wa hii kadhia ya kusikia na mahusiano ya Quraan Alfajir, kila kitu kinafunguliwa kwako kunakua kweupe, na pia utapata maelekezo ya mambo mema mchana kutwa ikiwa umeyashika sawasawa mafunzo ulopitia Alfajir yenye Uongofu kutoka kwa Mollah wako, Maisha yako yatabadilika ikiwa Quraan itajaa kwenye moyo wako ikiambatana na tafsiri yake , itakupa uwezo wa kuacha Maasi na kuipata Sala yako sawa sawa bila ya upungufu, utaacha maasi na Sala zako zitakamilika bila ya wewe kuyarejea maasi,  hii ndio ngao ya pili, kumbuka ya Mwanzo kutumia jina La Mollah wako kwa ukumbusho na hii ya pili kukisoma kitabu chake kama Muongozo.  Mollah wangu anajua zaidi. 4