Aslm alekum, Mambo yanofanyika katika (Kasri) ya Bwana huyo hayasemeki, wanaingia wanawake wamefunga vioo kwenye viuno ukiwatizama mpaka wewe mtazamaji unapata kizunguzungu kwa jinsi wanavocheza, muziki na mvinyo unagaiwa bila ya kikomo watu wanalewa na kufurahi yote hayo kutoka kwa fadhila za Bwana aitwaye (Ashraq bin Malik), Siku moja katika baadhi ya hizi (Party) akawa anapita Mcha Mungu Mmoja kwenye hilo kasri akasikia kelele za ngoma na watu wanaimba mara akafungua mtu mlango anatoka nje na hakuwa mwengine ila mfanyakazi pendwa wa Ashraq bin Malik anakwenda kutafuta ongezo la mvinyo ambao ulikua umekwisha, kwa bahati wakakutana uso kwa macho na huyu Walii aliyekua anajipitia njia ndio Akamuuliza nani nani huyu anafanya (Party)hii , yule Mfanyakazi akajibu Bwana wa mabwana (Ashraq bin Malik)ndie anafanya hii Party, yule Walii Akamjibu neno moja tu akamwambia(Laaillah Illah Allah) nilijua atakua Bwana wa mabwana kwa sababu Mtumwa wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya haya, huyoo yule Walii akashika njia na kuzama mitaani, mfanyakazi akanunua ulevi kufika juu ikawa kachelewa kidogo (Ashraq bin Malik) akamuuliza mbona umechelewa?, yule Mfanyakazi akamuhadithia yale mazungumzo na yule Mcha Mungu akamwambia kasema kwanza kabisa Katamka Laaillah Illa Allah , ikisha akasema Mtumwa (Abidi)wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya mambo haya, kusikia maneno hayo pale pale (Ashraq bin Malik)Alitoka mbio kumtafuta yule Walii akamwambia umesema maneno makubwa yamepasua Moyo wangu kuanzia leo mimi nimeacha kila kitu, nimeacha mali yangu na nimeacha family yangu mimi kuanzia sasa nataka kuwa mtumwa wa mwenye enzi Mungu, yule walii akamwambia ewe (Ashraq bin Malik)Mollah wako kakupenda kakupa mali zote na furaha yote ulonayo kwa ajili ya mapenzi yake kwako, (Ashraq) Akajibu na mimi kuanzia leo naacha kila kitu kwa Ajili ya Mollah wangu muumba, Na kuanzia leo sitovaa viatu tena kwa sababu Mollah wangu kaniita bila ya viatu vipi leo mimi nirejee nikavae vitu, ndio kuanzia hapo (Ashraq)akajulikana (Kwa jina la Darweish asovaa viatu)Na akasamehe Mali zake na Kasri lake akawa Mcha Mungu mkubwa kwenye Jiji la Iraq, family yake walimbebeleza sana arudi nyumbani lakini hakutaka tena akawa ni mwenye kumsabahi Mollah wake na vikao vyake ni vile vya wacha Mungu tu, ikapita miaka miwili mitatu watu wake wa nyumbani wakamsihi akawatemblee japo kwa masaa tu wamuone, basi ikapangwa siku wakamualika kahawa akawa amekaa kwenye varanda na watu wake anakunywa kahawa kwenye urefu wa kama ghorofa moja hivi, mara huku chini wanapita vijana wanadhikiri chini mtaani huku wanasema kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge, kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge nasi, mara wanasikia makelele Ashraq bin Malik Juba linazunguka hewani kachupa mpaka chini, alipofika chini wale vijana wote wakatawanyika wakenda mbio, mara wanamuona Ashraq bin Malik ananyanyuka anakumta juba lake wakarudi wakamuuliza hujaumia akawajibu yule alonambia nichupe atashindwa kunidaka, vijana wakatizamana machoni, Ashraq akwaambia nikadhani nyie wapenzi wa Mungu kumbe ni mdomoni tu lakini bado hajaingia moyoni, nendeni mkajizoeshe mpaka Mollah wenu ajae moyoni hapo ndio mtakua mesimamisha Sala. Sasa tunaingia kwenye Aya mloileta pengine na nyinyi mnataka neno moja muwe kama Ashraq bin Malik, lakini tukumbuke kuacha ni aina mbili, ya kwanza ni aina ya Ashraq bin Malik, hapo hapo unaacha kila kitu na ya pili hii ya taratibu anasema (Mshairi) (Nilipogundua mimi kwenye Moyo wangu anakaa asiekua wewe, nilifanya jitihada, kila njia kuujaza muongozo wako mpaka akawa hakai asiyekua wewe) sasa wacha tuingie kwenye hii Darsa soma kwa makini na wewe uwache maasi yote, sasa Ufanye nini? 2
No comments:
Post a Comment