Aslm alekum, Ndugu zangu wa Kiislam leo nataka kuzungumza na nyinyi kuhusu huzuni nilo nayo katika jambo la misiba yetu, Imekua desturi sasa kila nikihudhuria Maziko au kwenye misiba majumbani unakuta watu wamegeuza mkusanyiko huo kuwa baraza ya kubadilishana mawazo au number za simu, mazungumzo hapo yanakua kama yale ya Tamaduni zengine wafanyavo kama vile kunywa pombe, au kucheza na jeneza, hali hii inasikitisha sana kwani inakwenda kinyume na maagizo ya Bwana Mtume s.a.w aliposema nendeni kudhuru Makaburi kwani katika hilo kuna makumbusho makubwa kwa nyie Mlobaki duniani. Sasa kwa Mwenendo huu tulofikia hivi sasa kuna mambo mawili yamejitokeza inatupasa tuyaangalie kwa undani zaidi, ikisha tukumbushane labda tumeghafilika, Mambo gani hayo? La kwanza labda mtu haja elimishwa kuhusu kadhia hii ya kufa mtu, au jambo la pili ni njia ya kudharau maelekezo ya Mtume wetu kuwa nendeni kwenye misiba kwani kufanya hivyo kuta kukumbusheni Umauti, na hapa leo ndio tutaingia (Deep)kwenye hii darsa yetu ya Kifo ili tujue kwanini Bwana Mtume s.a.w akayasema hayo na alikusudia nini kuamrisha tuka hudhurie Maziko. Sababu kubwa ilikua ukenda mazikoni pahala palipofiwa sio iwe ndio sehemu ya kukutana na marafiki au jamaa mlopoteana, kusudio lilikua sehemu hiyo au pahala hapo ni eneo litokufanya wewe kuzingatia au kujigundua wewe nani na dhumuni lako nini kuwepo hapa ulimwenguni.Mwenye enzi Mungu kakuuliza kwenye Sura ya Dhaariyat aya ya (21)" Na katika Nafsi zenu Je Hamuoni", Umauti kazi yake kubwa ni kukumbusha na kama hujakumbuka basi ogopa sana kuna kitu ndani ya nafsi yako kimeku (block) au ukijiona upo hapo lakini unazungumzia matokeo ya mpira au siasa basi jijue bado umo kwenye lepe lepe la usingizi na hiyo ni ishara kubwa umejisahau sana, fahamu wewe ushakua sugu , na kama hujakumbuka hapo basi tunakuchia endelea kujikusanyia mali, furahia maisha mpaka siku hii ikukute kwa ghafla hali yakua umefilisikana huna kitu chochote cha kuchukua huo upande wa pili unapokwenda ama kurejea kwa Mollah wako kwenye Nyumba ya milele, Napenda kukumbusha uelewe Mauti ni Mawaidha makubwa kwenye Maisha yako, Ikiwa wewe Raisi au Mwenyekiti, Kama wewe tajiri au Daktari au kuwa maskin wa hali ya chini kwenye kadhia hii nyote mko sawa na iko siku ilee uloandika (Contract)Yako ya kuondoka hapa ulimwenguni ikifika basi jijue haitokhairishwa saa wala dakika ukifika muda lazima uondoke. Kabla yakuingia kwenye Maudhui yenyewe Mwenye enzi Mungu anatukumbusha nini kuhusu Umauti, kumbuka hapo Mwanzo wasia wa Mtume na sasa Mollah wako anakufahamisha tena kuhusu tukio hili la kifo linakuaje? 1
Saturday, March 14, 2026
KICHEKO MSIBANI
فَٱلْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ ءَايَةًۭ ۚ وَإِنَّ كَثِيرًۭا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنْ ءَايَـٰتِنَا لَغَـٰفِلُونَ(Basi leo tutakuokoa ili tukuweke uje kuwa mfano kwa watakaokuja baada yako,Na watu wengi wameghafilika na ishara zetu. Naam kwanini ikawa mfano Kwa sababu Firaun alijisahau kama mimi na wewe ikafika mpaka kujiita Mungu kwa ajili ya cheo chake cha ufalme, akifanya alofanya mpaka khofu ikamuondoka, sasa kuwachwa kwake kwa hiyo Body ni kujulishwa sisi( body )itabaki, lakini kuna kitu kitaondoka ni ishara ya kutukumbusha sisi body sio wewe, ila kuna kitu chengine chenye mahusiano na mwenye enzi Mungu ambacho unatakiwa kukizingatia, na hii leo ndio madhumuni ya darsa hii ya kifo ili uwache kughafilika na kucheka misibani na kuleta mazungumzo yaso maana , kuanzia leo usichukulie kifo ni jambo la kawaida ni jambo zito ambalo wewe unalifanyia mazoezi kila siku, Ewe ndugu yangu wa kiislam kwani wewe si unapata usingizi kila unapoingia usiku, Unaujua wewe nini usingizi, wacha nikupe habari ya usingizi ili upate kuzinduka ujijue na wewe vilevile ni maiti mtarajiwa mwenzio tu katangulia na wewe wakati wowote unaweza kufatia, napenda ufahamu kuanzia leo kila ukenda kulala kitandani unatia saini yako ya kufa wewe kila usiku unakwenda safari hii bila ya kujijua unakwenda wapi, Miujiza hii unaitenda kila usiku, Ushawahi kujiliza unakwenda wapi?pahala unapokwenda wewe ndio alipokwenda huyo Maiti unae mpuuza wakati anafukiwa kwenye udongo mzito, sasa kuanzia leo Jiulize hivi mimi usiku nakwenda wapi ?, na kama unaogopa kujiuliza Mwenyewe acha nikupe dalili wapi unakwenda ikisha utaamua Mwenyewe nilete heshima na Taqwa nikiwa mazikoni au msibani , au niendelee kujificha kwenye chaka la mazungumzo kuepuka siku hii nzito ambayo na mimi itanikuta, basi kama upo tayari tega sikio uijue safari yako unayokwenda kila siku unayoishi duniani, kumbuka kila ukisema Innalillah waina Illahi Raajiun uijue na maana yake, sio unasema ikawa iko mdomoni lazima izame ndani ya Moyo ujijue unatamka maneno gani, maneno hayo na wewe yanakuhusu na kila ukilala tambua unakwenda sehemu Adhim, kwa hiyo lazima uelewe sehemu hiyo unarudi vipi na kwa adabu gani na umechukua nini kama zawadi siku hiyo اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
"Mwenye enzi mungu Huzichukua Roho wakati wa mauti yake, Na zile ambazo bado kufa kwake huzichukua nyakati za kulala, (kwenye usingizi wao) Basi huzizuia zile alozikidhia Mauti, Na huzirudisha zile nyengine mpaka ufike wakati (wake)ulowekwa, bila shaka katika hayo yamo mazingatio kwa watu wanaotafakari". Naam hapo wametajwa makundi Matatu, kundi la kwanza lile linalokufa (Shuhuda) yaani wakiwa macho, na kundi la pili lile linalokufa usingizini, na kundi la tatu ni lile ambalo linarudishwa ili kukamilisha muda wake ulopangiwa, hapo ndio mimi na wewe tunahudhuria pamoja kutafakari nini kinatokea muda huo 2
KICHEKO MSIBANI
Vipi kinatokea kifo chako wakati wa usingizi wako? Katika mambo yanokufanya uwe Hai vinatakiwa vitu vitatu, katika vitu hivyo kimoja tu ndio muhimu sana, bila ya hicho hakuna uhai, Kitu chenyewe ni hiyo Roho ambayo ni wewe lakini hujijui, Unapolala usingizi (Body)yako inabakia, Pumzi zinaendelea ila yuko wapi Mwenye kusikia ? Yuko wapi? Mwenye kuona, Ni yupi wakati huo Mwenye ku (Experience)Nani Mwenye kupanga na kufikiri, Yuko wapi Mwenye mke na watoto wakati huo, Iko wapi mali yako ukiwa umelala , ziwapi Jeuri na kiburi, iko wapi ile kauli unanijua mimi nani?, yako wapi Mabega yako unayo nyanyua juu na kuwabeza wenzio, Yawapi majivuno yako, Jee ile mipango ulopanga unataraji kuitekeleza, vyote hivo vina (Dissappear) Kwenye Muujiza huu wa usingiza ushawahi kuzingatia tukio hili ambalo unalifanya kila ukipanda kitandani, unaweza kusema mbona naendelea kuvuta pumzi?, Utajibiwa kazi hiyo hata (Machine) Inaweza kufanya , Mtu anakua kashakufa wanasubiriwa watu wake ndio izimwe (Machine) Wanokwenda pale kumtizama wanamkuta anavuta pumzi kama kawaida kumbe ile ni (Machine) ina (Pump oxygen) lakini Mwenye hiyo (Body) yuko wapi?. Napenda uelewe hiyo (Oxygen) ni Daraja katika madaraja ya kuunganisha Mwili wako na Roho, na hii (oxygen) ya kutengeneza sio ile ya (Natural)inokuja Na kitu Maalum kitokacho kwa Mollah wako ambacho ukikijua kitu hicho kilichomo kwenye pumzi basi miezi sita kabla ya kufa kwako utajua kwamba unakaribia kuondoka kwenye Ulimwengu kurudi kwa Mollah wako Muumba. Kwa hiyo (Body) Haimaanishi ni wewe, (Body) Ni guo umelivaa unaishi nalo kwa umri ulopangiwa ukifika wakati unavua na kubaki kitu chengine kabisaa, hivo ni vitu ambavyo unatumia wewe ukiwa kwenye Ulimwengu huu, unaweza kuwa na macho yako wazi pengine yanaona, au masikio labda yanasikia, na Madaktari wanasema bado Akili inafanya kazi lakini yuko wapi yule Mwenye kujua kama vitu hivyo vinafanya kazi(The Known)Mwenye kujua ndio hiyo Roho ambayo kila ukilala inarejea kwa Mollah Mlezi, Pia Napenda ufahamu kadhia hii ya kufa na kufufuliwa unafanyiwa kila siku unayoendelea kuishi hapa duniani (Sasa kwa wale wenye wasiwasi wakuamshwa kaburini inatakiwa wazingatie sana dalili hii ya kulala na kuamka) usije ukajikuta umekaa kitako kaburini wakati wenzio wote wamelala na kuna watu wanataka kukuhoji. Naam Tendo hili au mazoezi haya ya kufa unayafanya umri wako wote Mpaka ufike ule wakati wa kufa kwa (Permanent)ambayo hurudi tena kwenye uhai huu ulokua nao hivi sasa, Kwa hiyo kuanzia sasa ukenda Makaburini au Misibani elewa na wewe Ni Maiti Mtarajiwa inaweza kuwa usiku wa leo au wa kesho au baada ya miaka lakini na wewe utaonja Umauti kwa muda na nyakati ulopangiwa, hayo ndio Mazingatio unatakiwa uishi kama utakufa kesho au Ishi kama utakufa baada ya miaka 83 ili uyafanye Maisha kuwa (Balance) usiishi kwa dhuluma wala kufanya maasi bali Ishi kwa kufanya Ibada na kumkumbuka Mollah wako Mwenye kukufanyia Muujiza huu kila usiku akikuandaa na safari hii ya kurejea kwake kama alivokuleta mara ya kwanza, Kwa hiyo baada ya kuyasikia au kuyasoma haya kuanzia sasa elewa unaishi kwa (Bonus) na wakati wowote waweza kuondoka iwe usiku au mchana, ukenda mazikoni fanya tafakuri yakuona mwenzio katangulia na wewe utamfatia wakati wowote, pahala hapo sio pahala pakuleta mazungumzo ya kipuuzi au mambo ya kidunia, hapo ni karibu na Akhera na wewe unaweza kuteleza ukaanguka ukafukiwa wakati wowote, Muombee mwenzio kwa Ikhlas apate kusamehewa ukitaka na wewe uombewe siku yako ikifika, Ona Raha na Ridhia kwa kuona Mollah wako anakupa (Chance)nafasi baada ya nafasi Uendelee kuwepo duniani na kuishi ili upate kufanya Mema, Ili upate kufanya Ibada na kila siku ukenda kulala jiangalie umefanya mema mangapi na ushukuru na pale ulipokosea omba Maghfira sana upate kusamehewa kwani wewe kila ukilala unarejea kwa Mollah wako Muumba.Mollah wangu anajua zaidi 3
Tuesday, February 24, 2026
NJIA YA KUIPATA SALA
Aslm alekum. Limekuja . Swali wameniomba muongozo japo kidogo ili na sisi wasomaji wako tupate faida. Na swali la lenyewe tunakuomba tupe uchambuzi wa aya ya 45 iliyomo kwenye sura ya (An-Kabut)Tunaomba ufafanuzi kwa sababu aya hiyo inasema Sala inatuepusha na machafu na maovu, Na sisi tunasali kama wengine wanavosali, ila sisi bado tunaendelea na maasi na machafu, Na hali hii inaendelea miaka nenda miaka rudi na tumeshindwa kabisa kujivua katika katika kadhia hii ya uchafu na maovu. Naam Kwanza kabisa wacha niweke wazi mimi ni msafiri mwenzenu tumo kwenye meli hii ya Dunia tuna kwenda kwenye safari hii ya Ulimengu tunazungumza na nyie kwa kile kidogo alichotupa Mwenye enzi Mungu katika elimu zake, na ikifika wakati kila mmoja wetu anateremka na kuachia wengine waendelee na safari hii ya Maisha, Kwa hiyo kazi yangu mimi sio kusomesha (hiyo ni kazi ya Masheikh)kazi yangu mimi ni kukumbusha kile ulicho sahau, Naam sasa twendeni kwenye swali lenu lenye kuhusu hiyo aya mloitaja, Ama kuhusu kuendelea kwenu na maasi na machafu wakati mnasali inakushangazeni wakati (Quraan) imetoa Ahadi hilo nishalizungumza kwenye makala ya (Dawa ya Dhanbi)Lakini leo ntatoa tena ufafanuzi ili niongeze (Dozi)ya hilo swali ili mtibu maradhi mlonayo.Katika darsa hii wacha nikukumbushe kitu, katika harakati zote hizo lazima upate taa ya Mwenye enzi Mungu kwa njia ya Neno au ufahamu ndio utaweza kutekeleza kwa ukamilifu agizo la utiifu kwa Mwenye enzi Mungu, kwanini nikasema hivyo? Kwa sababu bila ya kupata taa uongofu huo itakua Taa inawaka lakini wewe (Still) Huoni bado upo kwenye kiza. Nikisema (TAA)(Light)Nina maana gani?, Maana yangu kuwa Uislam ndio dini pekee iloanza na Neno Soma, kwa hiyo Dini inakutaka usome kwanza ili upate kufahamu, ukisha kufahamu ndio matendo yako yote yatakua na mafanikio, sio ufate tu ukiambiwa, kwa hiyo ukisoma utapata kujua vipi Neno lina nguvu ya kubadilisha mwenendo wa mtu, Hapa wacha niwape kisa ili kukuonesheni nguvu ya neno linavopasua moyo na ujumbe kufika kwenye roho na ukaacha maasi na machafu mara moja, Lakini kwanza ifahamike Mwenye enzi Mungu hakubadilishi mpaka utake Mwenyewe kubadilika, kama anavosema kwenye sura ya (RAD aya ya 11), kwanza napenda ieleweke kuacha kuna aina mbili aina ya mwanzo unaacha hapo hapo, ukipata (Single spike)Ya neno likapenya kwenye Roho yako sio kwenye Akili basi unabadilika daima, na aina ya pili unaacha kidogo kidogo mpaka unatambua haya mambo hayana faida kwangu wala hayanipi furaha ila kunipa matatizo sasa na baadae. Sasa nifanye nini,? wacha tukisikilize kisa cha Tajiri Mmoja aliyeishi Iraq akawa na yeye mtenda maasi kama wewe na huku Ana sali Anafanya ibada lakini anaendelea na Maasi.kisome au kisikilize kisa hiki kwa mazingatio makubwa inaweza kuwa na wewe ni sababu yako ya kuacha maasi na ukaendelea na Ibada. Alikua tajiri huyu Akiishi kwenye nchi ya (Iraq) Na ikawa kawaida yake akialika watu kwenye (Party)zake wao wakiziita (Samra, au Raksa) au (Sumsumia)ila kwa lugha yenu ya sasa wacha tuite (Kizaizai). 1
NJIA YA KUIPATA SALA
Aslm alekum, Mambo yanofanyika katika (Kasri) ya Bwana huyo hayasemeki, wanaingia wanawake wamefunga vioo kwenye viuno ukiwatizama mpaka wewe mtazamaji unapata kizunguzungu kwa jinsi wanavocheza, muziki na mvinyo unagaiwa bila ya kikomo watu wanalewa na kufurahi yote hayo kutoka kwa fadhila za Bwana aitwaye (Ashraq bin Malik), Siku moja katika baadhi ya hizi (Party) akawa anapita Mcha Mungu Mmoja kwenye hilo kasri akasikia kelele za ngoma na watu wanaimba mara akafungua mtu mlango anatoka nje na hakuwa mwengine ila mfanyakazi pendwa wa Ashraq bin Malik anakwenda kutafuta ongezo la mvinyo ambao ulikua umekwisha, kwa bahati wakakutana uso kwa macho na huyu Walii aliyekua anajipitia njia ndio Akamuuliza nani nani huyu anafanya (Party)hii , yule Mfanyakazi akajibu Bwana wa mabwana (Ashraq bin Malik)ndie anafanya hii Party, yule Walii Akamjibu neno moja tu akamwambia(Laaillah Illah Allah) nilijua atakua Bwana wa mabwana kwa sababu Mtumwa wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya haya, huyoo yule Walii akashika njia na kuzama mitaani, mfanyakazi akanunua ulevi kufika juu ikawa kachelewa kidogo (Ashraq bin Malik) akamuuliza mbona umechelewa?, yule Mfanyakazi akamuhadithia yale mazungumzo na yule Mcha Mungu akamwambia kasema kwanza kabisa Katamka Laaillah Illa Allah , ikisha akasema Mtumwa (Abidi)wa Mwenye enzi Mungu hawezi kufanya mambo haya, kusikia maneno hayo pale pale (Ashraq bin Malik)Alitoka mbio kumtafuta yule Walii akamwambia umesema maneno makubwa yamepasua Moyo wangu kuanzia leo mimi nimeacha kila kitu, nimeacha mali yangu na nimeacha family yangu mimi kuanzia sasa nataka kuwa mtumwa wa mwenye enzi Mungu, yule walii akamwambia ewe (Ashraq bin Malik)Mollah wako kakupenda kakupa mali zote na furaha yote ulonayo kwa ajili ya mapenzi yake kwako, (Ashraq) Akajibu na mimi kuanzia leo naacha kila kitu kwa Ajili ya Mollah wangu muumba, Na kuanzia leo sitovaa viatu tena kwa sababu Mollah wangu kaniita bila ya viatu vipi leo mimi nirejee nikavae vitu, ndio kuanzia hapo (Ashraq)akajulikana (Kwa jina la Darweish asovaa viatu)Na akasamehe Mali zake na Kasri lake akawa Mcha Mungu mkubwa kwenye Jiji la Iraq, family yake walimbebeleza sana arudi nyumbani lakini hakutaka tena akawa ni mwenye kumsabahi Mollah wake na vikao vyake ni vile vya wacha Mungu tu, ikapita miaka miwili mitatu watu wake wa nyumbani wakamsihi akawatemblee japo kwa masaa tu wamuone, basi ikapangwa siku wakamualika kahawa akawa amekaa kwenye varanda na watu wake anakunywa kahawa kwenye urefu wa kama ghorofa moja hivi, mara huku chini wanapita vijana wanadhikiri chini mtaani huku wanasema kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge, kama kweli mpenzi wa Mungu chupa ujiunge nasi, mara wanasikia makelele Ashraq bin Malik Juba linazunguka hewani kachupa mpaka chini, alipofika chini wale vijana wote wakatawanyika wakenda mbio, mara wanamuona Ashraq bin Malik ananyanyuka anakumta juba lake wakarudi wakamuuliza hujaumia akawajibu yule alonambia nichupe atashindwa kunidaka, vijana wakatizamana machoni, Ashraq akwaambia nikadhani nyie wapenzi wa Mungu kumbe ni mdomoni tu lakini bado hajaingia moyoni, nendeni mkajizoeshe mpaka Mollah wenu ajae moyoni hapo ndio mtakua mesimamisha Sala. Sasa tunaingia kwenye Aya mloileta pengine na nyinyi mnataka neno moja muwe kama Ashraq bin Malik, lakini tukumbuke kuacha ni aina mbili, ya kwanza ni aina ya Ashraq bin Malik, hapo hapo unaacha kila kitu na ya pili hii ya taratibu anasema (Mshairi) (Nilipogundua mimi kwenye Moyo wangu anakaa asiekua wewe, nilifanya jitihada, kila njia kuujaza muongozo wako mpaka akawa hakai asiyekua wewe) sasa wacha tuingie kwenye hii Darsa soma kwa makini na wewe uwache maasi yote, sasa Ufanye nini? 2
NJIA YA KUIPATA SALA
Aslm alekum. Aina ya kwanza ni kupata uongofu wa taa ya Mollah wako ukaacha hapo hapo na aina ya pili ndio hii aya mloileta kwenye swali lenu kutoka kwenye aya ya 45 sura ya Ankabbot? Linasema hivi:
ٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَصۡنَعُونَ"Soma uliyoletewa Wahyi Katika kitabu na usimamishe Sala, Bila shaka (Sala ikisaliwa vizuri)Humzuiliya anaye sali na mambo machafu na maovu, na kwa yakini kumkumbuka Mwenye enzi Mungu ni jambo kubwa kabisa, na Mwenye enzi Mungu anajua mnayoyatenda" Naam ukweli wenyewe hii aya imeshajibu swali lenu lakini tunapishana katika ufahamu, Tatizo liko kwenye hiyo sala unaisali vipi?. Imepambanua hii aya halafu jibu rasmi tutalipata kwenye aya nyengine lenye kuitilia nguvu aya hii twende taratibu usikurupuke utakua hujafahamu kitu, najua litawagusa hili lakini itanibidi mnipe nafasi nifafanue kidogo ili mpate kuamka usingizini, pengine mja bado kalala japo anajiona yuko macho.Sala ziko za aina mbili aina ya mwanzo ni ile inotegemea Akili na aina nyengine ni ile inayo saliwa na Roho, hii ya Akili ndio wengi wetu Muadhini akinadi sote tunakimbilia msikitini na hapo vinaendelea vitendo vitupu ndio maana utajikuta mara upo bank mara upo ofisini, mara unamfikiri mkeo mara unakumbuka madeni, mara chache sana kuipata Sala yenyewe ndio maana ukitoka hapo unakwenda kuendelea na vitendo vyako viovu na machafu ya kuzini, kula rushwa kudhulumu kuiba, kusema uongo na kudhulumu masikini haki zao na hali ya kuwa umetokea msikitini kwa sababu kwenye hiyo sala yenywe wewe hupo kabisa madeni yanakuja hapo, Mara unamdai mtu hii ndani ya sala Mollah wako ulomuendea humkumbuki kabisa, Lakini yeye Ana kusubiri kwenye enzi ya kusubiri , anakungoja labda utatubia,bado umo kwenye Level ya kwanza ya Uislam,unajua kwanini? K kwa sababu Huzijui (Level)ya sala yenywe. Salah ina (Level 3) Sala ya mwanzo ndio niliitaja hapo juu ni (Level 1), na (Level 2) ya pili Hii ni ya Muumin (Fii Salat Ghashiun)Sala hii sasa niya unyenyekevu (Empty) hakiji kitu ndani ya Sala isipokua kumsabahi Mollah na kumtukuza hayaji mambo ya kidunia kabisa, Hii ndio ile Sala ya (Ghaib)ilothibiti Imani na matumaini halafu kuna hii (Level 3) Sala ya (Shahadat)ambayo hiyo imejaa (Taqwa)Mwanzo mpaka mwisho wa hiyo Sala inasaliwa Kiroho ndio za Mawalii na wacha Mungu wakweli mara utamuona mtu machozi yana miminika kwa sababu Sala imegusa kitu kisicho onekana. Kwenye (Level) hii wewe unageuka kuwa Shahid na hiyo ndio iwe (Target) yako ungali ukiishi kwenye Ulimwengu huu, Na Wakati wa kufa kwako, Naam sala hii inapatikanaje hapa nitakupeni(Dalili) halafu utaangalia mwenyewe unasali vipi kiroho au kutumia Akili. Aya inasema "Soma katika uliyoletewa wahyi katika kitabu na usimamishe Sala"Ulipoambiwa Soma umefundishwa uzingatie yaliyomo kwenye hichi kitabu ndio iwe muongozo wako ndio iwe taa yako, hayo utakayo yasoma ndio yatakufundisha usiibe, usizini, usidhulumu, usiseme uongo, usidhuru wenzio, usile rushwa, yaani kila ukisoma basi utakuta kuna mafundisho ambayo itakua muongozo na ndio taa yako itakayo kuepusha kwenye msitu wa mchana wa hayo machafu na maovu quraan itakua inakushitua, usome wahyi huu, halafu ukishasoma ufanye nini? Udumishe kumkumbuka Mollah wako aliye Mkubwa, kwanini ikawa umkumbuke kwa sababu ni jambo kubwa kabisa kivipi?Ukimkumbuka Mollah wako kila mara utaona kuna vitu viwili tafauti moja ni Sala na na la pili kukumbuka.nini kukumbuka? Ni (Awareness )(Hadhir)na unapofanya hivyo huipi Akili kupenyeza jambo lengine na Akili ikiwa haipewi nafasi inafanya nini? Ina kufa(au kutulia) Akili ikifa ndio mwanzo wakufunguliwa juu yako mambo mengine, (Elimu zengine)(Na Hekima nyingi)Sala yako sasa itakua tafauti, ucha Mungu wako unakua wa hali ya juu ila kufikia hali hiyo inabidi usubiri mlangoni kwenye kukumbukuka, kuna mambo mawili Mwanaadamu Huna uwezo nayo huwezi kuyatafuta ila yanakutafuta wewe, Kifo na Mapenzi viwili hivyo Huna uwezo navyo kabisa lakini kaa mlangoni gonga mlango asaa utafunguliwa itumie quraan au yatumie Majina 99 ya Mwenye enzi Mungu mlango ukifunguliwa utaacha machafu yote na maovu yote na utakua unapata Sala yako kikamilifu na aya inamalizia kuwa Mwenye enzi Mungu anayajua yote mnayoyatenda. Huo ndio Muongozo wa mwanzo kwenye hiyo aya mloleta, ama aya ya pili inayokupa nguvu zaidi ni hii aya ya 3.3b
NJIA YA KUIPATA SALA
Aslm Alekum, Kama nilivosema huo ni muongozo wa mwanzo sasa wacha tuingie kwenye muongozo wa pili pia tunabebwa na (aya ya 78 Sura ya israa)" simamisha Sala linapopinduka jua mpaka unapoingia usiku na Quraan wakati wa alfajir imekua yenye kushudiwa" Naam wamefasir kwa ukamilifu kuhusu kusimamisha sala na wakasema inashuhudiwa na Malaika, sasa sisi tuendelee zaidi tuchambue nini neno (Shahada)?Kwanini ikatajwa Shahada, na Kwanini ikazingatiwa Alfajir? Kwanza kabisa wacha tujue Shahada yenyewe ikoje,? Shahada iliyo kusudiwa hapo ni ile Shahada ya mwanzo ,napenda uelewe Shahada ina nguzo saba kikamilifu(Katika hizo 4 ndio kubwa) Lakini zote zinategemeana na katika hilo La shahada umelibeba wewe Mwanaadamu kutokana na kuwezeshwa na Mollah wako, Amma nguzo ya Mwanzo ya Shahada ni kusikia (Ndio maana utaona mwanzo inatajwa Samia 1) ikisha inafatia (Basira 2)Kuona, halafu tena inakuja Uwepo(Present au moment of Now 3)Na baadae inafatiwa na Kumbukumbu(history 4)nguzo ya tano (Experience 5)Nguzo ya sita ni elimu(Knowledge)au ita kujua na ya saba ni hiyo (Silent)Ukizipitia hizo zote hapo ndio utajikuta wewe mwenyewe jiite utakavo (Roho) Au (Human being) hizo ndio (Level) za Shahadat ambazo mja unatakiwa kuzitambua unaposema neno Shahidi, ujue umekusudia nini ama una shuhudia nini?, Sasa kwanini ikatajwa nyakati za Alfajir?. Tukitaka kulijua hilo tukihudhurie kwanza kisa kilichomo kwenye (Quraan) Kuhusiana na wale (As-Habul-Kahf)Kuhusiana na Kadhia ya kusikia ili tupate kujua kwani kusikia kuna faida gani, Mollah wako ?Alifanya nini, (Quraan aya ya 11 sura ya Al-Kahfi) "Tukaziba masikio yao (Wakalala hawasikii chochote) Katika pango hilo kwa idadi ya miaka mingi. Wameondoshewa uwezo wa kusikia ili wapate kulala, hata wewe unafanyiwa kitendo hicho kila usiku ukenda kulala, bila kuondoshewa uwezo huo utakua hulali kabisa, kumbuka huna uwezo wewe wa kuzuia usisikie, ( Natural)Huwezi kufanya usisikie, ukiziba masikio (Still) Utasikia sauti Nyengine ambayo pia ita ku (Disturb)Utaipa jina (Tinnitus), sasa baada ya kujua hayo Sayansi inasemaje katika hili, Wanasema wanasayansi Kusikia ni kitu cha Mwisho Mwanaadamu anapolala kuondoka, Kwa Sababu kusikia ndio chanzo kinachoiweka Akili (Active)Ukiondoshewa Uwezo wa kusikia Akili inajizima (Data)Na kuanza (Kudelete)Mambo ya mchana kutwa. Na ikiwa haijazimika inabakia (Alert) utaona kelele kidogo umeshituka, Wagonjwa walio kwenye (Coma) Wanapata kusikia ndio maana (Akili)zao zikitizamwa zinafanya kazi, kwa sababu ya sauti, wakaendelea kusema Wachunguzi wa Sayansi ya usingizi sauti zinakuzuia kupata (Deep sleep)Mwanaadamu katengenezewa (System)Maalum itwayo (The Reticular Activating System) Hii (RAS) ndio inayokuweka (Awake,conscious, Aware) Na sikio ndio Sehemu yenye nguvu ya kupitisha sauti za kila aina, hiyo (RAS System) inapofungwa au kufunikwa ndio Mwanaadamu anapata (Deep unconscious sleep) Akili haipat (Sensory disturbance) ndio inapoingia kwenye (Minimal activity ) hapo ndio unapata nafasi ya kufuta yale yote yasokua muhimu na mengine kuyaweka kwenye (Memory) Ukiamka usha (Deleted) Unakuwa mweupe hukumbuki mengi yalopita jana. Sasa nini kinatokea unaporudishiwa uwezo wa kusikia, Jambo la mwanzo linalo rudi ni kusikia, ila wewe kwakua huko (Aware) unadhani ni kufungua macho, Lakini ukichunguza utakuta jambo la mwanzo ni kusikia kama ulivokuja duniani wakati wakuzaliwa, (Umo kwenye darsa ya simulizi ya kusikia katika fani ya Shahada zingatia sana Miujiza ya Mollah wako ikisha useme Ametukuka mbora wa Uumbaji) Naam Sasa kumbuka ikiwa ulipokuja kwenye Ulimwengu kwa mara ya Mwanzo ni kusikia basi elewa na jambo la mwisho pia itakua kusikia itakua sauti (Kwa hiyo kuweni na tahadhari mkiwa kwa wagonjwa mahtuti wanokaribia kufa kumbukeni wanasikia mnayoyasema yote), Sasa kwanini ikatajwa (Quraan) Wakati wa Alfajir ni kwa sababu kinachoingia na kusikiwa Mwanzo ndio kina kua (Pure) kina kaa kwa muda mrefu kina kuwa Na (Direct communication) Na Roho yako, hapo kinakupa (Deep Meaning) Ufasaha wa wazi , sasa ikiwa tabia yako kusoma, kusikiliza, Quraan nyakati za Alfajir wakati una Sali au baada ya sala ndio nyakati hizo za Alfajir unapata hiyo (Hudan lin-nasi)Muongozo kutoka kwa Mollah wako(Al-Baqarah 120) Ukiufata sawa sawa muongozo huo ndio itakua taa yako (Torch) ya kukumurikia njia kwenye huu msitu wa dunia ulojaa maasi, hapo ndio unapata (clear Picture) Wewe usitende Dhanbi, usile rushwa, usidhulumu, Usizini, unapata ufafanuzi wa mambo hayo kama ulivopata ufafanuzi wa hii kadhia ya kusikia na mahusiano ya Quraan Alfajir, kila kitu kinafunguliwa kwako kunakua kweupe, na pia utapata maelekezo ya mambo mema mchana kutwa ikiwa umeyashika sawasawa mafunzo ulopitia Alfajir yenye Uongofu kutoka kwa Mollah wako, Maisha yako yatabadilika ikiwa Quraan itajaa kwenye moyo wako ikiambatana na tafsiri yake , itakupa uwezo wa kuacha Maasi na kuipata Sala yako sawa sawa bila ya upungufu, utaacha maasi na Sala zako zitakamilika bila ya wewe kuyarejea maasi, hii ndio ngao ya pili, kumbuka ya Mwanzo kutumia jina La Mollah wako kwa ukumbusho na hii ya pili kukisoma kitabu chake kama Muongozo. Mollah wangu anajua zaidi. 4
Wednesday, January 7, 2026
WASIA WA NDOA
Aslm alekum.
Amesema Bwana Mtume s.a.w "Atakapo funga ndoa Mja Amekamilisha nusu ya Dini, Nusu ilobakia ni Kumcha Mollah wake" Yamesemwa maneno haya na kipenzi chetu alotuletea uongofu Katika Ulimwengu huu, Sasa kwanini akayasema haya hususan kwenye sehemu na pahala kama hapa kwenye (Nikkah) Ndoa. Amechukua Bwana Mtume s.a.w nusu nzima ya dini na kuiweka katika kitendo cha kufunga ndoa, halafu akaichukua nusu ya pili akaiweka kwenye Ibada, halafu akasema ukifanya Mawili hayo basi wewe ushakamilisha dini, na unakua huna mashaka tena katika hii dunia, Sasa kwa wale wenye kutarajia kuoa pitia au usikilize wasia huu ili upate muongozo wakuingia kwenye ndoa ukiwa umejiandaa kikamilifu, Na wewe ulokwisha kuoa sikiliza kwa makini Asaa unaweza kurekebisha mambo ambayo ulokua huyajui ukaijenga ndoa yako kuwa Imara, Sasa kwa pamoja tuzitafute nusu hizi zimepatikana kutokea wapi?
Twendeni pamoja ikisha tuanzie kwenye Quraan aya ya 26 sura ya (Al-Aaraf)
يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًۭا يُوَٰرِى سَوْءَٰتِكُمْ وَرِيشًۭا ۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌۭ ۚ
ذَٰلِكَ مِنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ Enyi Wanaadamu hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za Ucha Mungu Ndio bora ,Hayo ni katika ishara za Mwenye enzi Mungu ili wapate kukumbuka.
Naam huku ndio yalipoanzia , Wazee wetu Adam a.s na bibi Hawa walipokua kwenye Pepo Walikua wako huru Hawana fahamu ya sehemu zao za siri, Lakini baada ya Shetani kuwashawishi wakapata fahamu Awareness na kujitambuawana viungo vyengine ndipo walipoona haya na kuanza kujihifadhi kwa mikono yaondipo Mungu akawapa fahamu wakaweza kujihifadhi kwa kutumia majani ili wajistiri, kwa hiyo hapo utaona jambo la kujistiri lime token mbali sio tu kujihifadhi kwa wanaadamu wenzako hata kwa Mollah wako kunahitaji heshima hiyo ndio maana hata tukisali tunajihifadhi, Kwa huzuni walokuwa nayo na kujuta kwao Mwenye enzi Mungu akawafundisha maneno ya kuomba msamaha ili wapate kumkumbuka kwa toba na Ibada ndio akawaambia guo moja la kuhifadhi tupu zenu na hili la pili ni hiyo Body yako ambayo unatumia kwa kumuabudu Mollah wako kuanzia Akili moyo kichwa kumsujudia Moja akaitaja limeteremshwa sasa kwanini likateremshwa Waulize Wanasayansi watakwambia Katika vitu vyote vyengine tunaviona na kugundua kwenye Sayari zengine isipokua Lakini kuna kitu kimoja tu ambacho hatujawahi kukuiona kwenye Ulimwengu huu, Nini kitu hicho? ni Miti hawajawahi kuona pahala popote huko juu wameona madini kama dhahabu, diamond lakini hajakutana na forest kabisa, Mambo yanashangaza ndio yana thibitisha kutremshwa kwa miti, kwa maana hiyo wakathibitisha miti pia ni life na pia ni biology na nguo zetu zinatokana na hizo mbao.1
WASIA WA NDOA
Aslm alekum Kwa hiyo guo la mwanzo ni Miti (Wood) ndio maana utakuta mti unaviashiria vya (Uhai) Kama vile kunywa maji na kadhalika, na guo la pili ni huo mwili wako ambao baada ya muda unakufa na kuuwacha ukazikwa, Ndio maana kwenye aya ya (187)Sura ya (Baqarah)Ilipitolewa Ruhusa ya kukutana kimwili na wake zenu usiku wa Ramadhani ikasemwa "Wake zenu ni nguo kwenu na nyie ni nguo kwao", Nataka Uelewe (Body)Yako ndio inokutana na mwenzako, ndio maana katika Uislam mnaamrishwa mkimaliza kukutana mkakoge kabla ya kufanya Ibada, Kwa sababu hiyo (Body)yako ni vazi la Ucha Mungu usilipeleke wakati hujakua (Tohara) sio msafi, Ndio Bwana Mtume s.a.w "Akasema Nusu ya mwanzo ni kuoa na nusu ya pili ni Kumcha Mungu.
Naam ukiyapata yote Mawili basi umekamilisha Dini, Sasa nini Ndoa ? Neno lilotumika kwa (Arabic ni Zawj)Ni sehemu moja ya (Pair) Ni wajibu wako kutafuta ile sehemu ya pili kukamilisha hiyo (Pair) Kwani ni kama (Viatu) Huwezi kukivaa kimoja lazima upate cha pili ndio utaweza kutembea vizuri, Wajibu wako kumtafuta (Soulmate) wako ambaye mtaishi pamoja kwenye Ulimwengu huu.
Huyo mwenza ni Roho nyinyi mloandikiwa mkutane na Mollah karim ili muishi kwa furaha na msaikilizano pale mtakapo kamilisha muungano wenu, Ndoa haina maana pekee ya mume na mke , ina maana ya upeo yakua huyo ni mwenzio mwenza Mollah alokukutanisha nae ili muwe pamoja, hakutaka Mollah wako uishi maisha ya upweke au peke yako, Na kumbuka kama ulivoambiwa ndoa ni kama mfano wa nguo hakikisha ina kaa vizuri kwenye (Body) yako ikikubana itakukera na ikipwaya itakuvuka kwa hiyo hakikisha inakaa sawa na kuku(Fit).
Ndoa ni kwa yule Atoridhi Roho yako na kuishi vizuri na wewe kwenye maisha haya, Pia iliposemwa Mke na mume ni kama nguo ilikua na maana nguo inakustiri , inaziba mapungufu yako, nguo ni kitu cha karibu kwenye (Body)yako, kwa hiyo ni lazima kihifadhi kasoro zako, Mke au Mume Mwenye mapenzi anahifadhi siri zako, Analinda heshima yako. Mume au Mke sio mtu ambaye Ana kununulia Maua tu, Mume ni Mtu ambaye ni mizani kwako wewe ni lazima mpate (Balance)Kwenye mizani yenu ya maisha, Kila kitu chenu kiwe kimoja, mawazo yenu yawe yanalingana, tafauti zenu ziwe zinayayuka kama barafu ilokutana na jua, mmoja akiwa juu basi mwengine akubali kujishusha na kuwa chini katika masikilizano, Quraan ilipomwita mume na Mke hakiua na maana ya cheo cha sheria ilikua inawaelekeza wawili nyie kusaidiana, kwa yale ambayo mwenzio atakua na mapungufu nayo, Ndoa sio kumtawala Mtu na kumfanya kama mali yako, Ndoa ni kipimo cha nusu kwa nusu kwenye kibaba cha mapenzi baina ya wawili nyie, Kwa hiyo kumbuka unapoitwa Mume wewe hujatimia peke yako mpaka apatikane mkeo ndio uwe kamili, Katika lugha ya kiarabu (Zawj)Haina maana (Spouse)Ina maana ni sehemu ya nusu ya mwenzio, bila ya mwenzio wewe hujatimia , kwenye ndoa umeambiwa ni sehemu ya kupumzika upate utulivu kwa mwenzio(Litaskun ilahiya) Haina maana utapata mbora katimia, hana doa laa ni sehemu ya kupata (Rest)Kupumzika kwa ukamilifu kutokana na mashaka yote ya Ulimwengu. 2
WASIA WA NDOA
Aslm alekum.
Ukitaka ndoa ya uhakika yenye kheri sio ujitukuze Mwenyewe, Ufanye mambo peke yako, Uwe (Selfish)Hichi changu hichi chako hapo tayari ushaigawa ndoa, Usijitukuze peke yako hili nimefanya mimi, Watoto nimelea peke yangu, hizi ni mali zangu, ndoa ni kusaidiana , mkisimama mnasimama pamoja na mkianguka mnaanguka pamoja, kwenye ndoa lazima iwepo njia ya kusameheana, kuombana radhi na kuepuka mambo yanayo karibisha kuchafua ndoa, na kubwa la mwanzo katika hayo ni kukaribisha mtu wa tatu ambaye ni kimada, Kwanini ndoa ina haribika kwa sababu Roho inaona hususan ya Mwanamke, Ndio maana utaona Mwanamke Analia na Na Mwanamme anahuzunika unajua kwanini?,
Kwa Sababu ikumbuke aya ya Mwenye enzi Mungu wewe ndio guo lake na yeye ni guo lake, Sasa vipi leo unakwenda kumchafulia guo lake, kwenye (Level) ya kiroho anapata habari kuwa sasa unacheza, ama hisi guo umerudi nalo chafu, kumbuka jambo moja mnapokutana Mke na mume kimwili Mollah kakujaalieni Maji tu mnasafika, Lakini ukiingiliana na Mwanamke wa Nje Uchafu unabakia (Wamefanya utafiti) na kugundua (DNA) yako inabakia kwa miezi kadhaa ndani ya guo lako na huyo mwengine, kama mtapimwa basi yatakutwa mahusiano yenu kwamba mlifanya tendo la maingiliano baina yenu, Ikiwa (Forensic science) Inakukamata ni habari yetu sisi kwa Mollah wetu, na maisha yetu ya ndoa hapo ndio kinaanza kifimbo cheza kutokea Mbinguni, hapa Ulimwenguni si hamfati sheria hampigani mijeledi 80, nini kinafatia unaanza kupigwa kwa Nakama,
Yanaanza Maugonvi, Upungufu wa mali, matatizo ya Riziki, kwenye Nyumba hakuna utulivu, Pesa sasa haikai, kazi haipatikani, Machafuko mengi kwenye ndoa yenu na la mwisho mapenzi hayo yanakimbia.
Naam lakini ukisikiliza Maneno ya Bwana Mtume s.a.w anakwambia nusu ya kwanza funga ndoa, halafu nusu ya pili mpende Mwenye enzi Mungu kwa Ibada na kumkumbuka nini kinatokea?,
Mapenzi kama (Mirror) kioo ukijitizama unajiona ukipenda utapendwa na Mollah wako ndio hapo inatimia Ahadi yake ya kukushushia Mapenzi na Rehema zake zitokazo kwake Napenda uelewe kuna vitu viwili hata ukivitafuta huvipati ila vinakutafuta wewe kwa time yake, vitu hivyo ni Mapenzi na kifo, Hata ufanye nini huna uwezo nao isipokua atake Mwenye enzi Mungu, Ukimpenda Mungu ukafanya Mema basi Mollah anakuteremshia Mapenzi unampenda mkeo na mkeo anakupenda mapenzi makubwa mpaka nyote mnajiuliza hichi nini?
Mbona kama layla na majnu, uko njiani unatamani chakula fulani ukirudi nyumbani unakuta hicho ndio kapika mambo yanakushangaza kila saa na dakika unajikuta umezama mapenzini, na hiyo ndio furaha ya dunia, furaha ndio afya ya mapenzi, hapo tena zina zidi kushuka Rehma na baraka nyingi nyingi kutoka kwa Mollah wenu Karim mnakua ndani ya (Bliss)Na maisha yanakwenda vizuri, mnaongezewa kizazi,, mnapewa riziki kwa wingi. Kuyapata yote hayo lazima mzijue siri ya maisha ndoa na kanuni zake kama vile kutobishana mbele za watu, kuwa wavumilivu, kuleta subra kwenye migogoro, umpende mkeo kiroho na awe rafiki yako, epukeni kubishana mbele za watu, himizaneni kwa njia ya upole kufanya ibada, msiambieni uongo, usimtukanie wazee wake na watu wake, tumia lugha nzuri, usiwe na wivu wakufikiri, na Inshaalah Mwenye enzi Mungu atakujaalieni Maisha ya Furaha.3