فَٱلْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ ءَايَةًۭ ۚ وَإِنَّ كَثِيرًۭا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنْ ءَايَـٰتِنَا لَغَـٰفِلُونَ(Basi leo tutakuokoa ili tukuweke uje kuwa mfano kwa watakaokuja baada yako,Na watu wengi wameghafilika na ishara zetu. Naam kwanini ikawa mfano Kwa sababu Firaun alijisahau kama mimi na wewe ikafika mpaka kujiita Mungu kwa ajili ya cheo chake cha ufalme, akifanya alofanya mpaka khofu ikamuondoka, sasa kuwachwa kwake kwa hiyo Body ni kujulishwa sisi( body )itabaki, lakini kuna kitu kitaondoka ni ishara ya kutukumbusha sisi body sio wewe, ila kuna kitu chengine chenye mahusiano na mwenye enzi Mungu ambacho unatakiwa kukizingatia, na hii leo ndio madhumuni ya darsa hii ya kifo ili uwache kughafilika na kucheka misibani na kuleta mazungumzo yaso maana , kuanzia leo usichukulie kifo ni jambo la kawaida ni jambo zito ambalo wewe unalifanyia mazoezi kila siku, Ewe ndugu yangu wa kiislam kwani wewe si unapata usingizi kila unapoingia usiku, Unaujua wewe nini usingizi, wacha nikupe habari ya usingizi ili upate kuzinduka ujijue na wewe vilevile ni maiti mtarajiwa mwenzio tu katangulia na wewe wakati wowote unaweza kufatia, napenda ufahamu kuanzia leo kila ukenda kulala kitandani unatia saini yako ya kufa wewe kila usiku unakwenda safari hii bila ya kujijua unakwenda wapi, Miujiza hii unaitenda kila usiku, Ushawahi kujiliza unakwenda wapi?pahala unapokwenda wewe ndio alipokwenda huyo Maiti unae mpuuza wakati anafukiwa kwenye udongo mzito, sasa kuanzia leo Jiulize hivi mimi usiku nakwenda wapi ?, na kama unaogopa kujiuliza Mwenyewe acha nikupe dalili wapi unakwenda ikisha utaamua Mwenyewe nilete heshima na Taqwa nikiwa mazikoni au msibani , au niendelee kujificha kwenye chaka la mazungumzo kuepuka siku hii nzito ambayo na mimi itanikuta, basi kama upo tayari tega sikio uijue safari yako unayokwenda kila siku unayoishi duniani, kumbuka kila ukisema Innalillah waina Illahi Raajiun uijue na maana yake, sio unasema ikawa iko mdomoni lazima izame ndani ya Moyo ujijue unatamka maneno gani, maneno hayo na wewe yanakuhusu na kila ukilala tambua unakwenda sehemu Adhim, kwa hiyo lazima uelewe sehemu hiyo unarudi vipi na kwa adabu gani na umechukua nini kama zawadi siku hiyo اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
"Mwenye enzi mungu Huzichukua Roho wakati wa mauti yake, Na zile ambazo bado kufa kwake huzichukua nyakati za kulala, (kwenye usingizi wao) Basi huzizuia zile alozikidhia Mauti, Na huzirudisha zile nyengine mpaka ufike wakati (wake)ulowekwa, bila shaka katika hayo yamo mazingatio kwa watu wanaotafakari". Naam hapo wametajwa makundi Matatu, kundi la kwanza lile linalokufa (Shuhuda) yaani wakiwa macho, na kundi la pili lile linalokufa usingizini, na kundi la tatu ni lile ambalo linarudishwa ili kukamilisha muda wake ulopangiwa, hapo ndio mimi na wewe tunahudhuria pamoja kutafakari nini kinatokea muda huo 2
No comments:
Post a Comment