Aslm alekum, Ndugu zangu wa Kiislam leo nataka kuzungumza na nyinyi kuhusu huzuni nilo nayo katika jambo la misiba yetu, Imekua desturi sasa kila nikihudhuria Maziko au kwenye misiba majumbani unakuta watu wamegeuza mkusanyiko huo kuwa baraza ya kubadilishana mawazo au number za simu, mazungumzo hapo yanakua kama yale ya Tamaduni zengine wafanyavo kama vile kunywa pombe, au kucheza na jeneza, hali hii inasikitisha sana kwani inakwenda kinyume na maagizo ya Bwana Mtume s.a.w aliposema nendeni kudhuru Makaburi kwani katika hilo kuna makumbusho makubwa kwa nyie Mlobaki duniani. Sasa kwa Mwenendo huu tulofikia hivi sasa kuna mambo mawili yamejitokeza inatupasa tuyaangalie kwa undani zaidi, ikisha tukumbushane labda tumeghafilika, Mambo gani hayo? La kwanza labda mtu haja elimishwa kuhusu kadhia hii ya kufa mtu, au jambo la pili ni njia ya kudharau maelekezo ya Mtume wetu kuwa nendeni kwenye misiba kwani kufanya hivyo kuta kukumbusheni Umauti, na hapa leo ndio tutaingia (Deep)kwenye hii darsa yetu ya Kifo ili tujue kwanini Bwana Mtume s.a.w akayasema hayo na alikusudia nini kuamrisha tuka hudhurie Maziko. Sababu kubwa ilikua ukenda mazikoni pahala palipofiwa sio iwe ndio sehemu ya kukutana na marafiki au jamaa mlopoteana, kusudio lilikua sehemu hiyo au pahala hapo ni eneo litokufanya wewe kuzingatia au kujigundua wewe nani na dhumuni lako nini kuwepo hapa ulimwenguni.Mwenye enzi Mungu kakuuliza kwenye Sura ya Dhaariyat aya ya (21)" Na katika Nafsi zenu Je Hamuoni", Umauti kazi yake kubwa ni kukumbusha na kama hujakumbuka basi ogopa sana kuna kitu ndani ya nafsi yako kimeku (block) au ukijiona upo hapo lakini unazungumzia matokeo ya mpira au siasa basi jijue bado umo kwenye lepe lepe la usingizi na hiyo ni ishara kubwa umejisahau sana, fahamu wewe ushakua sugu , na kama hujakumbuka hapo basi tunakuchia endelea kujikusanyia mali, furahia maisha mpaka siku hii ikukute kwa ghafla hali yakua umefilisikana huna kitu chochote cha kuchukua huo upande wa pili unapokwenda ama kurejea kwa Mollah wako kwenye Nyumba ya milele, Napenda kukumbusha uelewe Mauti ni Mawaidha makubwa kwenye Maisha yako, Ikiwa wewe Raisi au Mwenyekiti, Kama wewe tajiri au Daktari au kuwa maskin wa hali ya chini kwenye kadhia hii nyote mko sawa na iko siku ilee uloandika (Contract)Yako ya kuondoka hapa ulimwenguni ikifika basi jijue haitokhairishwa saa wala dakika ukifika muda lazima uondoke. Kabla yakuingia kwenye Maudhui yenyewe Mwenye enzi Mungu anatukumbusha nini kuhusu Umauti, kumbuka hapo Mwanzo wasia wa Mtume na sasa Mollah wako anakufahamisha tena kuhusu tukio hili la kifo linakuaje? 1
No comments:
Post a Comment