Wednesday, January 7, 2026

WASIA WA NDOA

 Aslm alekum.  


Amesema Bwana Mtume s.a.w "Atakapo funga ndoa Mja Amekamilisha nusu ya Dini, Nusu ilobakia ni Kumcha Mollah wake" Yamesemwa maneno haya na kipenzi chetu alotuletea uongofu Katika Ulimwengu huu,  Sasa kwanini akayasema haya hususan kwenye sehemu na pahala kama hapa kwenye (Nikkah) Ndoa. Amechukua Bwana Mtume s.a.w nusu nzima ya dini na kuiweka katika kitendo cha kufunga ndoa, halafu akaichukua nusu ya pili akaiweka kwenye Ibada,  halafu akasema ukifanya Mawili hayo basi wewe ushakamilisha dini,  na unakua huna mashaka tena katika hii dunia, Sasa kwa wale wenye kutarajia kuoa pitia au usikilize wasia huu ili upate muongozo wakuingia kwenye ndoa ukiwa umejiandaa kikamilifu, Na wewe ulokwisha kuoa sikiliza kwa makini Asaa unaweza kurekebisha mambo ambayo ulokua huyajui ukaijenga ndoa yako kuwa Imara, Sasa kwa pamoja tuzitafute nusu hizi zimepatikana kutokea wapi? 


Twendeni pamoja ikisha tuanzie kwenye Quraan aya ya 26 sura ya (Al-Aaraf)


يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًۭا يُوَٰرِى سَوْءَٰتِكُمْ وَرِيشًۭا ۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌۭ ۚ  

 ذَٰلِكَ مِنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ Enyi Wanaadamu hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za Ucha Mungu Ndio bora ,Hayo ni katika ishara za Mwenye enzi Mungu ili wapate kukumbuka.


Naam huku ndio yalipoanzia , Wazee wetu Adam a.s  na bibi Hawa walipokua kwenye Pepo Walikua wako huru Hawana fahamu ya sehemu zao za siri, Lakini baada ya Shetani kuwashawishi wakapata fahamu Awareness na kujitambuawana viungo vyengine ndipo walipoona haya na kuanza kujihifadhi kwa mikono yaondipo Mungu akawapa fahamu wakaweza kujihifadhi kwa kutumia majani ili wajistiri, kwa hiyo hapo utaona jambo la kujistiri lime token mbali sio tu kujihifadhi kwa wanaadamu wenzako hata kwa Mollah wako kunahitaji heshima hiyo ndio maana hata tukisali tunajihifadhi, Kwa huzuni walokuwa nayo na kujuta kwao Mwenye enzi Mungu akawafundisha maneno ya kuomba msamaha ili wapate kumkumbuka kwa toba na Ibada ndio akawaambia guo moja la kuhifadhi tupu zenu na hili la pili ni hiyo  Body yako ambayo unatumia kwa kumuabudu Mollah wako kuanzia Akili moyo kichwa kumsujudia Moja akaitaja limeteremshwa sasa kwanini likateremshwa Waulize Wanasayansi watakwambia Katika vitu vyote vyengine tunaviona na kugundua kwenye Sayari zengine isipokua Lakini kuna kitu kimoja tu ambacho hatujawahi kukuiona kwenye Ulimwengu huu, Nini kitu hicho? ni Miti hawajawahi kuona pahala popote huko juu wameona madini kama dhahabu, diamond lakini hajakutana na forest kabisa, Mambo yanashangaza ndio yana thibitisha kutremshwa kwa miti, kwa maana hiyo wakathibitisha miti pia ni life na pia ni biology na nguo zetu zinatokana na hizo mbao.1

WASIA WA NDOA

 Aslm alekum Kwa hiyo guo la mwanzo ni Miti (Wood) ndio maana utakuta mti unaviashiria vya (Uhai) Kama vile kunywa maji na kadhalika, na guo la pili ni huo mwili wako ambao baada ya muda unakufa na kuuwacha ukazikwa, Ndio maana kwenye aya ya (187)Sura ya (Baqarah)Ilipitolewa Ruhusa ya kukutana kimwili na wake zenu usiku wa Ramadhani ikasemwa "Wake zenu ni nguo kwenu na nyie ni nguo kwao", Nataka Uelewe (Body)Yako ndio inokutana na mwenzako, ndio maana katika Uislam mnaamrishwa mkimaliza kukutana mkakoge kabla ya kufanya Ibada, Kwa sababu hiyo (Body)yako ni vazi la Ucha Mungu usilipeleke wakati hujakua (Tohara) sio msafi, Ndio Bwana Mtume s.a.w "Akasema Nusu ya mwanzo ni kuoa na nusu ya pili ni Kumcha Mungu. 




Naam ukiyapata yote Mawili basi umekamilisha Dini, Sasa nini Ndoa ? Neno lilotumika kwa (Arabic ni Zawj)Ni sehemu moja ya (Pair) Ni wajibu wako kutafuta ile sehemu ya pili kukamilisha hiyo (Pair) Kwani ni kama (Viatu) Huwezi kukivaa kimoja lazima upate cha pili ndio utaweza kutembea vizuri, Wajibu wako kumtafuta (Soulmate) wako ambaye mtaishi pamoja kwenye Ulimwengu huu. 




Huyo mwenza ni Roho nyinyi mloandikiwa mkutane na Mollah karim ili muishi kwa furaha na msaikilizano pale mtakapo kamilisha muungano wenu, Ndoa haina maana pekee ya mume na mke , ina maana ya upeo yakua huyo ni mwenzio mwenza Mollah alokukutanisha nae ili muwe pamoja, hakutaka Mollah wako uishi maisha ya upweke au peke yako, Na kumbuka kama ulivoambiwa ndoa ni kama mfano wa nguo  hakikisha ina kaa vizuri kwenye (Body) yako ikikubana itakukera na ikipwaya itakuvuka kwa hiyo hakikisha inakaa sawa na kuku(Fit). 



Ndoa ni kwa yule Atoridhi Roho yako na kuishi vizuri na wewe kwenye maisha haya, Pia iliposemwa Mke na mume ni kama nguo ilikua na maana nguo inakustiri , inaziba mapungufu yako,  nguo ni kitu cha karibu kwenye (Body)yako, kwa hiyo ni lazima kihifadhi kasoro zako, Mke au Mume Mwenye mapenzi anahifadhi siri zako, Analinda heshima yako. Mume au Mke sio mtu ambaye Ana kununulia Maua tu, Mume ni Mtu ambaye ni mizani kwako wewe ni lazima mpate (Balance)Kwenye mizani yenu ya maisha, Kila kitu chenu kiwe kimoja, mawazo yenu yawe yanalingana, tafauti zenu ziwe zinayayuka kama barafu ilokutana na jua, mmoja akiwa juu basi mwengine akubali kujishusha na kuwa chini katika masikilizano, Quraan ilipomwita mume na Mke hakiua na maana ya cheo cha sheria ilikua inawaelekeza wawili nyie kusaidiana, kwa yale ambayo mwenzio atakua na mapungufu nayo, Ndoa sio kumtawala Mtu na kumfanya kama mali yako, Ndoa ni kipimo cha nusu kwa nusu kwenye kibaba cha mapenzi baina ya wawili nyie, Kwa hiyo kumbuka unapoitwa Mume wewe hujatimia peke yako mpaka apatikane mkeo ndio uwe kamili, Katika lugha ya kiarabu (Zawj)Haina maana (Spouse)Ina maana ni sehemu ya nusu ya mwenzio, bila ya mwenzio wewe hujatimia , kwenye ndoa umeambiwa ni sehemu ya kupumzika upate utulivu kwa mwenzio(Litaskun ilahiya) Haina maana utapata mbora katimia, hana doa  laa ni sehemu ya kupata (Rest)Kupumzika kwa ukamilifu kutokana na mashaka yote ya Ulimwengu. 2

WASIA WA NDOA

 Aslm alekum.  


Ukitaka ndoa ya uhakika yenye kheri sio ujitukuze Mwenyewe, Ufanye mambo peke yako, Uwe (Selfish)Hichi changu hichi chako hapo tayari ushaigawa ndoa, Usijitukuze peke yako hili nimefanya mimi, Watoto nimelea peke yangu, hizi ni mali zangu, ndoa ni kusaidiana , mkisimama mnasimama pamoja na mkianguka mnaanguka pamoja, kwenye ndoa lazima iwepo njia ya kusameheana, kuombana radhi na kuepuka mambo yanayo karibisha kuchafua ndoa, na kubwa la mwanzo katika hayo ni kukaribisha mtu wa tatu ambaye ni kimada, Kwanini ndoa ina haribika kwa sababu Roho inaona hususan ya Mwanamke, Ndio maana utaona Mwanamke Analia na Na Mwanamme anahuzunika unajua kwanini?, 



Kwa Sababu ikumbuke aya ya Mwenye enzi Mungu wewe ndio guo lake na yeye ni guo lake, Sasa vipi leo unakwenda kumchafulia guo lake, kwenye (Level) ya kiroho anapata habari kuwa sasa unacheza, ama hisi guo umerudi nalo chafu, kumbuka jambo moja mnapokutana Mke na mume kimwili Mollah kakujaalieni Maji tu mnasafika, Lakini ukiingiliana na Mwanamke wa Nje Uchafu unabakia (Wamefanya utafiti) na kugundua (DNA) yako inabakia kwa miezi kadhaa ndani ya guo lako na huyo mwengine, kama mtapimwa basi yatakutwa mahusiano yenu kwamba mlifanya tendo la maingiliano baina yenu, Ikiwa (Forensic science) Inakukamata ni habari yetu sisi kwa Mollah wetu, na maisha yetu ya ndoa hapo ndio kinaanza kifimbo cheza kutokea Mbinguni, hapa Ulimwenguni si hamfati sheria hampigani mijeledi 80, nini kinafatia unaanza kupigwa kwa Nakama, 


Yanaanza Maugonvi, Upungufu wa mali, matatizo ya Riziki, kwenye Nyumba hakuna utulivu, Pesa sasa haikai, kazi haipatikani, Machafuko mengi kwenye ndoa yenu na la mwisho mapenzi hayo yanakimbia. 


Naam lakini ukisikiliza Maneno ya Bwana Mtume s.a.w anakwambia nusu ya kwanza funga ndoa, halafu nusu ya pili mpende Mwenye enzi Mungu kwa Ibada na kumkumbuka nini kinatokea?, 


Mapenzi kama (Mirror) kioo ukijitizama unajiona ukipenda utapendwa na Mollah wako ndio hapo inatimia Ahadi yake ya kukushushia Mapenzi na Rehema zake zitokazo kwake Napenda uelewe kuna vitu viwili hata ukivitafuta huvipati ila vinakutafuta wewe kwa time yake, vitu hivyo ni Mapenzi na kifo, Hata ufanye nini huna uwezo nao isipokua atake Mwenye enzi Mungu, Ukimpenda Mungu ukafanya Mema basi Mollah anakuteremshia Mapenzi unampenda mkeo na mkeo anakupenda mapenzi makubwa mpaka nyote mnajiuliza hichi nini? 


Mbona kama layla na majnu, uko njiani unatamani chakula fulani ukirudi nyumbani unakuta hicho ndio kapika mambo yanakushangaza kila saa na dakika unajikuta umezama mapenzini, na hiyo ndio furaha ya dunia, furaha ndio afya ya mapenzi, hapo tena zina zidi kushuka Rehma na baraka nyingi nyingi kutoka kwa Mollah wenu Karim mnakua ndani ya (Bliss)Na maisha yanakwenda vizuri, mnaongezewa kizazi,, mnapewa riziki kwa wingi. Kuyapata yote hayo lazima mzijue siri ya maisha ndoa na kanuni zake kama vile kutobishana mbele za watu, kuwa wavumilivu, kuleta subra kwenye migogoro, umpende mkeo kiroho na awe rafiki yako, epukeni kubishana mbele za watu, himizaneni kwa njia ya upole kufanya ibada, msiambieni uongo, usimtukanie wazee wake na watu wake, tumia lugha nzuri, usiwe na wivu wakufikiri, na Inshaalah Mwenye enzi Mungu atakujaalieni Maisha ya Furaha.3