Aslm alekum, Ndugu zangu wa Kiislam leo nataka kuzungumza na nyinyi kuhusu huzuni nilo nayo katika jambo la misiba yetu, Imekua desturi sasa kila nikihudhuria Maziko au kwenye misiba majumbani unakuta watu wamegeuza mkusanyiko huo kuwa baraza ya kubadilishana mawazo au number za simu, mazungumzo hapo yanakua kama yale ya Tamaduni zengine wafanyavo kama vile kunywa pombe, au kucheza na jeneza, hali hii inasikitisha sana kwani inakwenda kinyume na maagizo ya Bwana Mtume s.a.w aliposema nendeni kudhuru Makaburi kwani katika hilo kuna makumbusho makubwa kwa nyie Mlobaki duniani. Sasa kwa Mwenendo huu tulofikia hivi sasa kuna mambo mawili yamejitokeza inatupasa tuyaangalie kwa undani zaidi, ikisha tukumbushane labda tumeghafilika, Mambo gani hayo? La kwanza labda mtu haja elimishwa kuhusu kadhia hii ya kufa mtu, au jambo la pili ni njia ya kudharau maelekezo ya Mtume wetu kuwa nendeni kwenye misiba kwani kufanya hivyo kuta kukumbusheni Umauti, na hapa leo ndio tutaingia (Deep)kwenye hii darsa yetu ya Kifo ili tujue kwanini Bwana Mtume s.a.w akayasema hayo na alikusudia nini kuamrisha tuka hudhurie Maziko. Sababu kubwa ilikua ukenda mazikoni pahala palipofiwa sio iwe ndio sehemu ya kukutana na marafiki au jamaa mlopoteana, kusudio lilikua sehemu hiyo au pahala hapo ni eneo litokufanya wewe kuzingatia au kujigundua wewe nani na dhumuni lako nini kuwepo hapa ulimwenguni.Mwenye enzi Mungu kakuuliza kwenye Sura ya Dhaariyat aya ya (21)" Na katika Nafsi zenu Je Hamuoni", Umauti kazi yake kubwa ni kukumbusha na kama hujakumbuka basi ogopa sana kuna kitu ndani ya nafsi yako kimeku (block) au ukijiona upo hapo lakini unazungumzia matokeo ya mpira au siasa basi jijue bado umo kwenye lepe lepe la usingizi na hiyo ni ishara kubwa umejisahau sana, fahamu wewe ushakua sugu , na kama hujakumbuka hapo basi tunakuchia endelea kujikusanyia mali, furahia maisha mpaka siku hii ikukute kwa ghafla hali yakua umefilisikana huna kitu chochote cha kuchukua huo upande wa pili unapokwenda ama kurejea kwa Mollah wako kwenye Nyumba ya milele, Napenda kukumbusha uelewe Mauti ni Mawaidha makubwa kwenye Maisha yako, Ikiwa wewe Raisi au Mwenyekiti, Kama wewe tajiri au Daktari au kuwa maskin wa hali ya chini kwenye kadhia hii nyote mko sawa na iko siku ilee uloandika (Contract)Yako ya kuondoka hapa ulimwenguni ikifika basi jijue haitokhairishwa saa wala dakika ukifika muda lazima uondoke. Kabla yakuingia kwenye Maudhui yenyewe Mwenye enzi Mungu anatukumbusha nini kuhusu Umauti, kumbuka hapo Mwanzo wasia wa Mtume na sasa Mollah wako anakufahamisha tena kuhusu tukio hili la kifo linakuaje? 1
Saturday, March 14, 2026
KICHEKO MSIBANI
فَٱلْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ ءَايَةًۭ ۚ وَإِنَّ كَثِيرًۭا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنْ ءَايَـٰتِنَا لَغَـٰفِلُونَ(Basi leo tutakuokoa ili tukuweke uje kuwa mfano kwa watakaokuja baada yako,Na watu wengi wameghafilika na ishara zetu. Naam kwanini ikawa mfano Kwa sababu Firaun alijisahau kama mimi na wewe ikafika mpaka kujiita Mungu kwa ajili ya cheo chake cha ufalme, akifanya alofanya mpaka khofu ikamuondoka, sasa kuwachwa kwake kwa hiyo Body ni kujulishwa sisi( body )itabaki, lakini kuna kitu kitaondoka ni ishara ya kutukumbusha sisi body sio wewe, ila kuna kitu chengine chenye mahusiano na mwenye enzi Mungu ambacho unatakiwa kukizingatia, na hii leo ndio madhumuni ya darsa hii ya kifo ili uwache kughafilika na kucheka misibani na kuleta mazungumzo yaso maana , kuanzia leo usichukulie kifo ni jambo la kawaida ni jambo zito ambalo wewe unalifanyia mazoezi kila siku, Ewe ndugu yangu wa kiislam kwani wewe si unapata usingizi kila unapoingia usiku, Unaujua wewe nini usingizi, wacha nikupe habari ya usingizi ili upate kuzinduka ujijue na wewe vilevile ni maiti mtarajiwa mwenzio tu katangulia na wewe wakati wowote unaweza kufatia, napenda ufahamu kuanzia leo kila ukenda kulala kitandani unatia saini yako ya kufa wewe kila usiku unakwenda safari hii bila ya kujijua unakwenda wapi, Miujiza hii unaitenda kila usiku, Ushawahi kujiliza unakwenda wapi?pahala unapokwenda wewe ndio alipokwenda huyo Maiti unae mpuuza wakati anafukiwa kwenye udongo mzito, sasa kuanzia leo Jiulize hivi mimi usiku nakwenda wapi ?, na kama unaogopa kujiuliza Mwenyewe acha nikupe dalili wapi unakwenda ikisha utaamua Mwenyewe nilete heshima na Taqwa nikiwa mazikoni au msibani , au niendelee kujificha kwenye chaka la mazungumzo kuepuka siku hii nzito ambayo na mimi itanikuta, basi kama upo tayari tega sikio uijue safari yako unayokwenda kila siku unayoishi duniani, kumbuka kila ukisema Innalillah waina Illahi Raajiun uijue na maana yake, sio unasema ikawa iko mdomoni lazima izame ndani ya Moyo ujijue unatamka maneno gani, maneno hayo na wewe yanakuhusu na kila ukilala tambua unakwenda sehemu Adhim, kwa hiyo lazima uelewe sehemu hiyo unarudi vipi na kwa adabu gani na umechukua nini kama zawadi siku hiyo اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
"Mwenye enzi mungu Huzichukua Roho wakati wa mauti yake, Na zile ambazo bado kufa kwake huzichukua nyakati za kulala, (kwenye usingizi wao) Basi huzizuia zile alozikidhia Mauti, Na huzirudisha zile nyengine mpaka ufike wakati (wake)ulowekwa, bila shaka katika hayo yamo mazingatio kwa watu wanaotafakari". Naam hapo wametajwa makundi Matatu, kundi la kwanza lile linalokufa (Shuhuda) yaani wakiwa macho, na kundi la pili lile linalokufa usingizini, na kundi la tatu ni lile ambalo linarudishwa ili kukamilisha muda wake ulopangiwa, hapo ndio mimi na wewe tunahudhuria pamoja kutafakari nini kinatokea muda huo 2
KICHEKO MSIBANI
Vipi kinatokea kifo chako wakati wa usingizi wako? Katika mambo yanokufanya uwe Hai vinatakiwa vitu vitatu, katika vitu hivyo kimoja tu ndio muhimu sana, bila ya hicho hakuna uhai, Kitu chenyewe ni hiyo Roho ambayo ni wewe lakini hujijui, Unapolala usingizi (Body)yako inabakia, Pumzi zinaendelea ila yuko wapi Mwenye kusikia ? Yuko wapi? Mwenye kuona, Ni yupi wakati huo Mwenye ku (Experience)Nani Mwenye kupanga na kufikiri, Yuko wapi Mwenye mke na watoto wakati huo, Iko wapi mali yako ukiwa umelala , ziwapi Jeuri na kiburi, iko wapi ile kauli unanijua mimi nani?, yako wapi Mabega yako unayo nyanyua juu na kuwabeza wenzio, Yawapi majivuno yako, Jee ile mipango ulopanga unataraji kuitekeleza, vyote hivo vina (Dissappear) Kwenye Muujiza huu wa usingiza ushawahi kuzingatia tukio hili ambalo unalifanya kila ukipanda kitandani, unaweza kusema mbona naendelea kuvuta pumzi?, Utajibiwa kazi hiyo hata (Machine) Inaweza kufanya , Mtu anakua kashakufa wanasubiriwa watu wake ndio izimwe (Machine) Wanokwenda pale kumtizama wanamkuta anavuta pumzi kama kawaida kumbe ile ni (Machine) ina (Pump oxygen) lakini Mwenye hiyo (Body) yuko wapi?. Napenda uelewe hiyo (Oxygen) ni Daraja katika madaraja ya kuunganisha Mwili wako na Roho, na hii (oxygen) ya kutengeneza sio ile ya (Natural)inokuja Na kitu Maalum kitokacho kwa Mollah wako ambacho ukikijua kitu hicho kilichomo kwenye pumzi basi miezi sita kabla ya kufa kwako utajua kwamba unakaribia kuondoka kwenye Ulimwengu kurudi kwa Mollah wako Muumba. Kwa hiyo (Body) Haimaanishi ni wewe, (Body) Ni guo umelivaa unaishi nalo kwa umri ulopangiwa ukifika wakati unavua na kubaki kitu chengine kabisaa, hivo ni vitu ambavyo unatumia wewe ukiwa kwenye Ulimwengu huu, unaweza kuwa na macho yako wazi pengine yanaona, au masikio labda yanasikia, na Madaktari wanasema bado Akili inafanya kazi lakini yuko wapi yule Mwenye kujua kama vitu hivyo vinafanya kazi(The Known)Mwenye kujua ndio hiyo Roho ambayo kila ukilala inarejea kwa Mollah Mlezi, Pia Napenda ufahamu kadhia hii ya kufa na kufufuliwa unafanyiwa kila siku unayoendelea kuishi hapa duniani (Sasa kwa wale wenye wasiwasi wakuamshwa kaburini inatakiwa wazingatie sana dalili hii ya kulala na kuamka) usije ukajikuta umekaa kitako kaburini wakati wenzio wote wamelala na kuna watu wanataka kukuhoji. Naam Tendo hili au mazoezi haya ya kufa unayafanya umri wako wote Mpaka ufike ule wakati wa kufa kwa (Permanent)ambayo hurudi tena kwenye uhai huu ulokua nao hivi sasa, Kwa hiyo kuanzia sasa ukenda Makaburini au Misibani elewa na wewe Ni Maiti Mtarajiwa inaweza kuwa usiku wa leo au wa kesho au baada ya miaka lakini na wewe utaonja Umauti kwa muda na nyakati ulopangiwa, hayo ndio Mazingatio unatakiwa uishi kama utakufa kesho au Ishi kama utakufa baada ya miaka 83 ili uyafanye Maisha kuwa (Balance) usiishi kwa dhuluma wala kufanya maasi bali Ishi kwa kufanya Ibada na kumkumbuka Mollah wako Mwenye kukufanyia Muujiza huu kila usiku akikuandaa na safari hii ya kurejea kwake kama alivokuleta mara ya kwanza, Kwa hiyo baada ya kuyasikia au kuyasoma haya kuanzia sasa elewa unaishi kwa (Bonus) na wakati wowote waweza kuondoka iwe usiku au mchana, ukenda mazikoni fanya tafakuri yakuona mwenzio katangulia na wewe utamfatia wakati wowote, pahala hapo sio pahala pakuleta mazungumzo ya kipuuzi au mambo ya kidunia, hapo ni karibu na Akhera na wewe unaweza kuteleza ukaanguka ukafukiwa wakati wowote, Muombee mwenzio kwa Ikhlas apate kusamehewa ukitaka na wewe uombewe siku yako ikifika, Ona Raha na Ridhia kwa kuona Mollah wako anakupa (Chance)nafasi baada ya nafasi Uendelee kuwepo duniani na kuishi ili upate kufanya Mema, Ili upate kufanya Ibada na kila siku ukenda kulala jiangalie umefanya mema mangapi na ushukuru na pale ulipokosea omba Maghfira sana upate kusamehewa kwani wewe kila ukilala unarejea kwa Mollah wako Muumba.Mollah wangu anajua zaidi 3