Saturday, March 14, 2026

KICHEKO MSIBANI

 Vipi kinatokea kifo chako wakati wa usingizi wako? Katika mambo yanokufanya uwe Hai vinatakiwa vitu vitatu, katika vitu hivyo kimoja tu  ndio muhimu sana, bila ya hicho hakuna uhai, Kitu chenyewe ni hiyo Roho ambayo ni wewe lakini hujijui, Unapolala usingizi (Body)yako inabakia, Pumzi zinaendelea ila yuko wapi Mwenye kusikia ? Yuko wapi? Mwenye kuona, Ni yupi wakati huo Mwenye ku (Experience)Nani Mwenye kupanga na kufikiri, Yuko wapi Mwenye mke na watoto wakati huo, Iko wapi mali yako ukiwa umelala , ziwapi Jeuri na kiburi, iko wapi ile kauli unanijua mimi nani?, yako wapi Mabega yako unayo nyanyua juu na kuwabeza wenzio, Yawapi majivuno yako, Jee ile mipango ulopanga unataraji kuitekeleza, vyote hivo vina (Dissappear) Kwenye Muujiza huu wa usingiza ushawahi kuzingatia tukio hili ambalo unalifanya kila ukipanda kitandani, unaweza kusema mbona naendelea kuvuta pumzi?, Utajibiwa kazi hiyo hata (Machine) Inaweza kufanya , Mtu anakua kashakufa wanasubiriwa watu wake ndio izimwe (Machine) Wanokwenda pale kumtizama wanamkuta anavuta pumzi kama kawaida kumbe ile ni (Machine) ina (Pump oxygen) lakini Mwenye hiyo (Body) yuko wapi?. Napenda uelewe hiyo (Oxygen) ni Daraja katika madaraja ya kuunganisha Mwili wako na Roho, na hii (oxygen) ya kutengeneza sio ile ya (Natural)inokuja Na kitu Maalum kitokacho kwa Mollah wako ambacho ukikijua kitu hicho kilichomo kwenye pumzi basi miezi sita kabla ya kufa kwako utajua kwamba unakaribia kuondoka kwenye Ulimwengu kurudi kwa Mollah wako Muumba. Kwa hiyo (Body) Haimaanishi ni wewe, (Body) Ni guo umelivaa unaishi nalo kwa umri ulopangiwa ukifika wakati unavua na kubaki kitu chengine kabisaa, hivo ni vitu ambavyo unatumia wewe ukiwa kwenye Ulimwengu huu, unaweza kuwa na macho yako wazi pengine yanaona, au masikio labda yanasikia, na Madaktari wanasema bado Akili inafanya kazi lakini yuko wapi yule Mwenye kujua kama vitu hivyo vinafanya kazi(The Known)Mwenye kujua ndio hiyo Roho ambayo kila ukilala inarejea kwa Mollah Mlezi, Pia Napenda ufahamu kadhia hii ya kufa na kufufuliwa unafanyiwa kila siku unayoendelea kuishi hapa duniani (Sasa kwa wale wenye wasiwasi wakuamshwa kaburini inatakiwa wazingatie sana dalili hii ya kulala na kuamka) usije ukajikuta umekaa kitako kaburini wakati wenzio wote wamelala na kuna watu wanataka kukuhoji. Naam Tendo hili au mazoezi haya ya kufa unayafanya umri wako wote Mpaka ufike ule wakati wa kufa kwa (Permanent)ambayo hurudi tena kwenye uhai huu ulokua nao hivi sasa, Kwa hiyo kuanzia sasa ukenda Makaburini au Misibani elewa na wewe Ni Maiti Mtarajiwa inaweza kuwa usiku wa leo au wa kesho au baada ya miaka lakini na wewe utaonja Umauti kwa muda na nyakati ulopangiwa, hayo ndio Mazingatio unatakiwa uishi kama utakufa kesho au Ishi kama utakufa baada ya miaka 83 ili uyafanye Maisha kuwa (Balance) usiishi kwa dhuluma wala kufanya maasi bali Ishi kwa kufanya Ibada na kumkumbuka Mollah wako Mwenye kukufanyia Muujiza huu kila usiku akikuandaa na safari hii ya kurejea kwake kama alivokuleta mara ya kwanza, Kwa hiyo baada ya kuyasikia au kuyasoma haya kuanzia sasa elewa unaishi kwa (Bonus) na wakati wowote waweza kuondoka iwe usiku au mchana, ukenda mazikoni fanya tafakuri yakuona mwenzio katangulia na wewe utamfatia wakati wowote, pahala hapo sio pahala pakuleta mazungumzo ya kipuuzi au mambo ya kidunia, hapo ni karibu na Akhera na wewe unaweza kuteleza ukaanguka ukafukiwa wakati wowote, Muombee mwenzio kwa Ikhlas  apate kusamehewa ukitaka na wewe uombewe siku yako ikifika, Ona Raha na Ridhia kwa kuona Mollah wako anakupa (Chance)nafasi baada ya nafasi Uendelee kuwepo duniani na kuishi ili upate kufanya Mema, Ili upate kufanya Ibada na kila siku ukenda kulala jiangalie umefanya mema mangapi na ushukuru na pale ulipokosea omba Maghfira sana upate kusamehewa kwani wewe kila ukilala unarejea kwa Mollah wako Muumba.Mollah wangu anajua zaidi 3

No comments:

Post a Comment