Dhanbi hiyo imetajwa ndani ya Quraan sura ya Al-Aaraf kwenye aya ya 20 mpaka aya ya 22 "Pale Shetani alipowafata (Nabii Adam a.s na Bibi Hawa)Alifanya nini Shetani ", Ukisoma kawaida utaona kawatia ushawishi wakala Tunda mara wakaona tupu zao, wakajiona wako (Uchi)Wakajifunika majani, Wao walikua wanaishi (Innocent)Mpaka Shetani alipokwenda akawavua (Guo Lao la Utiifu)Guo la Ucha Mungu, alifanya nini?, Jambo la kwanza alizungumza nao (Wakasikia)akawaambia na (Kuwaonesha)huo mti akazipata (Senses)Mbili za kusikia na kuona akawaambia kuleni ili mpate kuishi milele kwenye Raha hizi za Peponi au mpate kuwa Malaika, wakaenda kuushika na kuipata (sense) ya tatu na wakamalizia (Sense)ya Nne ya kula na kuonja ladha yake, wakakamilisha (sense)ya tano ya Harufu ndipo wakaamka kiroho (Au) niite (six sense). Kama umefahamu uzuri utajua tunda lilikua mtego wa kutizamwa Utiifu wetu au ita (Taqwa)Kwa Mollah wetu, tumeshindwa vibaya sana mpaka leo tunaendelea kushindwa, umekua mtihani mkubwa na kila Jambo ulifanyalo limefunikwa na kitu(Sex).Sasa guo lenyewe ni huo utiifu ulovikwa na Mollah wako lakini tumelivua sisi wenyewe kutoka kwenye Roho, likivuliwa guo hilo la Ucha Mungu utiifu unaondoka na wewe unahamia kwenye Akili, hapo tena unaendelea kuteseka mpaka utake Mwenyewe kulivaa tena hilo guo la utiifu hapo tena ndio linaitwa Taqwa, maana umelivaa kwa mapenzi yako ili kurudi kwa Mollah wako ukiwa Umetubu. Hiyo ndio Taqwa mwanzo ulivishwa na Mollah kwa mapenzi yake kwako na sasa unatakiwa ulivae Mwenyewe kwa ajili ya mapenzi kwa Mollah wako , huku ukijua Mollah wangu nimekuasi sana kwa umri ulonipa wa miaka 20 ama 30 au sasa nimefikia 60, ukilikumbuka tu kulivaa guo hilo basi hapo hapo ushaanza kupata (Transformation)sasa utaanza kuwapenda na kuwalisha maskini, utatunza mayatima, na vyote utakavyoruzukiwa utajua si vyako peke yako ila utatumia na wenzako, Usione naandika ukaona hiyo ni kazi Rahisi, Inatakiwa ifanyike kazi kubwa ili uweze kupigana na nafsi yako ambayo inaongozwa na Akili. Unatakiwa uwe na uwezo wa kui (control) Akili yako, ukiweza kulifanya hilo kitu cha mwanzo utajiona Mwenyewe na unatekeleza Amri zote za Mwenye enzi Mungu ukidumu katika hali hiyo kwa Mara ya mwanzo utajikuta umeanza kulivaa guo la ucha Mungu tena na unakwenda (Beyond Mind) na ukenda (Beyond) mfano wake kama umesahau Jambo, usishtuke hujapoteza Akili ila sasa (Source)Yako inakua (Direct )Kutoka kwenye Roho na wala haipitii kwenye hiyo nyumba, utakua unaona mambo (In Clarity)Utakua sasa unatumia hiyo wanoita (Six sense)Na ukianza kutumia hiyo (Sense)YA sita utajua kwa dalili hizi unaanza kuwa mkimya, hasira zinaondoka, utakua mpole, hapo tena mambo yanafunguliwa kwako na utaanza kufahamu wewe sio (Body)Nyumba yako ila ni kitu chengine tafauti, na hapo ndio utajua (You belong to know one and know one belong to you) utapata maarifa hata hii (Body)Nayo siku ya kufa naondoka naicha tunakua (separate)Kwa hiyo itakujia hekima huu Mwili nimepewa kama nyenzo ya kufanyia kheri na Ibada kwa ajili ya yule Aliyeniumba, basi ukielewa hivyo utakua umepata ufunuo huikumbatii tena dunia kwa Maasi na kula haram, kula Rushwa ,Kufanya Machafu, kujikusanyia mali , utapata uelewa umekuja na (Nothing) na utaondoka na (Nothing) ( In between) kila kitu Muachie Mungu utaona vipi unafunguliwa mambo usivotegemea ,Riziki zinakuja bila kutegemea au kutarajia na maisha yote yanakua furaha juu ya furaha Mpaka mwisho wako wa Uhai.
No comments:
Post a Comment