Friday, May 9, 2025

NYUMBA YA ROHO

 Umepewa Neema 5 mpaka kwa 6 labda nikikutajia utazinduka usingizini na kujijua wewe nani?. Sasa nakutaka ukumbuke hili, hilo jina sio wewe, wazee wamekupa ulipozaliwa ili wapate kukutambua, umepewa (Tag)ili watu wengine pia waweze kujua, kwa hiyo usije kudanganyika ukadhani wewe ni (Abdulla Au Khamis au Juma)wewe ni kitu chengine kabisa, nia yangu nakutaka ukitafute ujijue wewe nani, fanya hima ukijue kabla siku yako ya kufa ikifika siku hiyo utakua umeridhika kurejea kwa Mollah wako. Sasa wacha nikuoneshe njia labda huenda ukajiona au kujijua wewe nani?, Nakutaka uchunguze katika kadhia ya usingizini wako, baina ya kulala na kuwa macho (body machenism)inafanya tokeo la kuhamisha kutoka kwenye (Uko macho)kwenda katika hali ya( kulala)au kwa lugha ya kigeni(conscious to unconscious)ufanye uchunguzi mkubwa, inatakiwa jitihada ili wakati ule (Body)ina( Transfer from waking to sleep)jitahidi hapo mambo yanatisha lakini ukifanikiwa utabadilika kabisa, utakua mtu mwengine kabisa, utasema kumbe mimi ndio huyu hapo (Your being Reveal)hapo ndipo utakapojijua kumbe mimi ndio Roho, utajiona kama unavojiona kwenye kioo, tafauti yake kwenye kioo unaona body, baina ya usingizi na macho unajiona wewe Roho na mwili mko tafauti, hilo linawezekana usiogope fanya mazoezi hayo baada ya miezi 3 (New You) utakua mtu mwengine kabisa. Utajiuliza kwanini nikataja mambo haya?, Kwa sababu niliposema huu mwili ni (Robot)pengine wengine watakua ((upset)nimewakera kidogo, labda wanatembea mabega juu, labda mtu ana cheo au tajiri halafu ajione kumbe yeye ni jumba la (Robot)na atakapo kufa linarejea kwenye mchanga,dhumuni langu Acha kujigamba na udongo tafuta (Diamond within you)niliposema (Robot) nilikua naashiria kuwa Wewe ni (living organism) Umeumbwa na Mwenyewe aliye mtukufu mbora wa Uumbaji kakuumba na kitu (Self intelligence)kubwa ikisha akakuweka wewe kwenye Jumba hilo uishi kwa miaka 60 au zaidi kama alivokupangia. Kwenye Nyumba hiyo akakupa Neema ndani humo ukawa unazitumia bila ya kutoka kwa miaka yote unayoishi duniani, Umo kwenye Ufalme wako, kumbuka wewe ni Khalifa wewe ni (Master)Akakupa neema Tano kubwa kabisa ili ziwe mawasiliano yako wewe na (Body)yako pamoja na Ulimwengu ulo kuzunguka. Sasa neema gani umepewa katika jumba hilo?, (1)Umepewa Pua wewe ili upate harufu ya chakula kitamu, upate harufu ya manukato yalo mazuri, vyote hivyo vinatoka nje vinaingia ndani kwako. (2)Ukapewa raha ya Ulimi kuonja na kutest vyakula na vinywaji tafauti vya kila aina, (3)Ukapewa za kugusa(Feeling) na kupata raha na machungu, ikaonekana isitoshe (4)Ukapewa uzuri wa kusikia na huku kusikia elewa husikii kutumia sikio, sikio lako ni chujio tu ila kusikia ni njia nyengine kabisa ambayo hiyo na (5)Kuona ndio viko karibu zaidi na hiyo Roho yako, Kuona ni kitu Adhimu sana kilichopo karibu na Roho ili upate Ku (Experience) hii Dunia yako ambayo unaishi. Hizo ndio neema za Mwenye enzi Mungu kwako wewe Baba Mwenye Nyumba, Sasa ikiwa utafanikiwa kujijua wewe ni Roho sio kwa kuhadithiwa bali kujitambua mwenyewe kuwa mimi Naishi Kwenye Nyumba hii mvua ikinyesha hainipati, maumivu yakija yanaishia kwenye Nyumba, fikra zote hazinigusi zinaishia kwenye nyumba, hata mtu akinitukana anatukana nyumba ila sio mimi basi utajiandaa kwa mtazamo mwengine hususan ukijua au kuona Nyumba yenyewe ishaanza kuchakaa, nyumba yenyewe karibu itabomoka, msingi ushachoka magoti milingoti hii inauma au kuanza kutetemeka na sio imara tena, Maradhi ndio yanaanza kulishambulia Jumba lako ukilizingatia hilo ukajua kuwa nyumba hii ikibomoka natakiwa nirudi nilipotoka Kwa Mollah wangu aliyeniumba, swali unalotakiwa ujiulize narejea vipi kwa yule aliyeniumba ambaye amesema kila tendo ameshapitisha lilofanywa duniani lazima lilipwe, liwe la shari au kheri ni lazima ama kwa bahati mpaya yeye Mwenyewe ndio ataamua ama kwa lile la kusudi ujue lazima yafanyike malipo na hiyo ndio Hukumu iliyokatwa, kitacho kunusuru wewe ni kuzidi kwa yale yenye kheri ulowatendea wanaadamu wenzio sio kujenga majumba au kuchangia michango mikubwa mikubwa, kumbuka kinacho hesabiwa huko ni vitendo vya mbinguni vyenye kuhusu Roho. Unatakiwa wewe kama Roho ujiulize maswali haya?, wapi nimekosea , kwanini siwezi kujirekebisha, Tatizo liko wapi?, Utakumbuka niliposema Macho ndio yapo karibu na hiyo Roho, na ndio msingi wa maisha na ku (Experience)hii Dunia, ambayo ukichanganya na Akili utakuta viwili hivyo vyote ni sehemu ya hiyo Nyumba. Sasa tatizo limeanzia wapi ? , Tatizo kuna Kiumbe kiliingia kati akasema kutumia sauti ikisha akatuonesha Jambo ndio ikawa sababu yetu sote mpaka leo tumekuwa wateja(Addict) ukiangalia vizuri (Addiction) ziko za aina mbili moja hii ya nje ambayo tuinaona ya (Drugs)Na nyengine hii ya ndani ambayo hatuioni kila mmoja wetu anayo tokea tuliponjeshwa hakuna mwenye kuvuka isipokua atake Mollah wako au kwa jitihada zako utakapo kugundua wewe Roho una thamani zaidi na inakubidi uachane na uteja huu wa Maasi. Sasa ulianzia wapi uteja huu wa Ndani? Soma kwa utaratibu ili upate kujua dhanmbi hii ya kudumu imekugusa vipi wewe binafsi na jee ina epukika?

No comments:

Post a Comment