Asalaam Aleiykum
Nini Kusoma? Ushapata kujiuliza swali hili na kupata jawabu lake, basi kama bado wacha nikuchukue katika safari hii ya kushangaza ambayo inakutoa kwenye kiza kukupeleka kwenye Nuru, Safari ambayo ikiwa mwenye upeo wa kufahamu italeta Mapinduzi kwenye maisha yako. Binaadamu umeumbwa kila kitu chako kinafanya kazi kwa mwenendo wa aina mbili (Mfano)kama vile kuvuta pumzi na kuzitoa, kulala na kuamka na mengi mengine yenye kujulikana na yasojulikana. Na hili la kusoma pia lina mwenzie, na hapa leo ndio msingi wetu mzima wa darsa hii ili upate kumsaidia kila mmoja wetu apate faida na maana halisi ya kusoma.
Ikiwa utafata Muongozo huu basi utakua mwenye kufahamu kwa urahisi kila unacho fundishwa, utapata kitu kiitwacho hekima na kuyajua mambo mengi kwenye Ulimwengu huu.
Darsa hii itawasaidia wale wlioko (Ma-School)kwenye vyuo, nyumba za Ibada na kwengineko, Na kwa wale wenye kutaka kuhimili(Nyenzo)hii kwa manufaa yao wenyewe. Itabidi mnipe Ruhusa nikupeni changa moto ya kuifanyia kazi kabla ya kuendelea na ufafanuzi wetu, na changa moto ya leo ni kukuuliza hivyo ushawahi kujiuliza kwanini(Mtoto mdogo anafahamu haraka)?Na vile vile kwanini watu wazima hawazungumzi sana?. Ukipata majawabu mawili hayo wewe ushaingia katika siri ya kusoma, na kama bado, wacha sasa tuingie kwenye darsa yakusoma na moja kwa moja naazima neno kutoka katika kitabu cha (Injili-John-16-13)"(Nina mengi ya kusema kwenu nyinyi,Lakini hamuwezi kufahamu hivi sasa, Lakini yule (Spirit)Mjumbe wa ukweli atakapokuja,atakuongozeni katika Ukweli Mtupu,Kwa sababu yeye hatosema kwa matamanio ya (Nafsi) yake, lakini atakwambieni chochote atakachosikia, atakwambieni na kukupeni habari za mambo yajayo, atanitaja kwa kuninyanyua(jina langu)) atachukua yalo yangu na kukufungulieni nyinyi)".Sasa narejea kwenye Quraan nipate kuiliza nayo inasema nini kuhusu Mjumbe huyu wa kweli?, sura ya (Najm aya ya 3-4)"وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ ""Wala hasemi kwa matamanio(Ya nafsi)""Hayakua haya (anayosema)ila ni Wahyi ulofunuliwa(Kwake)".
Sasa kwanini nikataja aya mbili hizo kutoka katika vitabu viwili tafauti, kwa sababu ndio msingi mzima wa kukuonesha hiyo siri ya kusoma imetokea wapi. Sasa nataka utupie macho hilo neno la kwenye (Injili) linalosema "Lakini atakwambieni chochote atakachosikia", anasema Mtume s.a.w unapokuja huo (Wahyi)"(Nasikia kama sauti inanijaa kwenye Kichwa changu na unapomalizika hiyo (Sound)(Wahyi) tayari nakua nishasoma), Hiyo ndio maana ya (Iqraa)"Sio kwamba Mollah hakujua Mtume wake hajui kusoma kama wanavosema wengine" Bali alikua anapewa Amri ya kusikiliza hicho atakachosomewa, Na kusikiliza ndio mwenza wa kusoma, bila ya kusikiliza tabu sana kusoma, Na"Hapo kuna hiyo siri yenyewe, nayo ni hiyo kusikia" na hii kila Mwanaadamu anao uwezo huu wa kusikia, ndio utaona hata hiyo (System) ya (Wahyi) inamjia Mtume s.a.w kwa njia ya kusikia, na ndio maana na nyinyi mkaambiwa katika Quran aya ya (204)sura ya (Aaraf)"وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ"
Inaposomwa Quran isikilizeni nyamazeni ili mpate kurehemewa.
Kwanini mkaambiwa sikilizeni na Nyamazeni? Kwa Sababu (Method) hiyo hiyo inayotumika kwenye Quraan na ilosemwa kwenye (Injili) inatumika pia kwenye masomo mengine yote.
Sasa kwanini mkaambiwa sikilizeni? Endelea part 2
No comments:
Post a Comment