Asalaam Aleiykum
Ukifahamu Elimu ya Dini kwa undani utajua kuwa Dini ni msingi mzima wa maisha katika Ulimwengu huu, Bila ya Dini Mwanaadamu hana pakushika, hajui pakwenda, maisha kwake hayana umuhimu wowote na mwisho anamalizikia kupoteza (Akili).
Halafu kuna kinachofatia ni kile kilicho simamisha (Jengo) hili la Dini nayo ni hayo Matofali ya (Elimu) ya Sayansi, sasa nini wanasayansi wanafanya , kazi yao ni kuchunguza hili tofali limetengenezwa kwa kitu gani, kwa kuwa Nyumba imejengwa kwa Matofali mengi, na kila Tofali limetengenezwa kwa (Material) tafauti, wafanyacho wao Wanasayansi ni kuchambua, ambapo kwenye fani hii (Waislam) wamechangia pakubwa katika upatikanaji wa maelezo ya matofali hayo.
Viumbe tumepewa uwezo wa (Uchambuzi) ikisha tukaambiwa msije mkaringa na kuvimba kwa viburi (Hamkupewa ila Elimu chache sana). Kwa kuwa Ulimwengu huu ni mkubwa na mambo yake ni mengi yasokua na mwisho inatubidi kila kukivumbuliwa mambo mepya lazima tuyaseme, ili angalau wale walokua bado na Imani dhaifu linaweza kuwatingisha jambo kama hili na kuwashukia kitu katika nyoyo zao.
Ndio maana leo nikasema vikutanapo dini na sayansi sisi wenye matumaini ni lazima tufurahie jambo hili kwa sababu sayansi imetupa ushahidi wa kile tunachokiamini, japokua ushahidi wenyewe umepatikana kwa tabu lakini hatuna budi kuwaarifuni ili mpate uyakinifu wa jambo hili. Jambo hili limesemwa zamani na (Dini) zote lakini kwa kuwa Imani zetu ni dhaifu Mtu anasema inaweza kuwa kweli au uongo, hivyo ndivyo Imani zetu zilivyo.
Sasa matokeo kama haya ya Mkutano wa dini na sayansi kutokezea ni mara chache sana katika umuri wa mwanaadamu, wangapi wamekufa hawajawahi kuona (computer) na venginevyo, ndio maana nikasema mara chache sana, sasa hii ni nafasi kwa wale watopenda waijaze mioyo yao kwa Imani madhubuti ili ipate kuwarejesha kwa Mollah wao.
Nini Kimetokezea?
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment