Sunday, February 15, 2015

VIKUTANAPO DINI NA SAYANSI PART2

Asalaam Aleiykum

Mwanzoni mwa mwezi wa January wanasayansi wametangaza kupiga hatua japo kwa (Theory)na kutangaza kwamba kutokana na hesabu zao za uhakika sasa wanaamini kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna Mlango Mbinguni ambao ikiwa tutaweza kuufikia kuutumia basi tunaweza kupita na kutokezea kwenye Ulimwengu mwengine(Usianze kukuna Kichwa ntakupa Link, ambayo unaweza kuzisoma habari hizo).(Http//Uk.news.yahoo.com/space-time-tunnel-milk-way-161910082.
hicho kiungo utazipata habari hizo na ripoti kamili.
Dini inasema nini kuhusiana na uvumbuzi huo. Kabla ya kutaja (Milango ya Mbingu) wacha kwanza tuihudhurie aya ya (12) ya sura ya (Talaq) tuone inatwambia nini kuhusu jambo hili.
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا 
"Mwenye enzi Mungu ni Yule ambaye ameumba Mbingu saba, Na Ardhi kwa mfano wa hizo(Mbingu), Amri (zake) zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua(Kwa elimu yake)".
Kwa Mwenye kutaka kusoma au kujua au kuongeza  nguvu ya Imani yake, basi katika aya hii na habari hizo za wanasayansi kuna mazingatio makubwa kabisa yenye kukupa tamaa kwamba hicho unacho kiamini sio jambo la mzaha.
Mwenye Enzi Mungu ameumba Mbingu saba na Ardhi mfano kama huo, jamani mambo makubwa, Mtume s.a.w "Katika kisa cha (Miraji)" anasema nimetembea mimi katika mbingu zote Saba, Na nimepita katika Miji nikakuta watu wanateswa(Rejea Quraan aya ya Mwanzo sura ya Israa) iliposema na nukuu karibu ya mwisho "Ili Tumuoneshe baadhi (Tu) ya Alama zetu". Alikua yeye anatutajia mambo aloyakuta huko na kuyaona kwa macho yake katika hizo Ardhi zilizotajwa katika Quraan.
Lakini wapi wanaadamu ni wagumu kukubali au kuamini maelezo kama hayo, na wamesimama wengi katika hao wenye Imani ya Dini hii na kusema(Zilikua ndoto) za kisa cha Miraji, imekua leo hata hakizungumzwi kisa hichi kwa ajili baadhi ya kundi linaona hilo jambo haliwezekani.
Sasa Wanasayansi wanasema nini?
wasikize wanavosema kwa lugha yao(A Giant door way to another galaxy or universe may exist at the centre of the Milky way).
Quraan inasema kwenye sura ya Nabaa aya ya 19
"وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٲبً۬ا " Na Mbingu zitafunguliwa ziwe milango (Kwa) Milango.(A Wormhole in Milky way could lead to another Galaxy)(There could be a huge "Wormhole" at the centre of the Milky way).
Scientist Believe it would be possible to navigate through the wormhole.
Huku Mwenye enzi Mungu anasema Kaumba Mbingu saba na Ardhi mfano wake, Yeye ndiye aloleta hiyo dini na sayansi na anavikutanisha vitu viwili hivi ili kukuzidisha Imani wewe unaye kubali kuwa Mwenye enzi Mungu yupo na hayo yalosemwa na wajumbe wake ni kweli na wala huna shaka nayo.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment