Sunday, February 1, 2015

SIRI YA KUSOMA PART 2

Asalaam Aleiykum

Kusikiliza ndio (Mama) wa masomo nataraji mliopo kwenye madarsa na vyuoni mtachukua (siri) hii ili ikusaidieni na kupata faida kubwa kabisa.
Mwanaadamu una nyenzo mbili za ufanyaji kazi kwa kutumia Sauti, nyenzo ya kwanza ni ile ya kusema kwa kutumia sauti, Na ya pili ni ile ya kusikiliza, moja unatoa sauti na ya pili unatia sauti, unaposema au kuzungumza huwezi kusikiliza wakati mmoja, lazima unyamaze ndio uweze kusikiliza, Sasa kwanini ukaambiwa utulie unaposomewa kitu, kwa sababu (Any Movement inside) inatingisha Akili, Na Akili ikitingishwa ina mambo mengi ya mawazo. Nini Mawazo ? Mawazo ni mzungumzaji wako wa ndani, ukikosa Mtu nje unamualika rafiki yako mawazo mnaanza kuongea, unaweza kuwa nje umenyamaza kumbe ndani ya Akili yako una hutubia mkutano wa hadhara, Mwalimu anasomesha na wewe huko mawazoni unasomesha inakua hapo wewe husomi ila unashindana na Mwalimu kusomesha, na huku unabakia kusindikiza Darasa.
Kwa kuwa (University) au taasisi nyengine umelipa pesa basi hawawezi kukufelisha kwa hiyo wanakupa (cheti) Shahada ambayo haina faida yoyote huwezi kuleta maendeleo kwa sababu hujasoma,
Na kichwani umebaki mweupe. Sasa Siri yenyewe ni lazima ujifundishe kunyamaza kimya ndani ya kichwa chako kwenye Akili.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment