Asalaam Aleiykum
Binaadamu sote tuna uchu na hamu ya kujijua mimi ni nani, hivyo mimi ndio huu Mwili(Body)au kuna kitu chengine cha ziada kimejificha ndani ya Mimi ambacho sikijui, Na kama kipo Jee naweza kukijua?.
Utakaposema waweza kukijua unakua ushakipoteza zamani, lazima ujipe matumaini kuwa kinaweza kujulikana, kama inavo kufahamisha(Tawhid)siku zote uwezekano huo upo, lakini tatizo lake ni wewe unaogopa, unatishika huitaki kabisa elimu hii ya (Tawhid). Na sababu kubwa unajua elimu hii itakuonesha ukweli na siku utakapo uona ukweli, uongo wote utapotea, kwa sababu hivi sasa umo katika kuishi ndani ya uongo, umo katika kujificha unasubiri mpaka siku yako ya kufa ndio ujijue wewe nani?.
Siku ambayo itakapofika utatenganishwa na Mwili wako(Body) na kukumbuka Alaa kumbe mimi ni Roho, kumbe mimi sio mwili kama nilivokua najiona na kuringa nao, pengine utajiuliza hivyo kuna haja gani kuijua Roho yako hivi sasa? Haja iliyopo kwamba ukijijua kuwa wewe ni Roho kutabadilisha maisha yako na kuwa mtu mwengine kabisa, hutotenda dhanmbi kwa kusudi tena, na hiyo ndio khofu yako kubwa hutaki kubadilika.
Kwani Ukibadilika itabidi usithamini mali yako, dunia itakua haina umuhimu kwako, kiburi kitapeperuka kisionekane, kwa sababu ukiigundua Roho yako utakua mtupu, mweupe(Pure) hivyo ndivyo ilivyo Roho. Sasa wacha tuiweke upande Roho na tuzungumzie nguo za hiyo Roho ili tupate kukuonesha hizo Alama tano upate kuzifahamu. Kuzifahamu nguo hizo (Tawhid) inatufahamisha tusome sura ya Muuminun aya ya(12 mpaka 14).
" وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن سُلَـٰلَةٍ۬ مِّن طِينٍ۬ "
Hakika tulimuumba mwanaadamu kwa udongo ulio safi.
Asili yake ya mwanzo Mwanaadamu ni udongo msafi ambayo ndio hii ardhi, huna chengine ulicho valishwa isipokua hii Ardhi.
"ثُمَّ جَعَلۡنَـٰهُ نُطۡفَةً۬ فِى قَرَارٍ۬ مَّكِينٍ۬ "
Kisha tukamuumba kwa tone la manii(Mbegu ya Uzazi)lilowekwa katika makao yalohifadhika.
Kisha ukawekewa(System)kuwa nguo hizi kwa njia ya kuumbwa utakua unazivalia kwenye Tumbo la Mwanamke.
" ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَـٰمً۬ا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَـٰمَ لَحۡمً۬ا ثُمَّ أَنشَأۡنَـٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَـٰلِقِينَ "
Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la damu, na tukalifanya pande la damu hilo kuwa pande la nyama, kisha tukalifanya pande la nyama hilo kuwa mifupa, na mifupa Tukaivika nyama, kisha tukamfanya kiumbe mwengine, Basi Ametukuka Mwenye enzi Mungu Mbora wa waumbaji.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment