Sunday, February 8, 2015

ALAMA TANO ZA ROHO PART 2

Asalaam Aleiykum

Vipi ukafanywa kuwa kiumbe Mwengine kwa kuwa sasa "Akampulizia Roho yake"(Sajjad aya ya 9)(ثُمَّ سَوَّٮٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِۦ‌ۖ) Alipopuliziwa hiyo Roho sasa Mwanaadamu akawa na sehemu mbili moja kutoka Ardhini na nyengine kutoka kwa Allah nao ni huo Utukufu wa Roho yako ulotokea kwa Mollah wako. Kukijua kitu hicho ni haki yako kwa sababu kama hujakijua wakati huu unaishi, basi jua utakijua siku ile ya kutolewa Roho yako, Na hakuna njia nyengine ya kujijua isipokua uzame kwenye Ibada, upotee kabisa sio kitendo cha mguu ndani mguu nje.
Kazi yangu mimi hapa kukuonesha hizo Alama kuwa kitu hicho kiitwacho Roho kipo na Alama zake ni hizi zitakazo kufanya ujijue wewe nani?. Alama hizo zenye kuonesha au kuashiria kuwapo kwa Roho ni zile bila ya wewe kuwa nazo ina maana wewe huna mahusiano na haya maisha kama tuyajuavyo. Alama zenyewe ni(1)Kuona(2)Kusikia(3)Kugusa(4)Kuhisi(5)Kunusa.
Ikitokea ukapoteza Alama hizo tano hapo Madaktari wa Ulimwengu huu wanatangaza na kutia saini kwamba wewe sasa ni (Maiti) na hufai kukaa na sisi tena, utatupa maudhi, ni lazima tuchukue dongo lako tukalifukie Ardhini, kwani kile kilichokua kina mahusiano na sisi kishaondoka(Sajjad aya 11)(قُلۡ يَتَوَفَّٮٰكُم مَّلَكُ ٱلۡمَوۡتِ ٱلَّذِى وُكِّلَ بِكُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ تُرۡجَعُونَ)."Sema; Atakufisheni Malaika wa Mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa Mollah wenu.
Kwa hiyo hapo inakujulisha huo Mwili ni Koti ambalo Roho linavaa na ukikamilika muda wake linavuliwa, (Unapata Elimu ya Tawhid ya juu kabisa isije ikakujia fikra naandika kwa matamanio yangu).
Naam, hiyo ndio Roho yenye kupita kwenye Uhai na Umauti, lakini kwenye (Life) Roho inaishi milele, ili hiyo Roho ihusiane na huo Mwili(Body) Mwenye Enzi Mungu akakupa vitu hivyo vitatu kwa vitano(Sajjad 9)ili upate kuwasiliana na Uhai huu tulo nao Mollah kakupa(وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَـٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَ‌ۚ ) (Masikio)kusikia, Na (Macho)kuona, Na(Nyoyo)Kugusa,kuhisi,na kunusa.
Vipi vinafanya kazi vitu hivi?
Ndipo pale tunapata hizo Alama tano za kuwapo kwa Roho kutokana na zinavotuashiria kuwapo kwa (Mfalme) Mwenye kuutawala Mwili huu, Na huyo Mfalme yeye ndie mwenye uamuzi wote wa alitakalo kwenye Mji wake, sasa wacha tuingie kuzipekua Alama hizi tano ili zipate kutupa ishara za hicho kilojificha chenye Umiliki wa mambo yote haya ya nje na ndani. Kutokana na sifa hiyo lazima Utukufu wa kitu hichi utakurejesha kwa Mollah wako na kujijua kumbe mie Khalifa, kumbe mie nina uwezo kama huu kwanini siku zote nilikua Mtumwa natumikia Alama tano hizi, wakati kumbe hizi zipo kwa ajili ya kunitumikia mimi.
endelea part 3

No comments:

Post a Comment