Sunday, February 15, 2015

VIKUTANAPO DINI NA SAYANSI PART 3

Asalaam Aleiykum

Kwa hiyo pata uhakika kuwa Mbingu ziko Saba na Ardhi ziko Saba, Na kwamba Safari ya wewe kwenda Mbinguni ipo, na utakwenda kwenye Ulimwengu mwengine kama inavothibitisha Quraan Adh-Dhaariyat aya ya 22.
وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ 
Na Katika hiyo Mbingu kuna Riziki zenu na mliyoahidiwa.
Yaani kuhaidiwa huku ni hiyo Pepo au Moto katika huo Ulimwengu mwengine, sasa kama Imani yako inakupelekea kuwa maisha au Uhai wako unamalizikia hapa hapa Duniani basi tia shaka sana kwa jambo hilo, kwani ziko Ulimwengu nyengine na hatujui makaazi yetu yatakua wapi baada ya kuondoka kwenye Ulimwengu huu.
Wanasema wanasayansi ikiwa tunaweza kufanikiwa kupenya kwenye hiyo (Tunnel) tunaweza kutokezea kwenye Ulimwengu mwengine kabisa, Dini inasema tumeziumba hizo mbingu mnazoziona Tabaka baada ya Tabaka, hata mkifanikiwa kupenya kwenye hiyo ya pili basi kuna sita nyengine mfano wa hiyo mnoiona ambayo hamjafikia hata chembe katika uchunguzi wenu.
Na huo Mlango mnaousema kweli upo na wala hamkukosea, kuna viumbe wenzenu husogea karibu kusikiliza Amri zilizotolewa lakini huwapiga kwa (Missile)na kukimbia (Sura ya Mulk aya ya 5)
 وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَجَعَلۡنَـٰهَا رُجُومً۬ا لِّلشَّيَـٰطِينِ‌ۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ 
Kwa hakika tumeipamba Mbingu ya karibu hii kwa mataa, na Tumeyafanya ili kuwapiga mashetani, Na tumeweka tayari adhabu ya moto uwakao.
Naam hivyo ndivyo mambo yalivyo hapiti mtu kwenye hiyo Milango, wala hakuna awezaye kusikia Amri na siri za huko kwenye Ulimwengu wa Ajabu, kwenye Viumbe wengine wa Ajabu, Sasa Ikiwa Milango ishagunduliwa, jee wewe mpitaji ushajiandaa kwa safari ya huko, Na kama unasema safari ya (Miraji) ni ndoto, sasa tukuulize na Wanasayansi wanaota "Mchana" basi ikiwa habari hii imekushitua moyo wako basi nakuhimiza anza safari ya kumjua na kumtii Mollah wako ili upate furaha ya Milele, na Mapokezi yenye neema katika Ulimwengu mwengine wa Ajabu uliopo huko Juu kwenye Mbingu saba na Ardhi saba.

No comments:

Post a Comment