Sunday, February 1, 2015

SIRI YA KUSOMA PART 3

Asalaam Aleiykum

Sio ujifundishe kufunga mdomo tu bali kichwani uwe (Empty) hakuna mawazo mengine yanayopenya ila kwa lile unalofundishwa au kusomeshwa. Ukiweza Ku(Master Art) hii ya kusikiliza wewe utakua tayari Msomi, Na kila kitachofundishwa au kusomeshwa kitaingia ndani na kukaa kwa ufahamu wa hali ya juu na huko ndiko kurehemewa kulikotajwa katika (Quraan).
Kwa jinsi hiyo ndivyo kinavokaa kwa mtoto mdogo, sababu mtoto mdogo hana mawazo wala haongei kwenye Akili yake, ila yeye ana (Art) ya kusikiliza kwa makini ikiwa una uwezo wa kumuangalia mtoto mdogo mtizame anavo kusikiliza. Kwa kuwa wewe ni mtu mzima sasa ukiwa msikilizaji mzuri utaona unaanza kuzaa (Hekima) wala hujui inatokea wapi.
Ukiulizwa swali moja kwa moja unapewa na jawabu tayari ndani kwa ndani, Lakini inatakiwa kazi kubwa ifanyike kujifundisha tena kusikiliza, kazi pevu ifanyike kujifunza tena kunyamaza, lakini inawezekana ukiifanyia mazoezi ya kila siku, sasa hivi bado usikurupuke ukaanza kuona ushaweza, Jitizame mwenyewe huku unasoma, kichwani unazungumza, unapata matatizo matupu, ukimaliza (Class) unasema sijafahamu kitu, utafahamu vipi na wewe umemeza (cassete), Huku watu wanasema Maskini kajikalia kimya, kumbe wewe kichwani una mambo chungu nzima unayajadili.
Mpaka upate uwezo wa kukaa kimya nje na ndani ndipo Elimu itaingia, Hekima itakushukia, Sala yako itatimia, lakini kwanza lazima ujifunze tena kusikiliza, Iwe ndani ya akili hakiingii chochote isipokua yale unayo someshwa, lakini ikiwa Mwalimu anasomesha na wewe unamjibu na katika sauti ya ukimya basi haipatikani faida ya kusoma, kwenye sauti ya ukimya kazi yake kusikiliza na wala sio kuzungumza. Faida na siri ya kufahamu  inapatikana ndani ya ukimya wako wa nje na ndani ya Akili, na hiyo ndio siri ya kusoma kwa mwenye kuitaka.
Kumbuka siku zote Elimu inakuja kutokea nje, Ila kufahamu pekee ndio kunatokea ndani.

No comments:

Post a Comment