Asalaam Aleiykum
Naam Inapochafuka Bahari(Hamkani si shuwari tena) mashaka matupu yanatokea, hapo tena lazima Nanga ziteremshwe, ndipo hutumika njia mbili kuziteremsha nanga hizo, (Kumbuka tunaendelea na Darsa yetu ya Maradhi ya Matamanio, Tunaishi katika tendo la kuchafuka kwa maji ya Uhai).
Njia Mbili zinazopita maji hayo kwa Mwanaadamu moja ya Mwanamme inaitwa(Mahaladha) na kwa Mwanamke inaitwa(Muhuladha)hizo ndio zinazo tumika kusafirisha maji ya uhai,(Na kupita kwake ndiko kunapo kupa starehe), Maji yenye kutengeneza Binaadamu Mwenzio kiungo baada ya kiungo, Lau angejua Mwanaadamu hazina aliyobeba na matumizi yake asingekua anafanya mchezo mchezo wa kuyamwaga maji hayo bila ya utaratibu wa sheria au kwa mpango maalumu.
Sasa nini kinatokea mpaka unatokea msukosuko huu wa (Maradhi ya Matamanio) Tatizo kubwa siku zote bila ya kujijua wanaadamu tunalihusisha tendo hili na Akili wakati tendo hili halihusiani na Akili kabisa, tendo la Akili(Mind) kupenda, tendo la kuingiliana ni (Body) ndio utaona hata mnyama anayo bahati hii ya (Production) lakini Mnyama anasubiri mpaka (Body) itapohitaji ndio anatenda, lakini wanaadamu kwa kuwa (Mind) Akili ishachukua madaraka inaamrisha wakati wote (Body) kutenda kitendo ambacho lazima kitaarishwe kupitia (Process) zake, Na hayo Mataarisho ili Mwanaadamu uanze hiyo (Repaired) unahitaji masaa 48, lakini wapi, wee unajiona bingwa, unataka kutwa mara tatu na hapo ndipo yanapo anza (Maradhi haya ya Matamanio).
No comments:
Post a Comment