Sunday, January 4, 2015

DUNIANI KIPOFU NA AKHERA KIPOFU PART 3

Asalaam Aleiykum

Quraan daima inakuhimiza ufungue macho yako ungali uhai, inakwita kwa mambo mengi tafauti, lakini baada ya kukufungua macho ya Kiroho wewe unazidi kulala kwa sauti nyororo, na hiyo sio kazi yake, kazi yake ni kukuamsha, lakini kwa kuwa pengine Akili imejaa (nyimbo) ikisomwa vizuri unatingisha kichwa kwa mfano wa nyimbo, Quraan kazi yake ni kufumbua macho yalofumbwa na Akili, uone kwa uwazi na upeo wa hali ya juu, nitatoa mifano miwili mitatu ili uanze mazoezi yakufumbua macho yako ya Kiroho na hiyo ndio(sipirituality) au (Faith) Iman utakvo taka kuita, anza taratibu kidogo kidogo utaanza kuona vyengine, utapata (Change)mabadiliko mpaka kwenye Sala zako iwapo utaanza kufungua Macho ya Roho.
Inasemaje Quraan, Quraan inakwita kwa kukwambia (Na atizame)Mwanaadamu chakula chake anacho kula, sasa kwanini uambiwe utizame kwani huoni, si unaona chakula, lakini kutizama huku ni kwa njia ya Roho, Na Roho na Akili vyote viwili vikiona kwa pamoja ndio Ucha Mungu unazaliwa.
Roho inaona vipi? Umeambiwa utizame chakula na kuelezwa nani mwenye kukifanya na mfumo wake unavofanywa, kawaida utaishia hapo lakini kuna kitu cha zaidi aya inasema (Sisi) ndio wenye kukifanya, sasa nani Mwenye kuona hiyo sisi, Baina ya Kutizama kuna chakula na wewe mtazamaji, lakini kuna huyu wa tatu Mwenye kujua huyu kajificha, huyu ndio wewe, huyo ndio hilo jicho la Roho ambalo Quraan linasisitiza ufungue, uone kutumia Roho sio Akili.(فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِ)
Lakini huwezi kukubali bado umezama kwenye (Taraab)bado (Bongo Fleva)imekushika unaipenda Dunia hii imekufunga macho hujijui kabisa umo katika kukusanya mali na sherehe hizi na zile,mpaka umekua kama Kipofu kweli, na Mwenye enzi Mungu anasema katika sura ya Yaasin aya ya 9.
وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيہِمۡ سَدًّ۬ا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدًّ۬ا فَأَغۡشَيۡنَـٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ 
Na Tumejaalia(Kuweka)kizuizi mbele yao na kizuizi nyuma yao na tumewafunika(Macho yao) kwa hiyo hawaoni.
Sasa fanya hima uondoshe kizuizi, anza kuangalia kwa Roho utajua vizuizi gani vinavyokufanya usimuabudu Mollah wako, na kwanini hata ukimuabudu hupati mapenzi yake, Fungua macho yako anza kupunguza kuangalia mambo kwa kutumia Akili, soma Quraan ikupe muongozo, inasema Quraan tukaujaalia Usingizi kama kufa, tukajaalia usiku kama guo, tukajaalia mchana ni wakati wa maisha, jee umepata kuviangalia hivyo vyote kwa kutumia Roho yako, ikiwa umefanya hivyo wewe ushapata (Faith) Imani, vitu hivyo vinakupa (Mwanga) uhakika wa mambo ambayo hayana shaka ndani yake, sasa hivi Imani yako ya kushikiwa bado hujapata Ithbati, Tizama kwa kutumia Roho yako utayaona mambo hayo.
Zipo Njia nyingi za kuijua Roho yako na ukaona mambo kwa kutumia Macho ya Roho nitakupa moja mengine tafuta mwenyewe, hayana idadi, mwanzo wala mwisho, japokua mwanzo utapata tabu na kutishika lakini usiogope jambo la mwisho litotokea ni kufa, sasa unaogopa nini? kwa siku wanakufa karibu watu laki nne sasa hujioni wewe una bahati umebakia ili uyatafute mapenzi ya Mollah wako. Nini cha kufanya kutaka kuyajua kweli macho haya ya Roho yapo, Leo ukenda kulala lepe lepe la usingizi linakuja ushafumba macho ndani una uwezo wa kubakia macho, subiri kuna kipindi cha sekunde chache baina ya kulala kwako kuna vitu vinabadilika unatoka kwenye dunia ya Fahamu unakwenda kwenye dunia ya Usingizi vyote hivyo utavishuhudia mambo yatakushangaza lakini na wewe utabadilika (Forever)utakua ushaondosha (Cover) utakua huoni tena kwa kutumia macho ya Akili, utakua ushagundua siri ya (Maisha)utakigundua kile chenye kuiona ndoto wakati umelala, nje utabakia kama kawaida lakini ndani atakua anaishi Mcha Mungu, na huko ndiko Quraan inapotuita tuone ukweli wa mambo tupate ushuhuda wa mambo, tuthibitishe Imani zetu, lakini kama umeamua kuwa Kipofu hiyo ni hiyari yako, na utakapofufuliwa usije ukalalama mbona sioni kitu, wenzako wanakwambia huoni Rehma za Mungu unajibu sizioni, kwa sababu ya kuwa kipofu hapa Duniani, Fata nyayo za Wacha Mungu upate kuongoka, acha kukamata mambo ya mpito yatakupofua macho hapa na huko Akhera, shikilia vile venye kudumu upate furaha ya Milele.

No comments:

Post a Comment