Asalaam Aleiykum
Maradhi yanaanzia hapo kwa ajili ya kutumika maji haya pasi na kiasi cha makadirio ya Mwili, kisima kisha kauka wewe unaendelea kuchota, kumbuka maji haya yanapita katika hizo njia, na njia hizi zikipata mazoea ya (Raha) Mwanaadamu hana njia ya nusura, ni lazima ataangamia, atasahau dini na kila kitu kilicho mbele yake, kwa sababu hizo njia zishajenga mahusiano na Akili, inakua kama unga(Opium)na (Brain), nyote mnakua wateja lakini wa fani mbili tafauti, huyu ana raha ya kulala usingizi akajidhuru Afya yake, na wewe una Raha ya Matamanio na kudhuru Afya yako, tafauti ni wakati, mmoja anachukua muda mfupi, na mwengine anachukua muda mrefu kujidhuru.
Kutokana na njia hizo kutoa Raha muda mfupi kwa Mwanamme na muda mrefu kidogo wa sekunde kwa Mwanamke, inakua mazoea sasa lazima zipatikane Raha hizo kwa njia yoyote, kwa hiyo hapo ndio Akili inatangaza Mamlaka kamili, saa zote unatawaliwa na mawazo ya uchafu Akilini, kwa hiyo unakua huwezi kufatilia chochote inakua Filamu zako za mapenzi, ukipumzika hili mara unatia Nyimbo, nyimbo ikisha unaimba mwenyewe, ukimaliza hizo nyimbo unatoka kwenda nje kutizama, hutulii huna (Balance) ya Akili mambo yamechafuka, huwezi hata kukaa peke yako, mara umekamata gazeti, Quraan inakutisha huitaki, basi inakua Akili yako fujo tupu, inapumzika ukihesabu pesa tu, lakini vyenginevyo unazunguka kama pembea, (Jitizame sana na kuyachafua maji hayo)Hapo ndio inatokea hiyo uloambiwa hakika hii ni njia mbaya.
Njia mbaya kivipi? Kila ukiyamwaga maji hayo ya Uhai bila ya mpangilio na (Body) Mwili wako unakufa kidogo kidogo, kwa sababu gani?, sababu yenyewe (Body) inabidi itengeneze tena hayo maji, na katika kutengeneza inabidi itumike mali ghafi, inabidi (Body) yako ijitoe Muhanga, ndio maana utaona ukimaliza hiyo shughuli unalala au kuwa Tafran lakini pale utakapotumia maji haya ya Uhai pasipo na uangalizi. na hiyo ndio njia mbaya uliyoambiwa usikurubie kila maji yakiendelea kutoka na wewe unamalizika kidogo kidogo, watu wanasema mbona kazeeka ghafla kumbe maji yashakwisha (Mwilini)kwa uzinifu. Huko ndiko kupatwa na Maradhi ya matamanio(Mind) ina Maradhi yake na (Body) ina Maradhi yake ya (Biology). Mbali yale ya kuambukiza na kuzaa vizazi ambavyo vitakua havina pakushika.
Sasa ufanye nini kama ndio ushapata Maradhi haya jee Dawa ipo?
Endelea part 6
No comments:
Post a Comment