Asalaam Aleiykum
Kuona kupo aina mbili, kuna kuona kwa Macho ambako kunashirikiana na (Body) ama tuseme Akili, Halafu njia ya pili kule kuona kwa Roho, kuona huku ni (Pure) ni kuona kwa kudumu na wala hakuna shaka ndani yake. Isipokua Mja Mwenyewe utake kufunga Macho yako ya Kiroho, lakini katika sifa ya kuona huko ni haki ya kila mmoja wetu.
Lakini Wanaadamu wengi wanachagua kuyafumba Macho ya Roho moja kwa moja mpaka siku ya kufa kwao ndio Mja anashtuka kumbe mimi naona, ukifika wakati huo inakua wapi ushachelewa huna wakukushika mkono tena, Na katika Ulimwengu huu ukiamua kuyafunga Macho yako ya Kiroho basi jijue ushaangamia, ushajipa upofu wa lazima kwenye Dunia hii, Na ukiyafunga Macho ya Roho pale pale Macho ya Akili yanachukua Mamlaka ya kukuongoza, na yoyote yule Mwenye kuongozwa na Akili anakua haoni kwa sababu Akili imejaa (Memory) ndio maana siku zote unajipiga na makuta, unapapasa viwambaza kwa kujigonga kutokana na mwenendo wako wakurudia mambo yale kwa yale sababu huna macho ya kuona, Siku zote unajikuta unafanya makosa unatubu na kurejea tena, Unadhulumu na kunyanganya ikisha unarejea tena, unalewa ukiamka unajuta unalewa tena, unakwenda kwa mganga hujafanikiwa unajuta unatubu unakwenda kwa mara nyengine, umezama kwenye biashara unahangaika halafu unaona haina maana lakini hujui la kufanya unaendelea tena kutafuta mali.
Hivyo ndio Macho yako yenye kutumia Akili yanavokutuma(Full of Memory) Na kama hujazinduka ukafungua tena Macho yako ya Roho ndio Quraan inakwambia(Al-Israa-72)
وَمَن كَانَ فِى هَـٰذِهِۦۤ أَعۡمَىٰ فَهُوَ فِى ٱلۡأَخِرَةِ أَعۡمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلاً۬
"Na aliye Kipofu katika (Dunia)hii, Basi atakua Kipofu katika Akhera, Na (Huko atakua)aliye potea zaidi njia"
Watu wanaelekea peponi wewe huyo unaongoza njia kuelekea motoni kwenye mateso sababu huoni.
Sasa ufanye nini unatakiwa ujipime uelewe mimi Kipofu au naona ili wasiwasi uniondoke?, Inabidi tukuletee mifano, na mifano iko mingi kwa hiyo ukijiuliza swali hili la mimi kipofu au naona, basi ushajitilia wasiwasi, lazima unajijua unapapasa viwambaza kwa hiyo itabidi nikupe mkongojo(Fimbo) ili upate kujua Alaa kumbe mimi ni kipofu kweli, Na Mkongojo wenyewe ni huu wa kukuzindua kwamba wewe si Kipofu lakini umeamua kwa hiyari yako ku (Cheat) kudanganya kwa makusudi, umefunga macho Yallah Maskini kumbe unaona, Sasa macho haya umeanza kufunga lini? Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment