Sunday, January 4, 2015

DUNIANI KIPOFU NA AKHERA KIPOFU PART 2

Asalaam Aleiykum

Macho haya  ya Roho yameanza kufungwa kuanzia miaka Saba, kabla ya hapo ulikua unaona vizuri kila kitu kwako maajabu na hivyo ndivyo inavoona Roho (Crystal Clear)ndio maana ukaona mtoto mchanga anatizama kitu kisha anacheka, Na kwa kuwa huu Ulimwengu ni (Vast) Mkubwa maajabu hayeshi, lakini kuanzia miaka saba kila mtu katupa (takataka zake kwenye macho yako ya Kiroho)yakafumbwa na Majirani, jamaa, School, Marafiki, University, College,Tv,Games, kila ukionacho katika Ulimwengu huu ambacho umepitia shughuli yake kubwa ni kukusahaulisha kwamba wewe unayo macho mengine ya Kiroho lakini huna haja ya kujua, umejaa (Memory) tupu, wewe jiangalie utalijua hilo, hujapata hata siku moja kufungua macho ya Roho ukaangalia jee Roho inaona nini? Quraan inapiga kelele usiku na mchana lakini wapi, unaweza kuhifadhi Msahafu mzima lakini upo kwenye Akili, unasalisha watu wanaona Raha lakini wewe na wao hakuna aliyeijua hata aya moja kwa njia ya Kiroho, ndio maana utaona yule ambaye hakusoma inakua rahisi sana kwake kutumia Macho ya Roho, kuliko wewe mwenye kujinata umesoma na una mahadith mia kadhaa umehifadhi, tafauti yenu wewe una (Memory) yeye macho yake ya wazi akitajwa Mtume s.a.w machozi yanamtoka wewe unashangaa huyu naye, anajifanya anampenda sana Mtume, sio hivyo yaweza kuwa wewe umemtaja Mtume yeye kaikumbuka  hii Quraan aloachiwa na Mtume inasema nini? Na machozi yake yaweza kuwa analia kwanini hakuwepo kipindi cha Mtume s.a.w akayatumikia maneno haya kwa wakati ule, hilo ni jicho la yule mwenye kuona kwa Kutumia Roho, ita Imani au upendavyo lakini hakika huyo kama anavyo ona hapa na hukoAkhera ndivyo atakavyo ona bila ya kizuizi. Sasa Quraan inakuhimiza vipi ufungue macho?
Endelea Part 3

No comments:

Post a Comment