Sunday, January 11, 2015

MARADHI YA MATAMANIO PART 3

Asalaam Aleiykum

Kinacho Amshwa ni hayo Maji ya Uhai, iwe kwa Mwanamme au kwa Mwanamke, sasa nini habari yetu sisi wenye kucheza na maji haya ya Uhai?. Maji haya yakiguswa Mtungini yana shuruti mbili ima yatulizwe au mtu ayanywe yatoke, Hayana njia nyengine, ndipo pale utaona Maji haya yakichafuka ndani utaona Mtu nje anachanganyikiwa, Na hayo ndio Maradhi makubwa yaliyo ingia kwenye Akili zetu, kutokana na uchokozi wa maji hayo ndio wengi wamedhurika kwa (Video) za uchafu , kutokana na dhara hiyo wengine wanakamata watu kwa nguvu, kutokana na dhara hiyo wanaharibu watoto wadogo, hawa ni wagonjwa (Mental state zao) sio sawa wanatakiwa wapatiwe matibabu Akili hazijatulia kabisa.
Watu hawa wanatumia njia ya kuwa pamoja na jamii ili waonekane wako sawa, lakini tambueni kipimo cha Akili ni (very sensitive)unaweza kumkuta Mtu nje anacheka kumbe ndani analia, jamani nisaidieni lakini hasemi, kwa hiyo nini kifanyike Muandameni mkiomuona Mtu kakamatana na mwenendo huo mpaka akubali matibabu au aondoke katika Mitaa yenu, Kwani Mtu Mwenye Tabia hiyo anaharibu (Generation) nzima ya kizazi kijacho.
Naam hivyo ndio Majanga yanavotukuta ukicheza na Maji ya Uhai, ukipita ikawa wakati wote unaangalia mambo ya (Munkar) na huo ndio uchafu ulotajwa katika (Quraan) usiukaribie (Israa 32)
"وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓ‌ۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬"
Wala msikaribie zina, hakika hiyo ni  uchafu(Mkubwa)na ni njia mbaya.
Hakika huko kuchafuka kwa Akili ndio uchafu wenyewe, sio uchafu ambao unaweza kuusafisha kwa ufagio, ni uchafu uloingia kwenye Akili yako na kutawala sehemu zako mbili za (Male) na (Female),ndani mambo yamevurugika, unamtafuta mwanamke wa ndani kwenye Akili na unamtafuta wa nje kwenye Dunia, hata ukiwapata wanawake wote hutoridhika, kuridhika kwako mpaka umpate huyo wa ndani, hapo ndio unakua (Balance)lakini kama hajatulizana huyu ulomchafua ndani, hapo hakuna salama, vipi umeanza uchafuzi huu, angalia mambo yameanzia wapi.
Kila kitu unacho angalia kinapigwa picha na kupelekwa kwenye Akili kuhifadhiwa, sasa jitizame mambo mangapi machafu kwa siku tu unaona, Picha zote hizo zimo ndani na zinataka uchambuzi wako, unataka kusafisha Akili yako lakini haiwezekani uchafu mwingi, sio lazima uangalie alovaa sketi fupi, mpaka yule alovaa Buibui lilobana picha zake zimo na anaendelea kukushughulisha, unatizama nyama zinavyotingishika, Maskini alovaa kafunika mifupa tu kaachia nyama, na wewe mtazamaji umetoa (Camera) yako unachukua picha zako na hilo Buibui unakwenda kumvua baadae, unadhani nani ataokoka na mashaka hayo.
Na hivyo ndivyo machafu yafanyavyo kazi yake, kwa kuwa Maji hayo ni (Powerful) yanatawala mawazo yetu inakua kila unalofanya ni kwa ajili ya kutumikia machafu yaliyomo kwenye akili yako, Na kwa Mwanamke hali ni hiyo hiyo hakuna tafauti, Uchafu ulotiwa kwenye Mind lazima uchambuliwe (File)moja baada ya jengine, ikimalizika picha ya huyu inakuja ya mwengine, ndio maana utaona hata maji ya Uhai yakitulia unaendelea na uchambuzi kwa kuwa uchafu Akilini umekua mwingi, huna nafasi ya kuwaza jambo lengine, ukijiona una hali kama hiyo elewa hayo ni maradhi inabidi utafute dawa ya kujitibia, sababu sasa (Bacteria)wamezidi, kupona kwake sio rahisi, japo mbele za watu utajitahidi kukaza mguu, lakini kumbe ndani umeuregeza, ndio maana ukaambiwa usiukaribie uchafu huo kupona kwake sio rahisi.
Halafu sehemu ya pili ya hiyo aya ni njia mbaya , ni kitu gani hiyo njia mbaya?, Hapa itabidi nikutakeni ruhusa yenu ili nipate kukuchukua (Chumba cha Upasuaji) ili tujue inakuwaje hata ikaitwa njia Mbaya. Inaendelea part 4.

No comments:

Post a Comment