Sunday, January 11, 2015

MARADHI YA MATAMANIO PART 1

Asalaam Aleiykum

Baada ya kupokea taarifa na takwimu hususia za Matendo machafu ya (Ngono)(Sex)yalivoenea na kuikumba jamii yetu ya leo nimeona kuna haja ya umuhimu wa kuzungumzia chanzo cha Maradhi haya yaloambukizwa na kuenezwa kwenye Mwambao wetu wa (East Africa) Na kwengineko.
Sio Kificho tena kuwa Jamii inaangamia, sasa pengine kuna uwezekano Mtu kakumbwa na Maradhi haya na hajui afanye dawa gani ili apate kupona. Basi Darsa yetu ya leo tutajaribu kukupa dawa asaa unaweza kupata nafuu au kupona kabisa, Kwanini nikasema nafuu, kwa sababu Maradhi haya ni ya siku nyingi, kwa hiyo ili upone kabisa unatakiwa utumie dawa hiyo angalau kwa miezi sita mfululizo, lakini ukitaka upone kidogo kidogo ndio nikatanguliza neno nafuu kwa kuwa huwezi kuitumia hiyo dawa mfululizo ni chungu sana, inataka ustahamilivu wa hali ya juu.
Sasa kabla ya kwenda kwenye hiyo dawa ambayo itatoka mwishoni wa darsa hii kwanza wacha twende kwenye chanzo na uchambuzi wa hili jambo la (Ngono)likoje, Sababu huwezi kutibu Maradhi bila ya kujua chanzo chake.
Sasa Jambo hili limeanzia wapi kwa Mwanaadamu? Jambo la Matamanio (Sex) lina sehemu tatu, leo ntazizungumza sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ile ya (Mind) Akili (Al Imran 14 mpaka mwisho wa aya)زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ .
"Watu wamepewa huba ya kupenda Wanawake"
Hakuna kosa kiumbe unao udhaifu huo, ndio maana unaona wanawake wengi au wanaume lakini unamchagua mmoja mwenye (Macho ya duara na nyusi za kifungo) au Mwenye (Macho ya Ndege na Mashavu ya kopa)Unajua Mwenyewe ni kipi chenye kukuvutia, Na Mwanamke vile vile ana uchaguzi wake (Pengine anapenda (Baba la Miraba sita lenye nyusi za Mawimbi) au anapenda Mwembamba Mwenye pua ya Upanga.
Na Jambo la Pili ni (Physical) ni Hitimisho la tendo lenyewe(Sex) Ngono, ambalo ni (Biological). Na Jambo la tatu ni Mapenzi ambao ni moyo, Vikikutana vitatu hivi ndio linatokea tukio la (Mawadat wa Rahma) utaona kwa mpangilio wake vitatu hivi yaani (Mind)Akili ipo Juu,(Heart)Moyo upo kati na kiungo cha kutekeleza hilo tendo (Sex Organ) kipo chini kabisa.
Unapata Darsa kama hii usianze kuleta fikra zengine ila chukua chenye manufaa yenye kukuhusu ili upate kupona, usigeuze Darsa hii kuwa kama (Magazine).
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment