Asalaam Aleiykum
Naam Dawa zote mbili zipo, Ama ile ya (Mind) Akili inatakiwa uwezo wako wa kuweza kujiepusha na tabia za utazamaji na usikilizaji wako wa mambo machafu, Itabidi ubadilishe tabia yako kabisa kwa kukataa kwa nguvu zako zote kukurubia mambo machafu, ukifanikiwa kujizuia utaanza kuona kidogo kidogo unapona na Akili yako inatulia, na sababu kubwa hakuna tena (Information) za Uchafu zinazokwenda kwenye (Mind) yako.
Ama katika idara ya (Biology)kule utakapoona maji yashaanza kuchafuka au tuseme hamu imekushika, basi funga macho yako na tizama kwa ndani hamu hiyo iko wapi, ukifanya hivyo kwa utulivu wa dakika chache utaona hamu yote imekatika au kupotea, na hivyo ndivyo utavoweza kuyatunza maji ya Uhai na wala si vyenginevyo, kwani kutoka kwake ni sekunde chache na kutulia kwake vile vile ni dakika chache, wewe jaribu utalijua hilo, usifatishe kuwa nimeandika, ila fanya majaribio ndio utapata uhakika.
Sasa ikiwa utafanikiwa kutuliza (Mind) na hayo maji ya Uhai faida gani inapatikana? katika njia kuna matendo mawili kuna kwenda na kurudi, Kama ilivosema kwenye aya kuwa yanapita na kuteremka(Yakhruj)maji hayo katika njia zilotajwa, basi yakitulizwa yana njia nyengine maji haya baada ya kuteremka yanapanda, na hiyo ndio (Machenism) yake mwili wako yanapandishwa juu, sasa nini kinatokea maji haya yakipanda juu, yanafanya Ukarabati(Repaired) ya (Body) yako, na (Body) ikifanyiwa ukarabati utaona unaanza kupata utulivu(Peace of Mind)unapata (Tranquilty) unapata (Joy) ya maisha,unapata (Love)mapenzi kwenye moyo wako, na huruma zinazaliwa kwenye nafsi yako, na vyote hivyo vikikusanyika ndio (Mja unakua ushafanikiwa).(Ndio Maana mkaambiwa kwa mkato ili kujizuia na matamanio fungeni Saum).
Kwa hiyo ikiwa una nguvu zako kamilifu na una uwezo wa ku (control) maji hayo ya Uhai bila ya kutumia (Force) na kwa mafunzo ulopewa ya (Kufunga)Saum na mafahamisho haya nilokupa utagundua faida zake zisizo na mwisho. Lakini kama utaendelea kuyaachia Maji yako yamwagike ovyo ovyo bila ya kuangalia Afya yako, utakua mwenye hasara kubwa, utakua mwenye kujeruhiwa Akili yako vibaya sana, utakua huna mawazo mengine isipokua unatafuta njia za kuyatoa maji hayo, Na utakapoona una hali kama hiyo basi jijue una maradhi ya matamanio, kwa hiyo fanya haraka utibiwe ili usije ukadhurika.
No comments:
Post a Comment