Sunday, January 11, 2015

MARADHI YA MATAMANIO PART 2

Asalaam Aleiykum

Sasa nini kinatokezea ? huwezi kujua nini kinatokezea  mpaka kwanza upelekwe(Lab)ukaoneshwe hicho kinachotokea, kamata kitabu chenye elimu zote ikiwemo hii ya (Biology)alokuja nayo "Mtume s.a.w"utizame inasema nini katia tukio hili(Quraan Tariq aya ya 5-7)
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ
"Na Ajitizame Mtu Ameumbwa kwa kitu Gani"
Mwanaadamu ana uwezo mpaka wakutizama kile alichoumbiwa, inatakiwa mtazamaji ana upeo gani wa kutizama, jee anajua kama hicho alichoumbiwa ni maji ya Uhai? anajua thamani ya Maji haya, kwanini yakawemo Mwilini mwake, yana kazi gani ndani ya huo Mwili licha ya kumuwezesha kiumbe mwengine kuumbwa?.
خُلِقَ مِن مَّآءٍ۬ دَافِقٍ۬
"Ameumbwa kwa Maji yatokayo kwa kuchupa"
Yanayopita katika njia mbili tafauti kutoka kwa Mwanamme na Mwanamke.
يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآٮِٕبِ 
"Yatokayo katikati ya mifupa ya Mgongo na Kifua"
Yanatoka kwa Mwanamke kwenye mifupa ya mgongo ndio maana yanachukua muda katika utokaji wake, Na hutoka kwa Mwanamme kwa wepesi kutokana na utokaji wake ni kifuani kwenye (Kitovu) ndio maana wawili hawa Starehe zao zikawa hazilingani, kwa Jambo hilo Mwanamke anaongoza kutokana na Uti wa Mgongo ni Mfalme wa (Body) ya Mwanaadamu.
Sasa kabla kwenda (Deep)nipeni ruhusa nirudi  juu kwenye (Mind) ambako ndiko kwenye Maradhi yenyewe, Katika Ulimwengu wa leo kuna kila (Zana)nyenzo ya kuamsha Matamanio, kuanzia kwenye Nyimbo, Wanawake na Wanaume vivazi vyao, Kujipamba kila Mtu anamuamsha mwenzie alolala, Watu wanavo tizamana , halafu kubwa zaidi hi hizi (Filamu na Magazeti ya Uchi)mambo yote haya yanachangia kuamsha hisia usiku na mchana, ndio utakuta wakati wote watu mawazo yao yamo kwenye (Matamanio).
Mtu anafanya mambo bila ya kujijua anaamsha hisia za Matamanio kwa wenzake wengi wanafanya kwa makusudi na wachache wanafanya kwa bahati mbaya, Sasa nini kinachoamshwa?
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment