Sunday, December 14, 2014

NJIA YA MCHA MUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum

Kuna kitu kila Mwanaadamu anakitafuta kwa kuwa kimempotea, Kitu hichi uwe Kiongozi au Jambazi, Uwe Mkarim au Uwe Katili Mwenye kuwatesa wenzio, Uwe Tajiri Mwenye kumiminika Mapesa kitu hichi sote kimetukaa moyoni na ndio lengo letu muhimu kufanikiwa kukipata.
Watu wengi wanakitafuta kitu hiki kwa njia nyingi tafauti, Na ndio maana utaona unatafuta Utajiri ukiupata mwisho wake unaona hauna faida yoyote na Bado kuna kitu (Missing), Ukitafuta Mke aliye mzuri au Mume aliye (Handsome) ukishampata unaona bado kuna kitu (Missing), Ukipata cheo ukawa Rais au Mbunge au Waziri ukishafanikiwa unaona bado kuna kitu (Missing) sasa sababu za kukitafuta kitu hichi ni tafauti lakini lengo lililojificha ndani ya nafsi ya kila mmoja wetu ni lile lile moja la kukipata hicho kitu, na hiyo ndio (Nature) yetu hata kama utaleta sababu nyenginee.
Fanya ufanyavyo lakini hamu yako na matarijio ni kitu hicho na hakuna chengine, ndio Maana upesi ukiwa Mzee au ukiwa Mgonjwa unakua na Huzuni unaona sasa Mauti yashakaribia na wewe huna hakika kama utakipata kitu hicho au litatokea tukio lengine usilotarajia, ndio maana watu wote wakati wa kufa wanakua wenye kukata tamaa kwa sababu hawajakipata kitu hichi, sababu kwenye Ulimwengu huu ulikua umeshughulika na mambo mengine chungu nzima.
 Sasa kwanini ikawa sote tunataraji kitu hichi wakati hatukijui, Jawabu linafatia kitu hichi tunakijua lakini tumekisahau, hatukijui nini kitu hichi katika Ulimwengu huu wa Ardhini, Lakini ndani ya Nafsi zetu tunakikumbuka kitu hichi kipo ndio maana tunafanya jitihada ya kukipata tena. Kumbuka tumeumbwa kwa Nafsi moja iliyotokana na Baba yetu Adam a.s ambayo makaazi yake yalianzia Peponi, (Al-Baqarah 35)
وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ 
"Na tulisema (kumwambia) Ewe Adam kaa wewe na Mkeo katika Bustani hii (peponi), Na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu, msije kuwa miongoni mwa waliodhulumu"(nafsi zao kwa kuziacha Amri za Mwenye enzi Mungu).
Huko ndiko nafsi ilipoonja hicho kitu kinachoitwa (Bliss) au (Joy) ya Peponi na hilo pekee ndilo Walimwengu wote tunalotaraji tulipate lakini njia yake ni ngumu, na hakuna jambo la rahisi usijidanganye, masharti yake yana vishindo, sio kwa kusema tu ukadhani utaipata tunza hii, inatakiwa ufanye bidii kubwa na mapenzi ya kudumu utakapoigundua Njia hiyo ya Mcha Mungu.
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment