Sunday, December 14, 2014

NJIA YA MCHA MUNGU PART 3

Asalaam Aleiykum

Katika Njia hii Mcha Mungu katika kutufahamisha hatumii neno (haramu) ila anatumia neno(Haifai) halafu wewe mwenyewe ndio utaamua unautaka Ucha Mungu au huutaki, Kwa kuwa huo Ucha Mungu unakuja kwa njia ya Mapenzi, Na mapenzi hayalazimishwi ila inatakiwa hiyari.
Naam hichi chakula cha Pili ndio hicho kilotajwa katika hiyo aya kuwa Masikio, Macho, na Moyo vyote vitaulizwa, sasa jitizame unakula nini kupitia vitu hivyo?, hakuna mengine ila unakula wewe kwa kusikiliza Maasi yote kutwa nzima, Uongo na Matusi, nyimbo vyote vinakwenda kufanya makaazi kwenye Moyo wako, mpaka unakua vitu hivyo (Automatic) katika mazuungumzo yako, jitizame ukiulizwa japo saa, mtu anakuuliza saa ngapi basi ikiwa tano na dakika tatu, utamwambia na dakika saba, ukimgomba mtoto lazima tusi japo jepesi litakutoka, basi elewa mambo hayo yanaishi moyoni, Yanafanyiwa (Process) moyoni, hiyo ndio huduma ya kwanza kwa kile chakula unachokula, nini kinafanyika ? Matusi na Music kazi yake kubwa ikipita katika Moyo ni kwenda kusimamisha Mshipa wa Matamanio, Ndio maana (Music) au Nyimbo ikipigwa unatingishika sababu ishajenga jukwaa moyoni.
Kuna kitu ndani ya Nafsi yako kina nyanyuka kama Nyoka (Cobra) anavyonyanyuka akipigiwa firimbi, Lakini hili la (Music) wewe hulioni, tafauti yako na (Cobra) inakua hasikii  lakini anaona, wewe huoni ila unasikia, Na (Energy) hii ikishanyanyuliwa si Rahisi kupanda juu tena inateremka bondeni ndio maana mawazo mabaya mabaya yanakujia, upo kwenye Sala umerukuu unasoma sura ya (Fatiha), hivyo ndio athari za kusikiliza (Music), Ndio maana utaona kwenye (Dance) watu wanakatika viuno kuashiria kuwa sasa Furaha ya matamanio ishashuka kiunoni, Nyimbo iko kichwani na matamanio yashateremka kiuononi sasa lete mdundo tukimaliza tukakate matamanio.
Na hapo kama wapo wenye kushuhudia, Macho yanakula mpaka kuvimbiwa, Balaa tupu, hii anacheza vile, duuh sauti ile inakuaje lazima nimfatilie, Balaa kubwa wakati ule, muda ukiwa huyaoni yale basi unaamua ukaangalie TV ili uendelee kula kila aina ya maasi, Macho yanakula kila Maasi, Watu wanatembea Utupu, na ghasia zote za (Advertisement) na ikisha ukenda kulala huna usingizi ila moyo unakaa kwenye shift, unaanza kuchambua kwa njia ya ndoto kipi nitapike, kiporo gani nikale kesho, ikisha huyo ukiamka asubuhi unaanza tena, na kama hutizami unakula japo kwa kugusa lakini mwenyewe hujitambui unapeana mikono na wanawake na hivi na vile huku unaendelea kula kwa njia ya matamanio.
Kwa njia hiyo ndivyo tunavyo shiba chakula cha Dhanmbi, Na kwa hilo tutakwenda kuulizwa kwanini hamjafata njia ya Ucha Mungu.
Ipi Njia Hiyo?
Njia yenyewe ni Rahisi sana na pia ni vigumu sana lakini ukiamua unaweza kufanikiwa, ufanye nini ? anza kidogo kidogo kupunguza kusikiliza maasi, nyimbo, matusi, uongo, punguza kutizama mambo ya maasi na kusoma mambo mambo ya habari za kipuuzi, kidogo kidogo ukifanikiwa kuyapunguza mambo hayo utaona Muangaza unaanza kutokea kwenye Moyo, (Torch) ya Ucha Mungu inaanza kukuonesha njia, ni kama chumba chenye kiza ukaleta (Kibatari) au (Taa) na huo muangaza ni kuacha hayo matendo niliyoyataja hapo juu, na siku utakapo pata Muangaza ukawa (Full) katika chumba chako cha moyo, hapo utakua tayari huna wasiwasi unaweza kutizama TV lakini Moyoni kuna (adhkari ya Mollah wako)unaweza kukaa na watu wanatukana lakini matusi yao hayaingii moyoni mwako, unaweza kusikiliza nyimbo lakini hazifiki moyoni mwako zinapita kama sauti nyengine tu, sasa hivi si unasikia ndege, treni, gari lakini yote hayo hayaingii moyoni mwako na siku utakayopata (Taa) ya Ucha Mungu utakua na hali kama hiyo, hapo tena utabadilika utakua hukai katika mambo hayo, hutizami mambo hayo, husikilizi mambo hayo, lakini huyaogopi kwa sababu hayakai moyoni mwako, hayana nafasi tena ya kukutawala, ila wewe umeyatawala, na huo ndio Ukhalifa, huo ndio Ucha Mungu. Tunamuomba Mollah atujaalie kutufiksha katika njia hiyo.


No comments:

Post a Comment