Asalaam Aleiykum
Tunaendelea kutafuta kuifahamu japo kwa uchache elimu hii ya kuruka, na hakuna chengine kitotupa taarifa ya jambo hili ila tumuulize Mfalme wa (Mysticism) Nabii Suleiman a.s yeye alipewa nini? Quraan Sura ya (Saba aya ya 12)
وَلِسُلَيۡمَـٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَہۡرٌ۬ وَرَوَاحُهَا شَہۡرٌ۬ۖ وَأَسَلۡنَا لَهُ ۥ عَيۡنَ ٱلۡقِطۡرِۖ وَمِنَ ٱلۡجِنِّ مَن يَعۡمَلُ بَيۡنَ يَدَيۡهِ بِإِذۡنِ رَبِّهِۖۦ وَمَن يَزِغۡ مِنۡہُمۡ عَنۡ أَمۡرِنَا نُذِقۡهُ مِنۡ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ
"Na Kwa Suleiman(Tulimpa amri ya elimu ya)Upepo(Uliokwenda)Safari yake ya asubuhi(Kasi yake ni mwendo)wa mwezi mmoja, Na Safari yake ya jioni(Kasi yake ni mwendo wa)mwezi mmoja, Na tukamyayushia chem chem ya Shaba, Na katika Majini(Kulikuwapo)waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mwenye Enzi Mungu wake, Na kila anyejitenga(Akataka kutoroka)na amri yetu miongoni mwao tunamuonjesha adhabu ya moto uwakao."
Hivi ndivo tunavyojulishwa na Quraan kuwa jambo hilo lipo na linawezekana na wapo mpaka leo wanopewa taaluma hiyo adhimu ya kuweza (Kupaa angani), Walipewa pia Baadhi ya majini na Binaadamu katika zama hizo elimu tafauti kama tutakavo soma tukiendelea kuzichambua elimu hizi za Ajabu.
Sasa wacha tuiangalie Elimu hii ya kuruka au kupaa kama ndege ikoje, kwanza itatubidi tujiulize kwanini ukatajwa upepo? jee habari hizi zinatujulisha ndege za zama hizo? jee (Technology)hiyo bado ipo, Jawabu naam elimu hii bado ipo japo walo nayo kwa zama hizi wachache sana.
Nini Upepo? Upepo ni (Transport system)ya Ardhi yetu hii, Upepo kwa njia ya Rehma za Mwenye enzi Mungu ndio wenye kusafirisha maji kwa njia ya mawingu yakatolewa sehemu moja kupelekwa sehemu nyengine(Mvua) Upepo unasafirisha Mimea, upepo ndio tegemeo la vyombo vyote vya usafiri wa nchi kavu, majini na angani, hivyo vyote vinategemea upepo kwa njia tafauti kuweza kutekeleza kazi zake.
Na hizi Pepo zipo tafauti zipo za Misimu ya (Local, National, na Inaternational)zipo zinazoletwa kwa ghafla na zipo zinazodumu katika njia zake daima, zipo pepo hii za masafa marefu na masafa mafupi, zipo za juu sana na katikati pia na chini kabisa ambazo vyombo vyetu vya usafiri kama Jahazi ndivyo vinautegemea baada ya kubeba Marobota ya katani, na vyuma na saruji ikisha wakafunga kipande cha kitambaa hao kuelekea Mombasa kwa kutegemea upepo ambao hawana Amri nao wala kuwa na ujuzi nao sasa nini habari yako wewe kama utapata Elimu hii ya upepo na nini cha kufanya?.
Endelea Part 5
No comments:
Post a Comment