Sunday, December 14, 2014

NJIA YA MCHA MUNGU PART 2

Asalaam Aleiykum

Kwa hali tulo nayo sasa hivi sote tumo katika kiza, kila Mtu anapapasa vipi ataiona njia hii, Tunapigana vikumbo Misikitini lakini ni wachache wenye kuigundua njia hii, toa sadaka, jenga visima, jenga misikiti yote hayo ni bure unafanya (Business) ya kuipata njia hii kwa (Cheap)Elewa kitu hichi hakinunuliwi na pesa abadan, kinanunuliwa kwa nafsi yako na wala sivengine, kama huna Ucha Mungu wewe Muflis, na haipatikani ila mpaka uigundue njia hii ikisha Udumu nayo, Na wengi wanaigundua njia hii lakini kila mara inawapotea.
Kwanini Unapotea ? Kutaka kujua kwanini unapotea ndio Darsa yetu inatuchukua katika safari muhimu ili upate kujua (Drugs) au vile vishawishi vinavyo tupoteza na kama unaweza kuviacha basi basi hayo ni mafanikio yako, hata siku ya kufa kwako utakua ni mwenye furaha badala ya huzuni. Jambo hili ni vigumu sana na pia ni Rahisi sana, kati yake kunakaa maamuzi yako ya kuutaka Ucha Mungu.
Jee Unataka kubakia kwenye njia hiyo, Wewe unataka zawadi Maalumu ya Mollah wako ya (Bliss) idumu na wewe milele, basi ikiwa unalitaka hilo kwanza itabidi tujitizame sisi Binaadamu Umbile letu likoje?, Halafu tuanze na kazi ya Mataarisho ya kwenda kwenye njia ya Ucha Mungu.
Mwanaadamu umetokana na Ardhi, Na kila kitu chako ulichoumbiwa kinaitegemea hiyo hiyo Ardhi ili upate kuishi kwenye Ulimwengu huu,  Na ukiangalia (System) yako yote Mwanaadamu ina mwenendo wa kula kama tutavyoona katika uchambuzi wetu, Unaona vipi ukila ukashiba hali yako inavokua namna gani, Unapumzika unataka kulala, na mambo mengine ya matamanio ya Kilimwengu, hicho ndio chakula cha kukuweka hai, halafu kuna chakula chengine chenye kukufanya kuishi.
Napenda Uwelewe kuwa Hai na Kuishi ni mambo mawili tafauti, (Mfano)Mgonjwa yuko kwenye (Coma) yuko Hai lakini Haishi, kwa hiyo kuishi kunategemea matendo, Na hayo matendo ndio hicho chakula cha Pili, Tahadhari sana katika hicho chakula cha pili unakula nini?(Banii Israel 36)
"وَلَا تَقۡفُ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌ‌ۚ إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولاً۬ "
Wala usifate usiyo na Elimu nayo, Hakika Masikio na Macho na Moyo hivyo vyote vitaulizwa.
Sasa Jitizame unaifata wewe njia ya Ucha Mungu kwa matendo?, Au unafata yale usokua na Elimu nayo(Unapinga Amri za Mwenye Enzi Mungu) yepi hayo unayoyafata wewe?, Sasa unapata dawa kama hii usiitupe  japo chungu imeze itakuponesha ni (Gurantee)n hakuna alomeza kidonge hiki akawa asipone.
Tafauti yako Wewe na Mcha Mungu ni ndogo sana, ni kama hivi yeye anajua, wewe hujui, Yeye anayo (Torch) Wewe huna unapita kujipiga na makuta huoni kitu, Yeye ana Elimu yenye manufaa  wewe unafata Elimu isiyo na manufaa, Na ukifata Elimu isiyokua na manufaa inakupoteza ima iwe kwenye Dini au Dunia unakua (Split Mind) kama kwenye Dini unaamua kupiga marufuku vitu vyote unasema (Haram) na kama umezama kwenye Dunia vitu vyote unaona Halali unakua huna elimu ya kuvitenganisha, sababu elimu zote unofata ni za kusikia, labda umesikia fulani kasema hivi, au umehadithiwa, Sasa katika Njia hii ya Mwenye Enzi Mungu unatakiwa umfate kwa Makini Mcha Mungu yeye yuko mbele wewe uko nyuma ili upate kuweka Alama pale utakapobakia peke yako ujue wapi pakupita na wapi pakuepuka.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment