Sunday, December 7, 2014

ELIMU ZA AJABU PART 5

Asalaam Aleiykum

Halafu kuna upepo mwengine ambao mmeugundua karne hii tulonayo labda miaka 40 na ushei ambao upo takriban ya masafa ni kama (Mile) Saba kwa juu, mkauita (Jet Stream)ambao unaizunguka dunia ambapo hata hizi ndege zirukazo zinautegemea katika kuruka nk, Kwa hiyo wakati wa Nabii Suleiman a.s na yeye alipata Elimu ya kufahamishwa (Mystic Stream)na mpaka leo wapo wenye kuigundua Elimu hii ya Kuruka ama kwa kuitafuta au kwa bahati unakumbana nayo, kwa hiyo zile hadithi ulokua unasikia Walii fulani kaachwa Mangapwani au Bagamoyo mkamkuta kafika mjini mwanzo bila ya gari usije ukashangaa.
Nini Kinatokea huyo katumia Elimu yake ya siri ya kupaa hewani, na safari hii ni nzuri hata kupita hizi safari za ndege au hiyo gari unayopanda. Na kwanini isiwe hivyo wakati wale wanoishi nchi za Ulaya wanajua kuwa Mtu anatengeneza (Kishada) au (Kite) au (Hang Glider) akenda kwenye Kilima au kichuguu na kujifunga mgongoni au kwenye mabega na kujiachia akacheza angani kwa masaa huku akipunga mkono, Kwa hiyo Elimu ya Kuruka ipo inatakiwa utekeleze masharti yake ili uweze kuimiliki, na ntalisema hili sharti moja na kuyaacha mengine ili watu wasije wakadhurika, Sharti lenyewe kwanza lazima umiliki elimu ya (Levitation) katika Ulimwengu huu zipo Elimu mbili moja inayotuweka kwenye Ardhi ambayo ni (Gravitation) na hii ya pili ni hiyo (Levitation) ya kupaa ukiweza kunyanyuka ukaugundua Upepo wa (Mystic Jet stream) na wewe utakua unafanya safari zako bila ya wasiwasi, lakini kikwazo chenyewe huwezi kupata elimu ya (Levitation) mpaka uipate elimu ya kupotea, ndani ya elimu hiyo ndio wanaishi Majini kama inavotaja aya ya 27 sura ya (Al-Aaraf)mpaka inapoishia.
إِنَّهُ ۥ يَرَٮٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُ ۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَہُمۡ‌ۗ
"Hakika yeye(Ibilis) pamoja na Kabila yake wanakuoneni, na hali ya kuwa(Nyinyi) hamuwaoni".
Hiyo ndio Elimu ya Ulimwengu wa majini wanaishi ndani yake kwa kutoonekana, hiyo ndio elimu ya kupotea, ipo kama vile mithili ya moto mwanzo unakua haupo na mara unauwasha unatokezea, ikisha ukiuzima unapotea sasa jiulize mwanzo ulikua wapi? na sasa umekwenda wapi?, ukijua jawabu lake basi utakua ushaanza kuipata elimu hii ya kupaa, ndio maana ukaambiwa Majini kwao Rahisi kuruka kwa kuwa wameumbwa kwa Moto Baridi, na wewe potea ukakutane na moto baridi ukoje? Potea ukakutane na elimu hii ya (Levitation), itakua Rahisi kuanza kusafiri kama wafanyavyo Mawalii (Mystic) na baadhi ya wengine wenye kutumia elimu hizi kwa ufisadi.
Endelea part 6

No comments:

Post a Comment