Asalaam Aleiykum
Tunaendelea kupata habari hizi za elimu ya kuruka na napenda kukumbusha uelewe safari hii inafanyika nyakati za usiku, kwa kuwa ndio wakati muafaka wa kuingia katika (zone) ya (Levitation).
Ama kuhusu Elimu ya kupotea hii ni vigumu kufahamika kutokana na uhusiano wake wa karibu na Sayansi ya zama hizi, kama umeshawahi kusikia Sayansi ya (Time Travel)ambayo inazungumzwa na Wanasayansi wa kileo basi hiyo ndio elimu ya kupotea, ambayo wanasayansi wa kisasa wameigundua inawezekana lakini bado hawajajua inafanyika vipi, Na ndiyo ilotumika wakati wa Nabii Suleiman a.s kama ilivyotajwa katika Quraan sura ya (Naml) aya ya 38 mpaka 40,
قَالَ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَؤُاْ أَيُّكُمۡ يَأۡتِينِى بِعَرۡشِہَا قَبۡلَ أَن يَأۡتُونِى مُسۡلِمِينَ
(Nabii Suleiman a.s akawakusanya wazee wa Baraza lake la Hekima)"akasema Enyi Wakuu ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha kusilimu.
قَالَ عِفۡرِيتٌ۬ مِّنَ ٱلۡجِنِّ أَنَا۟ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَۖ وَإِنِّى عَلَيۡهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌ۬
Mjasiri(Ifrit) mmoja wa Majini akasema"Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo(Ulipokaa) na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni Muaminifu.
قَالَ ٱلَّذِى عِندَهُ ۥ عِلۡمٌ۬ مِّنَ ٱلۡكِتَـٰبِ أَنَا۟ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن يَرۡتَدَّ إِلَيۡكَ طَرۡفُكَۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسۡتَقِرًّا عِندَهُ ۥ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضۡلِ رَبِّى لِيَبۡلُوَنِىٓ ءَأَشۡكُرُ أَمۡ أَكۡفُرُۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّى غَنِىٌّ۬ كَرِيمٌ۬
Akasema Yule aliyekuwa na (Elimu) Ya kitabu, Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako(Kufumba na kufumbua) Basi alipokiona kimewekwa mbele yake alinena, Haya ni kwa fadhila za Mollah wangu, ili anijaribu nitashukuru au (nitakuwa mwizi wa Fadhila)Kukufuru, Na anaye shukuru, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake, na anayekufuru, kwa hakika Mollah wangu ni Mkwasi na Karimu.
Hiyo ndio Elimu ya Kitabu, elimu ya kuukunja (Wakati na Sehemu)(Appear and Dis-Appear) sio Mazingaombwe(Uchawi) Mnahadithiwa habari hizi za Mawalii(Mystic) mlokua mkisikia wanatiwa Gerezani lakini Usiku wanalala nyumbani, sala ya Alfajiri anasali msikitini halafu huyo anarejea (Mahabusu). Na Ukiipata Elimu hii ndio ushapata elimu ya kuonana na Majini na mambo mengine ya Ajabu, Unaweza sasa kuingia na kutoka Ughaibuni bila ya Mtu kujua, unaweza hata kumsoma Mtu Akili nini anawaza, Ametukuka Mwenye Enzi Mungu Mwenye kutukirimu elimu hizi za Ajabu.
Ama kuhusu Elimu ya kutibu wengine wanadhani huyo anataka kutibu Malaria akiwa mbali, kusudio langu ni kuzungumzia Elimu yenye kutibu tafrani hususan zenye kuhusiana na dhiki za Moyo na Akili, Na hili ni tendo ambalo wanaweza kufanya wale walopewa Hijaza na Mollah wao hata wakiwa mbali kwa kutumia sauti zao wakaponesha baadhi ya maradhi na kuondosha misukosuko ya dhiki za Moyo, ni jambo linalowezekana, kwanini lisiwezekane wakati unaweza kumsikia mtu kwenye simu aliyeko mbali bila ya waya kukamatana, na kama akikwambia nyumba yako imeungua unaanza kutokwa na machozi, na akikwambia nakulipa deni lako unajawa na furaha, nini kinatokezea? kinachotokezea hapo ndicho kile kile(Chenye kutokezea kwenye Dua), Na yule mwenye kujua kuponesha akajua kuitumia (Universal Mind)Ambayo hii tutaizungumza siku za mbele kwenye (Majaaliwa) basi anaweza kukutibu hata akiwa mbali, kwani maradhi ni yale yale anayotibu aliye karibu, au anayeomba aliyekaribu yote yanategemeana na mfumo wa (Dua) ndio maana wengine wanarekodiwa (CD) na kutibiwa, ni jambo linalowezekana na wala halina (Mushkeli wowote).
Ama kuhusu Elimu ya Kungara hii sitokwenda ndani sana kutokana vielelezo vyake ni virefu, lakini nitasema kwa kifupi Elimu hii inategemea vipi utaweza (kujikurubisha) au kuji(Tune) na mionzi ya Jua, na ukiweza kupata taaluma hii na wewe utakua unangara kama (Taa) na ukiwa mwanasiasa au Mtu wa kupenda vyeo hapo tena chaguzi zote unashinda wewe, na kila atokua karibu yako atakua mwenye kuvutiwa na wewe, lakini elimu hii ina kasoro zake na mbili katika kasoro hizo (Watu watakuwa wanavutiwa na wewe kimatamanio) Na kama huwezi kujizuia utakua na wapenzi hata elfu, na kasoro ya pili utakua katika hali ya umoto baridi (Mithili ya Majini), kwa hiyo utakua unaishi katika Ulimengu wa (Hasira) nyakati zote kwa kuwa sio (Nature yako).
Ama hii Elimu ya kutisha ni kama hiyo ya kungara ila hii imeambatana na (usiku) Giza, si unaona kila mtu anaogopa giza, ukiweza kuambatana ukaingia ndani ya (Dark matter)ukauingia usiku ukakuvaa, basi utakua unatisha mpaka watoto wako wakikuona watakukimbia, lakini ukifunikwa na mionzi ya giza tahadhari kwani utakumbwa na uvivu usiweze hata kunyanyuka kitandani, sababu kiza kinaletewa watu kupumzika na wewe unakitumia wakati wa mchana, kiza kishaondoka wewe umebaki na kivuli chake unatishia watu, hizo ni baadhi ya elimu za ajabu ambazo ziko nyingi, Na kama inavosema aya ikiwa utazitumia kwa manufaa ya uzuri basi ni fadhila kubwa kutoka kwa Mollah wako, lakini ukizitumia kwa ufisadi basi utakua umeangamia na kukufuru kukubwa, kwa sababu utakua unazitumia kinyume cha sheria.
Haya ni kwa ajili ya kukujulisheni uwapo wa Elimu hizi lakini cha muhimu zaidi ni kumuabudu Mollah wako na umuachie Mwenyewe ikiwa Kakupa Elimu hizi basi zitumie kwa manufaa na ukinyimwa basi shukuru wala usihangaike sababu utakua unanusuriwa na mengi. "Na wala hatukukupeni Elimu zetu isipoua kwa Uchache tu".
No comments:
Post a Comment