Asalaam Aleiykum
Leo napenda kukuchukua kwenye Safari ya Elimu za Ajabu, Lakini Safari hii watakwenda wale wenye kupenda kuyajua mambo mepya, wale wasochoka na kupata habari zilofichika, na zaidi ni wale Dini yao haijaishia kwenye kutia (Udhu) peke yake, Roho daima ina uchu wa kutaka kujua mambo ndio maana wakati mwingi tunatumia katika viwanja vya kutafuta habari, Sasa ukija kwangu mimi daima utapata mambo mepya kwani naelewa Elimu za Mwenye Enzi Mungu hazina mwisho wala upeo, Bahari yake haina Kipimo kila ukizama unaendelea chini wala hufiki Mwisho kwa kuwa mwisho wake ndio mwanzo wake, Kwa hiyo sisi hatujui mwanzo wake, vipi leo tutajua mwisho wake.
Najua Wengine Darsa zangu zinawakera wanakimbia ikisha wanarudi tena kuchungulia safari hii kaleta nini, hiyo ni kazi yangu ninayoifanya kwa siri juu yako ili upate mabadiliko, na ukiona umerudi tena kuchungulia ina maana ushaanza kupata Muongozo fulani ambao unakufanya uchungulie tena, hiyo ni ishara nzuri endelea utapata mafanikio makubwa.
Sasa leo pata faida ya Safari wanayokwenda (Mystic). Nini (Mystic)?.
Nimekuja kufahamu kwamba (Mystic)ni Mwanasayansi wa Dini, Mnao wanasayansi wenu wa Dunia, Na sisi tuna hawa wetu wa Dini, Tafauti yao hawa wa Dunia wanachambua kwa njia ya nje mpaka mara inatokezea tu kwenye (Akili)zao wakapata hii ni (DNA)Nikisema inatokezea nina maana wanafunguliwa na Mwenye enzi Mungu hiyo elimu ya kujua.
Na Wanasayansi wa Dini wao Wanakwenda Ndani Wanataka kujua hiyo (DNA)imetokea wapi, Nani aloileta kwa hiyo kwa kutaka kuyajua hayo ndio lazima Mwanasayansi wa Dini achupe katika kiza kinene, kwani nje kuna muangaza lakini ndani kuna Giza zito lazima ulipite giza hilo ndio utokeze kwenye Muangaza wa Elimu za Ajabu, ndio maana kuwa Mwanasayansi wa Dunia ni rahisi lakini kuelekea Uwanasayansi wa Dini ni kazi nzito ambayo mashujaa peke wanoweza kuchupa, wengine wanafanikiwa na wengine wanadhurika wakawa waharibifu na hata kufikia kupoteza Akili kwa mambo makubwa wanayokutana nayo huko kwenye hii (Mystical Journey).
Ndani ya Safari hii ndio unakutana na hizo Elimu za Ajabu, Kama Elimu ya Kuruka(Ukapaa kama ndege)
Elimu ya Kupotea(Mara ukawa huonekani)
Elimu ya Kutibu ukiwa Mbali.
Elimu ya kuona Viumbe wengine.
Elimu ya Kutisha Viumbe wakakuogopa.
Elimu ya Kungara ukawa unapendwa na halaiki ya watu.
Na Elimu chungu nzima ambazo hazina idadi maalum ambazo katika safari hii kila ukigundua zinazidi kuongezeka na hapo ndio Kiumbe kwa papara za kutaka yote anarudi Safari hii pengine kaambulia kupata elimu moja tu katika maajabu hayo, Napenda uelewe Safari hiyo ni ndefu na inataka mataarisho makubwa, kuzidi kuyachambua haya mambo endelea part 2
No comments:
Post a Comment