Sunday, November 16, 2014

URADI WA DHIKR YA (KUMTAJA MOLLAH) PART 2

Asalaam Aleiykum

Siri yenyewe yule Bwana alikua hajui kuandika ila yeye anajua kusoma, basi na wewe nenda kajifundishe elimu zote, elimu ni bahari ambazo kwenye Ulimwengu huu zipo tano,(Indian ocean, Pacific, Nk)kwa hiyo koga zote ili tukija kukuuliza usitwambie Mguu unakuuma, Na mwisho Usije kumlaumu(Doctor) wa Miwani kwa kuwa kakwambia ukipima miwani utaweza kusoma na kuandika, jilaumu mwenyewe kwanini hukujifunza kusoma na kuandika, ukimaliza hapo na wewe utakua na Mamlaka ya kusema (Dhikiri Haifai).
Sasa Tunaanza Darsa yetu kwa kujiuliza nini (Dhikiri)?ya kumtaja Mollah.
Wacha nikupe Dawa hii ambayo yaweza kukuponesha maradhi mengi na kukufanya Mja mwenye Afya nzuri kabisa, Kama nilivyosema mwanzoni Dhikiri zipo za aina mbili zenye kuashiria kitu kimoja, ile ya aina ya kwanza wewe imekushinda, ile ya kumkumbuka Mollah wako kwa kuona Nyota na Mwezi, kwa kuangalia Jua na Mbingu, kwa Kutizama Miti na Wanyama hayo yote haya kukumbushi Mollah wako, Na unaijua Sababu kubwa mpaka yakajiri hayo?. Sababu Kichwa kimejaa(Gossip)Kichwa kimejaa Siasa na Biashara, kichwa kina mambo mengi (Cinema)zimo humo, Utajiri umo humo, Umaskini umo humo, hasira na magonvi yote yamejaa kwenye kichwa hicho, wanawake na wanaume wote umewarekodi wewe, kila kitu Mja wewe unakihifadhi katika kichwa hicho, vipi leo unaweza kuwa na nafasi ya kumkumbuka Mollah wako.
Ukijiangalia Mja wewe kila baada ya sekunde chache Fikra za kila aina zinakujia kichwani humo, mara mipira mara madeni, mara nyimbo na mikasa ya kila aina, na kwa hali hiyo hakuna kabisa nafasi ya kumkumbuka Mollah wako.
Sasa nini Kifanyike?
Ndio Wale walotangulia wenye Hekima wakatafuta njia nyengine ya kumkumbuka Mollah wao kwa kuhama kutoka Juu kwenye Akili na kushuka chini kwenye Moyo. Na kwenye Moyo hakuna lugha nyengine inayofahamika isipokua utajo wa Mollah wako, huo ndio (Uradi), hiyo ndio dawa pekee ambayo ntakupa utumie kutwa mara zote. Sio ule Uradi wenu mnosoma wiki mara moja ile ni dua Uradi ni huu wa kudumisha kwa njia ya kurejea utajo wa Mollah wako, chukua dawa hii ya kumsabahi Mollah wako kwa majina yake yote 99.
Mimi nimekuchagulia hili la (Laa illah illah Allah)lidumishe ndani yake kuna siri kubwa, kuna mambo makubwa. Endelea part 3

No comments:

Post a Comment