Asalaam Aleiykum
Siku moja Mcha Mungu Hadad alisisitiza katika maombi yake kwa Mungu aoneshwe kwenye usingizi wake nani Mcha Mungu zaidi katika Mji wake, "Akajibiwa kwenye usingizi ni Jirani yako" akafurahi sana kujua kumbe Jirani yake ndio kamshinda kwa Ibada na mapenzi ya Allah, Akaomba tena sasa naomba nijulishwe yule Mtenda Dhanmbi kubwa kuliko wote ili nipate kumjua, "Akajibiwa tena ndani ya Usingizi wake ni Jirani yako" Mambo haya yalimshangaza sana Hadad akawa hajui la kufanya, kwa sababu Ucha Mungu anauona kwa yule Jirani, ana Duka lake, anasali kama kawaida, anatoa Sadaka, Lakini anashindwa kuona nini maasi yake.
Sote tumejificha kama huyo Jirani, kwa sababu Jirani alikua na udhaifu mkubwa, vita vya kujizuia na hili jambo la mwanzo vilimshinda, akichukua watoto wa watu mitaani kwa siri na kuzini nao, akichukua wake za watu na kufanya nao mapenzi, Jambo hili la (1)(Sex)lilimuhujumu kabisa ikawa kwa Binaadamu wenzie wasomjua wanamuona Mcha Mungu kwa kuwa hatoki katika Nyumba za Ibada na kutenda mambo mema,na ana simamisha Sala sana, lakini usiku ukiingia anageuka (Dracula). Na hivi ndivo wengi tunavoishi upande (Sinner) na tukigeuzwa upande wa pili (Saints).
Sex ni adui wetu mkubwa wa kutuzuilia kuipata (Pepo) ya Mwenye enzi Mungu, Ni tendo lenye kuichafua Roho, na kukaribisha maradhi ya Mwili na Akili yake ikiwa itatumika sivyo na maamrisho kama yalivyoteremka kwenye sura ya Muuminun aya ya 5 na 6. وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَـٰفِظُونَ.
"Na wale ambao wanalinda Tupu zao"
Vinatakiwa kulindwa Vipande vya nyama hizi kwa ulinzi wa hali ya juu kabisa, kwani ikiwa kitatumika kwa njia nyengine isiyokua ya kisheria kipande cha nyama hichi kitaleta madhara makubwa kwa muhusika na jamii nzima kwa jumla, kitapita njia zisizo amrishwa na kufanya uharibifu mkubwa kama vile wa kuacha kizazi kisichokua na familia ya upande mmoja, Muhusika atakua akisambaza maradhi kutoka huku kwenda kule, atakua akiacha maumivu makubwa kwa wale anowatekeleza, Ikiwa jambo hili halikuwekewa ulinzi linakufukuza kabisa katika enzi ya kumkumbuka Mollah wako, ndio maana likaambiwa jambo hili limeruhusiwa lakini ila kwa.
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٲجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَـٰنُہُمۡ فَإِنَّہُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ
"Isipokua kwa wake zao au kwa(Wanawake)wale iliyowamiliki mikono yao ya Kiume(Kulia)Basi hao ndio wasiolaumiwa.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment