Sunday, November 16, 2014

URADI WA DHIKR YA (KUMTAJA MOLLAH) PART 3

Asalaam Aleiykum

Nini Uradi?
Uradi ni nyenzo au (Method) ya kuinyanganya (Mind)Akili uwezo wake wa kukutawala kama ifanyavyo hivi sasa, Ndio walo wema walotangulia wakafanya njia hii ya kuidunda(Kuipiga)Akili kwa Majina ya Mwenye enzi Mungu, wakafanya hivyo kwa kutumia mambo matatu (Body, Mind, and Soul)kwa hiyo msipite mkawakejeli(Kuwafanyia mzaha) wazee kwa kushika (Tasbih mikononi)Tasbih maana yake ni (Body) inakumbuka na (Mind)kazi yake inahesabu na (Soul)Roho inataja na hakuna maana nyengine isipokua ndio hiyo ya Uradi.
Na yakijumuika na kukusanyika pamoja mambo hayo matatu katika huo Uradi wa Kumtaja Mollah kwa njia ya marejeo (Repitition)utaanza kuona zile fikra za Maimuna au Muumin, au za mpira na nyimbo zinaanza kutoweka kidogo kidogo mpaka unafikia wakati hakuna tena mawazo au fikra za kipuuzi katika (Mind)Akili yako ila linabaki jina la Mollah wako. 
Na ukifikia hatua hiyo inakua wewe sasa uko tayari kwenda (Beyond name to the Nameless)Utakuwa wewe tayari ushafika kwa wale wenye kutajwa katika sura ya (Al-Imran aya ya 191)
"ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَـٰمً۬ا وَقُعُودً۬ا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَڪَّرُونَ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَـٰذَا بَـٰطِلاً۬ سُبۡحَـٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ"
Ambao humkumbuka Mwenye enzi Mungu wakiwa wima(Wamesimama)na wakikaa na wakilala, na hufikiri Umbo la Mbingu na Ardhi(wakasema)Mollah wetu hukuviumba hivi bure, Utukufu ni wako, Basi tuepushe na adhabu ya Moto.
Na wewe sasa utakua unamtaja Mollah wako mpaka ukiwa usingizini, akiwa kuna Mtu analala na wewe basi anaweza kusikia kukoroma kwako kunataja (Laa illah Ilah Allah).
Na hizo ndizo faida za Uradi umeshindwa kwenye akili sasa shuka moyoni uwe kama hao walotajwa katika hiyo aya, na utaanza kuona kwa mara ya mwanzo moyo unashukiwa na mapenzi, wakati wote utakua furahani ukiwa sokoni au barazani wewe utakua unamtaja Mollah wako, jaribu japo wiki uone faida yake, na ukijaa mapenzi ya Mollah wako ndio unapanda kwenye daraja nyengine ya Imani unaingia katika kundi la wale walotajwa katika sura ya (Israa aya ya 107)
"قُلۡ ءَامِنُواْ بِهِۦۤ أَوۡ لَا تُؤۡمِنُوٓاْ‌ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهِۦۤ إِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡہِمۡ يَخِرُّونَ لِلۡأَذۡقَانِ سُجَّدً۬ا "
Sema Iamini au Msiamini(Hiyo Quraan) Hakika wale walopewa Elimu (Zamani)kabla hii(ya Quraan)wanaposomewa(aya zetu)huanguka kifudi fudi wanasujdu.
Huo ndio Uradi , hivyo ndio ukishiba Jina la Mwenye enzi Mungu utakavyokua, japo kwa sasa utaona haya kwa kudhani watu watasemaje lakini utasujudu mayoni kama vile afanyavyo mgonjwa, Huo ndio Uradi udumishe ukupele (Beyond) hiyo ndio itakua dawa yako ya kuondokewa na Dhiki moyoni mwako na pia katika maisha yako. Ukitaka soma kwa sauti au kimya kimya kwenye moyo wako yote ni sawa. Sio Haramu wala hukosei.

No comments:

Post a Comment