Sunday, November 9, 2014

MUANGAZA WA ROHO PART 3

Asalaam Aleiykum

Kuna kitu ambacho ni muhimu sana kukijua ndio maana unahimizwa kukumbuka mauti, kwanini ikawa Mauti kwa sababu Mauti yanachukua kila kitu isipokua kitu hicho ambayo ndio hiyo Roho,ndio hiyo wewe ambaye sasa hivi unaisoma habari hii, Na siri ya kukumbuka Mauti nikuwa kila ukikumbuka Mauti unapunguza dhanmbi, na dhanmbi zikipungua inakua rahisi kuijua Roho yako(قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّٮٰهَا)"Bila shaka Amefuzu aliyeitakasa(Roho yake) .
"Wanakuuliza habari ya Roho Sema" 
Tutizame sasa hili neno Amri linatokea wapi, Neno Amri ni tafsiri ile ile ya Majaala, na tutizame hili neno la kujaaliwa ni Amri hii inayopitishwa na Mwenyewe Mwenye enzi Mungu kama alivyosema kwenye aya nyingi mimi nitazitumia mbili ili zipate kutufungua macho tuweze kuona Muangaza wa Roho.
وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّ‌ۖ 
"Na tukajaalia(Kufanya)kwa maji kila kitu kilicho Hai" 
Kitu chochote kilicho hai kimefanywa kwa Maji, hapo itakuonesha vipi vyengine ambavyo vikiwa havipo hai vinavyokua, mtizame Maiti wa Binaadamu au Mnyama akisha kufa anakuaje dalili ya mwanzo anaanza kuoza na (source)ya maji inakatika katika mwili huo ndio maana tunamwita Maiti na ukimfufua utaona keshakauka,maji yamemalizika, kwa hiyo katika Ulimwengu huu tumeoneshwa vilivyo hai na vilivyokufa, kimoja kinategemea maji na chengine maji yashatoweka, chochote kile kisichotegemea maji kinakua Maiti, ile amri ya maji kuwepo kwenye kitu hicho imeshakatika, kumbuka vyote vinaishi ila kimoja katika uhai na chengine katika umauti, Na hiyo Roho yako inaishi katika sehemu hizo zote mbili,kwa hiyo kama huamini kufufuliwa zingatia sana habari hii nilokupa halafu uifanyie kazi. Katika daraja hilo la maisha ndipo ilipo Roho yako kwa amri ya Mwenye enzi Mungu.
"Wanakuuliza nini habari ya Roho sema" Na waambie kwa Amri hiyo hiyo ya kujaaliwa na nyinyi mnapewa vitu  muhimu sana navyo ni sura ya As-Sajda aya ya 9.
ثُمَّ سَوَّٮٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِۦ‌ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَـٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَ‌ۚ قَلِيلاً۬ مَّا تَشۡڪُرُونَ
Kisha akamtengeneza(Kumuumba) na Akampulizia Roho yake, na akakupeni masikio na macho na nyoyo, ni kidogo tu shukurani yenu.
Baada ya kwisha kuumbwa ukapuliziwa Roho itokayo na yeye Mwenyewe Mwenye enzi Mungu, ndio maana nikasema safari ya kutaka kuijua Roho ni kurejea kwa Mollah wako, ndio maana nikasema ni safari ya miujiza na yenye kutisha, ikapulizwa hiyo Roho katika hiyo (Body)yako, kwa hiyo Roho inaishi katika mwili wako lakini haikamatani na mwili wako, ndio maana ukaona mwili unafanya kazi zake pasi kuingiliwa na Roho,Lakini Roho ndio yenye ku (Control)huo mwili kwa kuwa wewe ni Khalifa wa huo mwili na hii Ardhi, halafu ukapewa hii amri au Jaala ya kuona na kusikia, Ifikiri sana habari hii ya kuona na kusikia, ina mazingatio makubwa katika muangaza wa Roho, huu ni uwezo wa kutoka kwa Mollah wako ndio maana utaona wakati wa usingizi wako amri hii unaondoshewa kwenye (Deep sleep)ukirejea kwa Mollah wako kikamilifu, na wakati Mwengine unakua nayo amri hii ndio unaona hizo ndoto na kusikia sauti, Ni lazima upewe viwili hivi adhimu ili upate uhai kwa ukamilifu na kama huna viwili hivi bado Roho yako iko hai lakini imenyimwa amri hii(Jaala)ya Muumba wako, ukapewa na huo Moyo ili uweze kujua, kumbuka macho ni kuona, masikio ni kusikia, halafu ukapewa na huu Moyo ili uwe na uwezo wa kujua, kupenda, kufahamu na hekima ya kuweza kuijua Roho yako. Kwa sasa hivi huwezi kujua moyo ulokusudiwa hapa mpaka ukifika mbali katika hiyo safari yako ya (Sipiritual Journey) ndio utajua alaa kumbe moyo una kazi mbili, na hii ya pili ndio ilokusudiwa katika Muangaza wa Roho.
Wanakuuliza nini habari ya Roho sema, ni jambo lilohusiana na (Amri) ya Mollah wangu, Na wala hamkupewa elimu isipokua kidogo.
Hakukataa Mwenye enzi Mungu wala hakuzuia mtu kutaka kujua nini hiyo Roho,ili kasema Elimu mliyopewa ni chache(Kidogo) basi mtu na aitafute asaa anaweza kupewa elimu ya Roho akaijua na ukiijua Roho yako, utapata ufahamu vipi ukawa wewe Khalifa katika Ardhi hii, usisubiri mpaka siku ya kufa ndio ukaijua Roho yako, anza sasa hivi kwa kujitakasa na kuusafisha moyo wako utaipata elimu hiyo, kumbukuka imetolewa kidogo lakini haikuzuiliwa kutolewa, Elimu zinazidi kutolewa, tunaendelea kuvumbua mambo,,  na sote siku ya kufa tunakutana na roho zetu kwa hiyo hakuna jambo la kuogopa ima usubiri siku ya kufa au anza sasa hivi, na ukianza sasa hivi basi unakwenda (Beyond death),hiyo ndio maana "Ya Ewe Mja wangu mwema Rejea kwangu ukiwa umeridhi na kuridhiwa"(Operation ya Mauti inaendelea wewe unaangalia, unajijua sina cha kuhofia, mimi Roho narejea kwa yule alonileta, na wala sina khofu tena ya Operation hii), lakini kwanza lazima usafishe machafu yako, omba maghfira kwa wingi ili uitakase Roho yako,ikiwa safi hapo utaona Muangaza wake, utaona Muujiza wake, fanya safari hii muhimu ya Muangaza wa Roho na ukipata Muangaza huu wewe ushafanikiwa, hukai tena ukalinda mali ya Ulimwengu huu, hakuna chochote kitakacho kudhuru na utakua karibu sana na Mollah wako na hiyo ndio maana ya, nasi tukaribu naye zaidi kuliko huo mshipa wake  wa shingo
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِيدِ.

No comments:

Post a Comment