Asalaam Aleiykum
Jambo la pili nii hizi Hamaki tulonazo.
Sasa tunaingia kwenye Sumu ya maangamizi ambayo kama utakunywa sumu hii basi wewe kwa hiyari yako umejiharamishia Pepo. Hamaki ni madhara makubwa kama utaitizama kwa undani, magonvi yote yanaletwa na hamaki, chuki zote zinatokana na hamaki, Hebu tuliangalie tendo hili la hamaki mwanzo wake wapi.
Hamaki ni tendo linalotokea ndani ya mwili wako ambalo ni (Energy)maalum inayoripuka kutokana na kitendo cha nje kilichofanywa na Mtu mwengine, Nini kafanya? kajeruhi (Chemical) za (Kiburi) katika Akili yako, Na Ufalme wako wa (Kiburi)ukiguswa kidogo tu hata na mtoto mdogo jiangalie unakuaje, ukikataliwa na mwanamke jiangalie unakuaje, ukinyimwa cheo tizama unafanyaje, ukigombana kitu kidogo angalia huzungumzi milele pengine na ndugu zako.
Sasa nini kimetokezea umeikera ile (Energy) yenye kukupa huruma na upole na kuipeleka kwenye Akili kwa njia ya kasi ambapo ndio inazaa Hamaki, unafanya mambo ukiwa umelala usingizi, inakwenda kukaa (Energy) hiyo kwenye Akili yako na kila mara huwa inakukumbusha ulivyofanyiwa, hapo tena unaondoka na visasi, unaondoka na chuki za uharibifu hupumziki na wewe mpaka ulipize japo kwa siri kwa lile tendo alofanya fulani siku ile, utakwenda kutafuta ushirikina, utatuma watu ili wamdhuru, utapigana vita, utapoteza maisha ya watu kwa kitu kimoja, au utaanza kutapakaza habari zisizo za kweli ambazo zinaleta madhara kwa muhusika, hayo yote unayafanya kutokana na Hamaki zako,na ukienda safari hiyo unasahau kabisa kuwa kuna Mollah wako, unafanya hasira za kudumu hali yakua ungesubiri kidogo au uka kaa chini ile (Energy)irudi sehemu yake badala ya kukupeleka kwenye uharibifu ingekupeleka Peponi, kutokana na (Energy) hiyo hiyo zinazaliwa huruma za mapenzi na upole, lakini ukiifata wakati imekwenda kichwani hiyo ndio inakua sababu ya uharibifu na kukukosesha Pepo.
Jambo la Tatu Kupenda Mali.
وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّ۬ا جَمًّ۬ا
"Na Mnapenda Mali Mapenzi mengi"(Makubwa)
Mnapenda majumba, Mnapenda magari, Mnapenda anasa za dunia, Mnapenda viumbe wenzenu Na Mali zenu hususan Pesa, zinakushughulisha kwa mapenzi makubwa, unasahau kabisa kama umeumbwa, unasahau kabisa kama unatakiwa ufanye Ibada, unatakiwa ufanye wema na Ihsan, unasahau kama mauti yanakunyanganya kila kitu na kukuacha mweupe, nini unafanya, unahesabu mali na kushughulika na watoto, unanyanganya huku na kule, uko tayari wende motoni ili wengine wastarehe na kufurahi kwa chumo lako, jiulize wewe unapata faida gani kwa shughuli hizo.
Angalia vipi mipango ya kazi na shopping ilivokuzonga, Fulani atavaa nini, leo tutakula nini, nani kenda nani karudi, harusi ya fulani iko lini, pesa ngapi zimetumika, kesho nani anacheza mechi ya mpira, kipindi changu cha Tv kinaanza saa ngapi, (Wassup)mbona sijapata (Msg) hivi ndivo tabia zetu za kila siku zenye kutusahaulisha mambo ambayo Mollah wetu katuamrisha ambayo ni ya kumkumbuka yeye na kufanya Ibada. Ukiangalia Mambo hayo yote Matatu ni yanokupelekea nje mja wewe, Maskini umekaa dirishani unashughulika na mambo ya Nje wakati huku ndani ya kifua chako, wamejificha (Hurulain)ndani kifuani kwako imejificha (Furaha ya Imani na Huruma na mapenzi) na humo ndani ya kifua chako kumejificha (Hazina) kubwa lakini wapi,, unashughulika na mambo ya nje kupita kiasi mpaka yanakua sababu ya adhabu yako, yanakutesa hapa duniani na unashindwa kujiuliza vipi itakua hali yako huko Akhera uendako. Basi Mja Unatakiwa Ujiulize hivyo uko tayari hapa Ulimwenguni uteseke na huko Uendako pia ukateseke, uamuzi unao mwenyewe, na kama umefahamu anza sasa ili usiikose Pepo ya Mollah wako,na kumbuka hayo yote unayafanya upate raha na furaha, Na Mollah wako kakwambia ukifanya Ibada, utayapata hayo yote na zaidi katika Ufalme wake wa Milele.
No comments:
Post a Comment