Sunday, November 9, 2014

MUANGAZA WA ROHO PART 2

Asalaam Aleiykum

Lakini ukiwa katika wale wachache ambao kwa Ushujaa wanalikabili swali hili la nini Roho?, Basi wewe ndio katika wale wanoanza ile Safari ndefu yenye kutisha, yenye miujiza na mambo ya ajabu, Safari yenyewe ni ngumu lakini inaendeka. Kinachotakiwa katika safari yako hii ni yakini katika moyo wako kuwa sasa nachupa nimeamua kutumbukia kisimani kitachonikuta sawa lakini lazima nijijue mimi nani.
Na mwanzo kabisa ukiamua kuchupa kuanza safari hii na kuuliza nini Roho?ina maana ushafanya (Tafauti)baina yako na huo Mwili(Body)zishakujia fikra kuwa wewe sio huu Mwili, kuna kitu chengine ambacho unataka ukijue, hapo tena ndio unaanza hiyo(Sipiritual journey)ambayo imeitwa safari ndefu.
"Wanakuuliza habari ya Roho sema(Waambie)" wala hakuna makosa mtu kutaka kujua nini Roho, cha muhimu kwanza kabisa uelewe kuwa hata hiyo (Body) Mwili wako si mali yako, ni zawadi uliyopewa nusu kutoka kwa Baba yako na nusu nyengine kutoka kwa Mama yako, halafu tena ndio unaendelezwa Mwili wako huo kwa njia ya chakula, sasa ukiwa huu mwili ni hicho chakula mimi nilobakia nisokua chakula mimi ni nani?, Nimetokea wapi, na wapi ninapo kwenda. Nini habari yangu mimi siku ile nitakapozimika,nini kinatokezea?.
"Wanakuuliza nini habari ya Roho Sema" uwaambie hakika ya hiyo Roho ni (Amri)ya Mollah wangu, ndio maana utaona mambo yote yenye kuhusiana na Roho unayakabili peke yako, umeshapata kujiuliza nani huyu Mke wangu au Mume wangu, nani hawa watoto wangu, wote hawa wametokea wapi, mbona naona sote sisi kama wageni tulokutana katika Ulimwengu huu, Jee hii ndio ile maana ya watoto zenu na mali zenu ni adui kwenu? unainza safari hii kwa unyenyekevu mkubwa kabisa, huku ukijua kumbe  katika mambo ya Kiroho niko peke yangu, na kila kitu nitakikabili peke yangu, hayatonifaa mali wala watoto ila lazima nirudi kwa Mollah wangu nikiwa safi, sasa Nani huyu anaye Rudi?
"Wanakuuliza nini habari ya Roho Sema" Waambie hiyo Roho ni kwa ajili ya (Amri) ya Mwenye enzi Mungu, Neno Amri inafaa tulizingatie sana tafsiri ya neno hili, Watu wengi wanadhani au wanashindwa kutafautisha baina ya Amri na maagizo, Amri ni tendo lisilopingika wala kubadilika isipokua mpaka atake huyo Mwenye kutoa Amri Mwenye Enzi Mungu mwenye Ufalme wa Milele.
Hizi zenu mnazotoa nyinyi si Amri sababu amri haipingiki, hayo yenu ni maagizo ndio maana kuna wakati mtu anakwenda kinyume na kiongozi au bosi wake, kwa kuwa hayo ni maagizo hawana hakika nayo ndio sababu pakawekwa washauri kuwasaidia kupitisha hayo maagizo. Ukilizingatia vizuri hili neno Amri litakusaidia pakubwa katika safari yako hii ya kutafuta Muangaza wa Roho.
Waambie habari hii wala usiwafiche kuwa imehusiana na Mwenye enzi Mungu na yoyote yule Mwenye kutaka kuijua habari hii anarudi kwa Mollah wake, Na kurudi huku ndiko kunakujulisha ukajua kila kitu katika Ulimwengu huu kinatii hiyo Amri ya Mwenye enzi Mungu, Mpaka huo Mwili wako (Body)unatii Amri hiyo, Moyo unapiga kwa kutii amri hiyo, Ini linasafisha damu kwa amri hiyo, damu inasambazwa kwenye Mwili kutokana na amri hiyo ikitimizwa na hewa itokayo nje unayovuta bila ya tabu wala kuitaka au kuikataa, ni katika mazingira ya kuitii Amri itokayo kwa Mollah wako, Mwili unahisi njaa unakula chakula, ikisha kinasagwa kwa kutii Amri hiyo, ikisha mwili ukichoka unalala hayo yote sio wewe, sasa wewe ni kitu gani?
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment