Sunday, November 9, 2014

MUANGAZA WA ROHO PART 1

Asalaam Aleiykum

Leo nakuomba safiri na mimi ili tuishi katika aya ya 85 ya sura ya (Israa) tupate kuhisi Muangaza wa (Roho)tujue ikoje taa yake.

وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلرُّوحِ‌ۖ قُلِ ٱلرُّوحُ مِنۡ أَمۡرِ رَبِّى وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ إِلَّا قَلِيلاً۬
Na Wanakuuliza habari ya Roho, Sema Roho ni Jambo lilohusika na (Amri)ya Mollah wangu. Na nyinyi hamkupewa katika elimu isipokua kidogo (Hivi).
Kumbuka kila mmoja wetu anauliza swali hili, ikiwa haulizi kwa mtu anajiuliza yeye mwenyewe, nini hasa hii Roho? kwanini likaja swali hili, lazima (Deep) katika nafsi zetu kuna Kiu(Thirsty) ya kutaka kujua nini hii Roho? kweli inaishi maisha, na kila mtu anauliza swali hili kutaka kujitosheleza kwa kuamini hakuna mwisho ila kuna uwepo wa kudumu milele, hamu kubwa na shauku Mwanaadamu imemkamata kulijua hili, Na kila mara japo ukilisukuma swali hili lisirudi ndio kwanza linazidi kukuandama.
Sasa ufanye nini? ndio kila mara mtu inabidi aende kuchungulia katika kisima hichi cha fikra ili apate kuona kama kuna maji apate kukata kiu yake ya kuijua Roho. Lakini kawaida ya kisima inataka ufanye kazi kupata kuyaona hayo maji kama yapo, sababu kisima ni kikubwa sana, hata ukipata huo Muangaza ukayaona maji inabidi ufanye jitihada ya kuyachota maji hayo.
"Wanakuuliza nini Habari ya Roho"
Napenda utambue waulizaji wa habari hizi si watoto au vijana ni mara chache sana wenye umri wa rika hilo kuulizia habari kama hizi,Waulizaji wakubwa wa habari hizi ni wale walofikia Umuri wa makamo au rika ya uzee. Pia napenda kukufahamisha waulizaji wako wengi lakini wafatiliaji ni wachache sana, Na sababu kubwa safari hii ya uchunguzi wa kujua nini Roho inatisha, ni safari mja unatakiwa uende peke yako, huna mshirika, na hivi sasa wakati ndio umefika, pengine watoto wameshakua na kuondoka nyumbani, Majumba umeshajenga yamemalizika, Mapesa (Bank)yamefurika, huna tena la kufanya, hakuna la zaidi, sasa swali hili ndio linakuja kila mara nini Roho?.
Na ukiona swali hili linakujia mara kwa mara basi elewa bila shaka limegusana na Mauti(Sio kwamba unakufa lakini ni njia moja ya Ulimwengu huu kukupa habari za hiyo siku ya siku). kwa hiyo ukiwa katika wale walo wengi ambao wanaogopa swali hili hapo tena utaanza kutafuta vitu vya kukusahaulisha, utaanza kukimbilia senema(Cinema)mara kwenye ma(Disco)hukosekani, kwenye Taarab wewe unakua wa mwanzo kuingia na wa mwisho kutoka, na kila sehemu inayokufanya wewe usahau habari hii wewe ndio unakua (Kinara wake)ili upate nafasi ya kusahau kuijua kadhia hii ya Roho.
Endelea part 2



No comments:

Post a Comment