Asalaam Aleiykum
Anahadithia Sayyidna Abu Huraira r.a "Akisema" Bwana Mtume s.a.w kanifundisha Elimu mbili ya kwanza nimekupeni, lakini ningekupeni hii ya pili mngenikata kichwa. Hayo ni maneno ya Sahaba wa Bwana Mtume s.a.w ambaye yeye kaenda hiyo safari kubwa ya (Mystical Journey)inayoitwa Miraji.Sura ya Israa aya 1.
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
Utukufu ni wake yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku kutoka msikiti Mtukufu wa(Makka)mpaka Msikiti wa mbali wa Aqsa(Bayyitul Muqadas)ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumuoneshe baadhi ya Alama zetu, Hakika (Mwenye enzi Mungu)ni Mwenye kusikia (na) kuona.
Kweli angekatwa kichwa kwa sababu ee hivi leo kuna baadhi ya watu wamo ndani ya Uislam wanaipinga safari hiyo kwa malumbano, seuze hayo mambo yalioko huko, kwa hiyo kuwa na hakika elimu hizo zipo na ziliwahi hata kuandikwa baadhi yake kwenye vitabu lakini maskini vikachomwa moto vyote mwanzoni mwa miaka ya 70 na (Library zote kufungwa), na hiyo ndio ikawa hasara ya (Generation)hii kunyimwa elimu hizi za Ajabu.
Imebakia sasa hivi elimu zinazofahamika ni zile za wazi, kwa hiyo umefika wakati sasa japo kuashiria, angalau kukumbusha kwamba hizi elimu zilikuwepo, zipo na zitaendelea kuwepo na pengine (Generation) ijayo itaweza kufatilia kwa undani. Kwani kutokana na aya hii ya sura ya (Fussilat 53)
"سَنُرِيهِمۡ ءَايَـٰتِنَا فِى ٱلۡأَفَاقِ وَفِىٓ أَنفُسِہِمۡ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّۗ "
Tutawaonesha(Ukweli wa)Maneno yetu haya katika nchi za mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.
Kutokana na maneno hayo inaonesha wazi mambo makubwa ya ajabu yasokwisha yapo, yanaendelea kuvumbuliwa kwa njia ya nje na ndani katika fani zote za maisha haya ya Ulimwenguni, Lakini kwa (Mystic) inakua tabu kuyaandika au kuhadithia kwa kuwa ni ya ajabu na hayana mfano, kwa hiyo (Mystic) anakaa kimya na kuashiria tu kuna hichi na kile, ili uende ukaone mwenyewe.
Sasa Baada ya kuizungumza Dhumuni la darsa yetu hii sasa wacha tuanze safari yetu hii ili tupate angalau chembe ya muangaza wa Elimu hizi za Ajabu. Basi tuanze na ajabu ya mwanzo iliyomo ndani ya kitabu hichi cha Quraan, Kumbuka kitu kimoja vitabu vyote unasoma unavimaliza lakini hichi cha Quraan hukimalizi, unaambiwa kisome daima, Jee huoni Ajabu kwa Jambo hilo, kwanini ukisome ikisha ukirejee tena na tena mpaka mwisho wa umri wako?, mbona vyengine ukimaliza inakua basi, kwanini hichi tu ndio uendelee?.
Utajibiwa Swali lako hilo na baadhi ya aya za Quraan ili upate muongozo na mimi nita (Share) ajabu hiyo na wewe ili upate kuijua kwa vizuri.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment