Asalaam Aleiykum
Ajabu yenyewe inaanzia katika maneno haya ya aya ya 5 na 6 sura ya (Muzzamil)"إِنَّا سَنُلۡقِى عَلَيۡكَ قَوۡلاً۬ ثَقِيلاً ""hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito""إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِىَ أَشَدُّ وَطۡـًٔ۬ا وَأَقۡوَمُ قِيلاً ""Hakika kuamka usiku(Na kufanya Ibada)kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno (yake) yanatua zaidi.
Hapo pametajwa jambo la ajabu, umetajwa moyo ikatajwa kutua kwa maneno, Maneno yanatokea wapi?, kwenye Akili, Moyoni yanakwenda kupewa tafsiri au maana, ndio maana ukaambiwa nyanyuka usiku, kwanini ikawa usiku? Kwa sababu umelala na Akili isha (Process) mambo yanotokea mchana wote, Unaamka ukiwa Mweupe, unasoma kitabu cha Mwenye Enzi Mungu kwa utulivu wa hali ya juu pasipo kuwa na mawazo mengine, hapo tena neno linaanguka moyoni na likianguka tu wakati umepata utulivu ndio unapata hicho kitu kinaitwa (Awakening) na ukipata hali hiyo japo kwa aya moja basi ushaonja tone la (Mysticism) na unabadilika daima, aya moja inakufanya utembee kwenye Bahari, aya moja itakufanya uwatibie wenzio Maradhi yao, pamoja na wewe mwenyewe.
Na kwanini isiwe hivyo na wakati imetajwa ndani ya Quraan kuwa huu ni muongozo na ponesho la maradhi yaliyomo kwenye vifua vyenu, na kifua kina mambo mengi, husda imo humo, kutokuamini kumo humo, Ini limo humo, Figo limo humo, lakini kuupata huo muongozo na ponesho lenyewe linahitaji huyo msomaji yupo kwenye daraja gani.Maskini leo wako wapi wale (Mystic) walokua wakiyasomea maji kama unaumwa tumbo linapoa, kama Mwanamke hazai anapata uja uzito, Ndio maana ukatajwa Usiku ndio wakati bora wa kutokea tukio hilo, "Hakika tutakuteremshia maneno mazito".
Sasa nini habari ya wale wasojua kusoma au wanajua lakini hawana nafasi ya kusoma, wao wanaambiwa Al-Araf (204)
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na Itakaposomwa Quraan isikilizeni na nyamazeni ili mpate kurehemewa.
Kwanza isikilize halafu kaa kimya, yametajwa maneno mawili ya mfano mzuri sana, kwanini usikilize? kwa sababu wewe hufanyi yote mawili, pengine inasomwa wewe unasikiliza sauti ya msomaji badala ya Quraan, na huku Akili yako inatizama labda videvu vya Sheikh, au kakosea Nun au hajatia shada na huku maskini unakosa kitu adhimu kinakupita cha Rehma ya Mollah wako nilichokitaja hapo juu, kwa hiyo ndio unaambiwa sikiliza ikisha ukae kimya, yaani nje unasikiliza na ndani huna mawazo yanoendelea kwenye Akili yako hapo huenda likatokea hilo tukio la Ajabu.
Pengine aya huenda ikapita na kuupasua hilo jipo la fahamu ukabubujikwa na machozi bila ya kujielewa, Ndio maana mnaambiwa sikilizeni mawaidha asaa yanaweza kukubadilisha, Lakini inategemea msomaji na huyo msikilizaji. Ama kwa wale wanotaka kushuhudiwa wao waisome Alfajiri, (Angalia katika Darsa yangu ya kushuhudiwa na Quraan).
Basi Naam yasome maneno haya mazito yaloteremshwa na Mwenye Enzi Mungu ambayo Mwanaadamu hujui ndani yake kuna Ajabu gani, Soma upate kujua kwanini Jahazi ya Nabii Nuhu a.s ilikua ikenda na kusimama kutokana na maneno ya (Bismillahi Majriha wamursaha), hayo ndio baadhi ya maajabu machache niloyataja yaliyomo kwenye Quraan, yapo mengi lakini muda wetu hautoshi kuyazungumza yote kwa njia ya maandishi, na Mifano ya maajabu hayo ni kama vile kuzuia gari isiondoke, ukasoma mpaka ukafanya Treni ikusubiri, Ndege isiruke nk, najua mtashangaa ndio maana nikaita Elimu za Ajabu na hayo ndio mambo ya (Mysticsim).
Sasa tuingie katika Elimu ya (Kuruka au Kupaa) sisemi hivi mtu akaanza kuniuliza(Method) ya kufanya, mimi nazungumza kwa njia ya Elimu, wewe una hiyari yako kutafuta(Method) ukija kukwama kwenye Miti mimi sichukui dhamana, wapi imepatikana Elimu hii tutaendelea wiki ijayo kwenye Part 4.
Shukran.
No comments:
Post a Comment