Sunday, November 16, 2014

URADI WA DHIKR YA (KUMTAJA MOLLAH) PART 1

Asalaam Aleiykum

Kukumbuka kuko kwa aina mbili, aina ya kwanza ya kukumbuka ni kwa njia ya kuona, na aina ya pili ni huko kusikia au kutaja ambacho ni kitendo kimoja kisichokua na tafauti na kuzungumza, kwani njia utaratibu ni uleule wa kusikia sauti ndio maana hata huyo mzungumzaji lazima atoe au apate (Gap) ya kuweza kulisikia analo zungumza au sivyo itakua tayari anasumbuliwa na matatizo kwenye Akili yake, (Ndio maana Mabingwa wa maradhi ya Akili wanatwambia tahadhari ukimuona mtu anazungumza sana bila ya kituo, jua huyo ana tatizo fulani na ukilichunguza utalijua).
Japokua kukumbuka ni jambo moja lakini hili la kutaja lina kazi maalum ambayo ndio msingi mzima wa darsa yetu ya leo ya (Kumtaja Allah).
Kabla ya kuanza na ufafanuzi huo napenda nikumbushe kitu kwa wale ambao kwa njia ya kusikia tu wanayapinga mambo bila ya kupata ithbati ya jambo hilo, bila ya kusoma au kufanya uchunguzi unasimama na kuharamisha kitu ambacho hufahamu undani wake, midamu umesikia Fulani kasema jambo hilo halifai na wewe unasimama kidete kulipinga, usifanye hivyo na wewe kwanza lipatie yakini ya kuto kufaa kwake, usisimame ukapinga  na kukanusha kitu usichokua na uhakika nacho.
Kuna kisa kimoja itabidi mnipe nafasi nikieleze ili uwe mfano kwa watozingatia, Kuna kipindi katika Kisiwa cha (Zanzibar) walikuja (Wajapan) kwa ajili ya kujenga Barabara na wakatangaza wanataka wafanyakazi, wakenda vijana wenzangu na walipofika wakaambiwa kila mmoja aandike jina lake, walipokwisha andika yule (Mjapan) akaanza kuita yale majina akaita kama watu kumi yakabakia majina mawili "Na watu wawili tu ndio walobakia""Akaita (Sidilia Adalasi)kimya, akaita tena nani (Sidilia Adalasi)kimya akaendelea kuita lile jina lengine akabaki kijana mmoja kamuuliza wewe jina yako nani, yule kijana akajibu mimi naitwa (Said Bin Abdullah)akampa peni hebu andika jina lako, yule kijana akaandika (Sidilia Adalasi)"Maskini ikawa peke yake (Said Bin Abdullah) ndio alokosa kazi, Basi na wewe (Please)usianze kusimama ukawa unapinga mambo au kukataa Uradi, ukawa unawacheka wale wenye kudumisha utajo huu tukikupa kalamu uandike kumbe na wewe (Sidilia Adalasi) kasome nenda (Deep) jifunze ukisha kujua na kufahamu ndio njoo utuambie sasa nimegundua Uradi haufai.
Pia nataka uelewe kufahamu na kujua ni vitu viwili tafauti, kujua kunatokana na (Experience) na kufahamu kunatokana na hekima(Wisdom)ambayo anakupa Mollah wako, sasa kitizame kisa hichi kilichotokea kwenye kijiji fulani kwenye zama hizo za zamani, "Kwa Bahati katika kijiji kile alikuwepo Mtu mmoja tu ambaye kafundishwa kusoma, ikawa Barua za kijiji kizima anasoma yeye" yatizame mabega yake yakoje yalivyo beba kiburi ya kujiona kumbe peke yake ndie anayejua kusoma""Ikatokea siku moja Mama mmoja akamfata anataka aandikiwe Barua, Akamjibu Mguu unauma, yule Bibi akenda akarudi siku ya pili na kujibiwa tena mguu unauma, akasema yule Bibi leo siondoki mpaka unambie Mguu umehusiana nini na kuandika, akamjibu unajua kile kijiji iendako barua hii hakuna anoweza kusoma (Herufi)zangu mpaka nende mwenyewe" na siri kubwa kumbe alikua hajui kuandika, kwa hiyo kazi yake kuhifadhi yale maneno halafu ndio aende kijiji cha pili na kumwambia huyo alokusudiwa hiyo barua, na kijiji kikiwa mbali ndio lazima mguu utakuuma(umefahamu).
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment