Asalaam Aleiykum
Lakini utapojaribu njia nyengine yoyote ya kuiba zabibu za watu basi ujue utalaumiwa, Kwa sababu njia uliyoifata ni chafu na ina mambo ya kila aina, na ni Mwenendo mbaya kabisa ambao maradhi yake ni magumu kupona, Na pia yana tabia ya kujirejea kwa kuwa yanaishi Akilini na wewe huna uhodari wa kuishinda Akili pamoja na (Ibilis).
Ndio maana ukianza uzinifu ni vigumu kuepuka, inatakiwa ifanyike kazi kubwa sana mpaka utolewe katika mzunguko huu wa mapenzi ya zinaa, Sasa sababu gani ikakupelekea mpaka ukaikosa pepo, sababu zipo nyingi lakini mie nitazitaja hizi mbili ili tupate kuzizingatia, Sababu ya kwanza(Sex)inakushughulisha humkumbuki kabisa Mollah wako, kwa sababu mambo mawili hayo hayakai pamoja moja linalaza na moja linakuamsha, (na mfano unao mwenyewe ukiwa na huyo wa halali wako mke au mume mkitaka kufanya tendo la ndoa ukiambiwa tutie udhu tusali Rakaa mbili basi hamu yote hapo hapo inaondoka)Kwa sababu unakua ushaamshwa, ushatolewa katika hali yakua mnyama umerejeshwa kwenye ubinaadamu, sasa jitizame huko uendako usikoambiwa tia udhu unakuaje, Wewe na mnyama hamna tafauti.
Unalala ukikoroma ndio maana hutaki mambo ya dini, huwezi hata kusali, kutokana na tendo unalo jishughulisha nalo ni la kukatazwa, na chochote kile unachokatazwa kina kushughulisha sana, wewe chunguza pahala uambiwe usichungulie uone utakavo hangaika kutaka kujua kuna nini hata nisichungulie?.Kwa hivyo tulivyoambiwa Zinaa ni haramu tumeumia, inafikia ukisikia muazini una hamaki, yana kushughulisha mambo haya mpaka kufikia Utu uzima bado mambo yamekuganda Akilini, Tahadhari sana huku mwili ushachoka, maradhi yashawasili na wewe umeshakua Muflis huna tamaa tena ya pepo.
Na Jambo la pili ni ule uharibifu unopita kuufanya, unaumiza Roho za Binaadamu wenzio, Unawacha kizazi kisichokua na Familia, basi kama wanavoteseka hao binaadamu wenzio jua na wewe maandalizi ya Adhabu yanakusubiri bila ya shaka yoyote na hilo pekee linakutosha kukukosesha pepo.
No comments:
Post a Comment