Sunday, February 8, 2015

ALAMA TANO ZA ROHO PART 3

Asalaam Aleiykum

Vipi Alama hizi zinakujulisha itabidi ufanye juhudi Mwenyewe ya kugundua hicho kilicho kusudiwa, Alama zinaashiria kwa mfano huu!!, Wakati ule unapotizama unajua nani anaona?, Na kwanini nikataja kutizama na kuona? Kwa sababu kutizama ni (Action) na kuona ni (Attention)"Mfano" kwenye (Match) ya mpira unatizama wachezaji wote lakini (Attention) yako iko kwa yule mwenye mpira.
Na Kusikia hali kadhalika unasikia kila kitu, mtoto analia, gari inapita, ndege wanaimba, lakini (attention) yako yote iko kwenye (Nyimbo)yako unayosikiliza. Hiyo ndio maana ya neno (Nia) kwa lugha yetu ya kiswahili ambayo pia inahusu mengine yalosalia ya Kugusa na kuhisi(Mfano)ikiwa utapewa Halua unakula na huku unakanyaga msumari jiangalie (attention) yako itahamia wapi, nina hakika itahamia kwenye msumari kwa sababu Roho haipendi machungu, utaacha utamu wa halua ukashughulikie maumivu kwanza, sasa swali la kujiuliza nini hicho chenye kuhama kutoka katika jambo moja kwenda kwenye jambo la pili.
Na Harufu kadhalika mpaka ipatikane (Nia yako ya kunusa) ndio uvute harufu nzuri au sivyo mtu atajitia Udi mpaka apande shetani wewe husikii chochote umezama kwenye (Match) ya mpira au mkutano wa siasa. 
Kwa hiyo kama ushalijua hilo la (Nia) muhimu sasa kuifanyia kazi  nia yako mpaka ikufunulie Miliki yake ya Fahamu na kuijua kumbe hii ndio Roho, Na ukishajitambua hapo tena wewe utakua unaishi Ulimwengu mwengine kabisa wa hicho kitu kiitwacho (Bliss) na (Joy) na (Happiness) utakua Mfalme wa (Body) yako unatawala (sense) zote za kuona, kusikia, kusikia, kunusa na kuhisi.
Lakini kwa hivi sasa usihangaike bado hujawa mfalme, umo bado unatumikia hizo Alama za macho, unatumikia kusikiliza, unatumikia kugusa, unatumikia kunusa pamoja na kuhisi, umetawanyika kila sehemu unataka utumike wewe, hujatulia kabisa mara unazidiwa na kutamani, mara unazidiwa na kutizama, jitizame utaona vipi umetawaliwa na (sense) pengine nyimbo huwezi kuzikosa, labda vyakula vinakutesa, na mambo mengi ya kilimwengu yanakutesa yamekutawala huna uwezo wa kuyatawala mpaka ujigundue, Yakwamba wewe ni Roho na una uwezo wa kuyatawala hayo yote yakafata amri yako. Kumbuka zote hizo ni Alama zinaashiria jambo la kuwapo kwa Roho, kwa hiyo ifate alama moja baada ya moja ikupeleke kwenye Ufalme wako ili uwe mtulivu wa kufanya na kuamua mambo yako kwa umakini na hekima ulopewa na Mollah wako, Hiyo nia ndio itakufanya upate utulivu wa sala, kuepuka madhanbi, na hiyo ndio itakayoweza kukunusuru na adhabu na kuipata pepo.
Wacha zifanye kazi zote Alama tano lakini wewe Baki kwenye hicho chenye Umiliki wa hayo mambo matano, (Mfano) Umefunga Sala, wacha mawazo yaje, wacha uso ukuwashe wewe bakia kwenye sura ya (Fatiha) huku harufu zinanukia, wewe yapuuze yote ukiweza kufanya hivyo baada ya muda utajijua kumbe mimi sio vitu hivyo vyote ni kitu Maalum ambacho ukikijua utanyamaza kimya huku ukishangaa maajabu yake.

No comments:

Post a Comment