Sunday, May 1, 2016

MILANGO MINNE YA DHANMBI PART 3

Asalaam Aleiykum

Katika Mlango huu ndio unafanya mambo kwa Ubabe wako wa akili, Unafanya hujuma na Fisadi katika Ulimwengu huu ukiwa umejipa Mwenyewe kidonge cha Usingizi, na Kidonge hichi jambo la mwanzo lina kusahaulisha kuwa wewe umeumbwa na Muumbaji yuko, Unaanza kudhulumu Haki za Watu, unafanya Fitna, unafanya uzinifu na mambo chungu nzima, na  kubwa zaidi unajisahau hata kama unafanya Dhanmbi, ukifikia katika hali kama hiyo unatakiwa uchukue tahadhari kubwa sana, au unaweza kukumbwa na balaa kubwa siku ya kurejea kwa Mollah wako.
Aya imeweka wazi hakuna msamaha kwa yule anoendelea kutenda dhanmbi(Action)mpaka akasubiri keshakua mtu mzima mate yanamvuja mdomoni hawezi kuyazuia tena na anaona mauti yashawasili ndio anasema Mungu wangu sasa nishachoka , jeuri imenisha, sasa nataka unisamehe, hakuna msamaha wakati huo, umri wako wote ufanye jeuri ikisha sasa hivi kwa sababu unataka kunyakuliwa ndio unasema nisamehe, aya imekataa kabisa kwa yule alotenda Dhanmbi au yule anokufa (Kafiri) hataki kumuabudu Mollah wake.
Basi ikiwa ushaijua Milango hiyo Minne na bado una nguvu zako ni bora ukurupuke sasa hivi, jihadhari sana na huu Mlango wa Nne uwe huingii tena, Kiepuke chumba hichi cha dhanmbi ili isije ikakukuta Balaa, na Hilo ndilo Jumba letu la (Akili) lifanyalo kazi yake, kwa wale wenye kufahamu watazinduka na kuwacha kutawaliwa na Akili na mambo yake ya kurejea rejea matendo ya dhanmbi, kumbuka dhanmbi umekwisha zitenda nyingi, ufanyavo hivi sasa ni kuzirejea tena na tena, kwa hiyo kama umefahamu basi zitakie Msamaha kwa Mollah wako na kufanya yalo mazuri, nenda kaingie kwenye vyumba vya mazuri, Kwani matendo mazuri yanafuta mabaya yako, Na utaona kidogo kidogo Mollah wako anaanza kukupa furaha na afya njema, pia na tahfif na ziada katika riziki zako. Mollah wetu tujaalie yaliyo mazuri na uturuzuku yalo mema.

No comments:

Post a Comment